Ujumbe wangu kwa Waziri Nape Nnauye

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,445
8,299
Ujumbe wangu kwako ni mfupi sana.

Ukiwa waziri wa habari na mawasiliano awamu ya sita naona umeruhusu kwa makusudi viongozi wa dini watukanwe na kudhalilishwa.

Kama haitoshi unabinya kwa makusudi taarifa zao kwenda kwa watanzania. Kinachoendelea mitandaoni nashindwa kuelewa weledi wako.

Basi kama unafurahia au ndo umepanga iwe hivyo basi sawa tu acha watu
walumbane na watukanane wanavyotaka.

Kumbu kumbu zangu zinanirudisha nyuma 2018 Maaakofu hawa hawa walitoa waraka kuhusu utawala bora na wewe ulikuwa mhanga wa hili. Na magazeti yote yaliandika kuhusu waraka huo.

Leo ukiwa kama waziri husika hutaki hata kusikia Maaskofu wanasema nini hata vyombo vya habari umevibinya kuhusu hili. Huku umekaa kimya viongozi hawa watukanwe hovyo.

Wengine tunaamini katika karma na muda ni mwalimu mzuri

Asante.
 
Jamaa kawa mbabe kweli

Alizuiwa press yake wakati ule hadi kutolewa bomba,leo hii kashika mpini


Ova
 
Mie nnachojua nape hanaga akili, inafikirisha anakuwaje waziri...matusi kwa watz wote mil 62!!!.
 
Back
Top Bottom