Ujumbe wangu wa wadada leo jumapili!

Ujumbe wangu wa wadada leo jumapili!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Habari zenu ........

Natumai ni wazima kwa wale ambao ni wagonjwa poleni sana na nawaombeeni mpone haraka

Kuna jambo ambalo limekuwa linawasumbua sana wadad wengi ambao wako kwenye mahusiano a vijana,jambo hilo ni kuwa wadada wamekuwa wakiingia kwenye madhila makubwa kwenye mahusiano yao na kujikuta wakijilaumu sana na wengine kujutia mahusiano yao

Madhila ninayoyazungumzia hapa sio mengine bali ni ujauzito

images


Kuna binti mmoja alipewa ujauzito na kijana mmoja na mara binti huyo kujua hilo aliamua kumwambia kijana huyo,baada tu ya kumuambia tu mawasiliano na kijana yalianza kupungua na hatimae kwisha kabisa na binti akaachwa na ujauzito.Binti alijaribu kumtafuta kijana lakini hakufanikiwa kwani alikuwa akimkwepa mara kwa mara

Binti aliamua kuitoa mimba na bahati mbaya alipata matatizo sana kwa kuugua wiki 2 bila msaada wowote ule lakini bahati nzuri alipona

Matukio ya kutelekezwa wasichana huku wakiwa na ujauzito au kutelekezwa kwasababu ya kupata ujauzito ni mengi sana na yameharibu sana maisha ya mabinti wengi sana.Kipindi kile ambapo binti alipokuwa amepata ujauzito na shule kuishia hapo wengi sana walipata hasara na wazazi pia kwani mabinti wengi sana walifukuzwa shule

Napenda kuwaambia tu kuwa wale ambao wanasoma ni bora wakaacha kabisa kushiriki ngono maana hao mnaojidai mnawapenda ni kujidanganya tu,hakuna cha upendo wala nini na hao wapo kwasababu ya kuwaharibia maisha yenu tu.Kama kuna kijana anajidai anakupenda mwambie asubiri umalize masomo yako ndipo mengine yaendelee,kama hataki mkimbie kama vile umeona mnyama mkali sana

Nyie ambao either mna shughuli zenu au mko katika vyuo,hao wanaojidai wanawapenda kuweni nao makini sana.Usikubali kubeba ujauzito hivi hivi tu bila ya kuwa na ndoa.Anaweza kukuambia maneno mengi sana matamu kumbe hamaanishi hayo anayosema,jihadharini sana na hawa watu

images


Kama utaamua kuzaa basi hakikisha kuwa umejipangia kulea mwanao wewe mwenyewe bila ya msaada wa huyo jamaa,kama ukijifungua na akawa pamoja na wewe mshukuru Mungu na leeni mtoto,lakini nakushauri usizae kabla ya ndoa na kama utaamua kuzaa basi zaa kwasababu unajiweza,kumtegemea huyo anaejidai kuwa anakupenda imekula kwako dada yangu

Kuna wanaume wa ajabu sana kwenye hii dunia,soon tu anajua kuwa umepata ujauzito atakukimbia na kukuacha huna pa kwenda,kuwa makini sana wewe unaesoma hapa

Kama unataka uije kujuta baadae au kuja kulia mwenyewe bila ya msaada basi epuka sana haya kwani wengine wamejaribu hata kujiua kwa kunywa vidonge ili kuepuka hii kadhia

images


Jipende na yapende maisha yako,epuka kuja kujutia na kutamani kujiua kwasababu ya raha au mtu mwingine ambae alikulaghai tu.Kama utamuambia asubiri na akakataa au utamuambia mfunge ndoa kwanza na akakataa achana nae dada yangu maisha yako yana thamani kubwa sana kuliko huyo jamaa

Inaniuma sana kuona akina dada wakiteseka na kuharibiwa maisha na watu ambao nao wana maisha yao

Jumapili njema ..........!!
 
Message sent and delivered!Ahsante sana kwa ujumbe murua..Nawe jumaapili njema!
 
Mmmmmmmh! Kuna watu wanazaa kwenye NDOA na mume IRRESPONSIBLE vile vile,. Zaa kwa jeuri yako si ya mtu yeyote hata mume.

Haya mambo 6anategemea ntu na ntu. Wengine anzaa na mume wa mtu na anakuwa VERY RESPONSIBLE hata kama wakwake mmoja una mwingine sio wake, anawasomesha wote mashule ya $$$$$$$$ wala haesabu, ila ndo WACHACHE. Mwingine irresponsible ila familia wanajiweza wanakwambia ukachukue matumizi. Kuna shosti wangu anapewa na baba mkwe wake 1.5m za kumlea mjukuu kila mwezi, wala hafanyi kazi njaa toka amalize shule. Na ada kaambiwa asiwaze baba mkwe atacover kuanzia kutafuta shule yeye. Kabla hujazaa na mtu unaangalia kwanza kwao neema za Mungu zipo zipo au majanga?

Unakuta uko na mtu BAHILI hakujali wewe, mia yake huioni afu utegemee ukizaa ndo atakuhudumia? Utakuwa chizi karogwa tena. Au labda ukampulizie ayoe matumizi against his will. Au ndo uka block mshahara ustawi wa jamii.
 
Niache kugegedana???hapana ntajikinga tu....
ahsante kwa ushauri
 
Mmmmmmmh! Kuna watu wanazaa kwenye NDOA na mume IRRESPONSIBLE vile vile,. Zaa kwa jeuri yako si ya mtu yeyote hata mume.

Ukiolewa na mtu wa aina hii wa kulaumiwa ni wewe mwenyewe!
 
Asante kwa ujumbe tumesikia na kuelewa
Umesema ukweli

Tatizo power of love
Mapenzi upofu uwiiiii
 
Nimeupenda ushauri wko Eiyer,, utakuwa umeponya wengi kama kweli wataamua kufata ushauri wako!! Nina rafki alipata mikasa kama hiyo na aliamua kuacha kazi kwaajili ya hyo bwana ila baada ya mimba jamaa akasepa nw ni full kuangaika na katoto tu!!
 
Back
Top Bottom