Ujumbe wa Valentine ‘Day wasababisha talaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa Valentine ‘Day wasababisha talaka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Feb 20, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]HAMISA HAMIDU[28] mkazi wa jijini Dar es Salaaam, amejikuta akitwanga talaka moja na mumewe kwa kile kilichosemekana ni kukosa uaminifu kwa mume wake aliyedumu nae kwa kipindi cha miaka minne toka kufungwa kwa ndoa yao
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Imedaiwa kuwa, sababu ya Hamisa kutwangwa talaka ilisababishwa na simu ya mkononi ambapo alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno unaohusiana na sikukuu hiyo ya wapendanao

  Imedaiwa kuwa, ujumbe huo ulihusisha ni kutumiwa ujumbe huo na namba ambayo mume wake alikuwa haifahamu na moja kwa moja mume huyo alidaiwa kuwa mbogo kwa mke wake huyo

  Imedaiwa kuwa, siku moja kabla ya sikukuu hiyo ilidaiwa mwanamke huyo alimuaga mume wake huyo kuwa atakwenda kumuona mama yake mdogo mkoani Pwani ambaye alikuwa mgonjwa ambapo tayari mume huyo alishamruhusu akamuone mgonjwa huyo

  Siku ya tukio Februari 14,mwaka huu majira ya saa 1 asubuhi, kabla mume huyo hajatoka kuelekea kazini kwake ambapo imedaiwa ni mfanyakazi wa serikalini, simu ya mkononi ya mke wake huyo ilikuwa ikiita ambapo muhusika alikuwa bafuni akijitayarisha na safari yake ya kueleka mkoani Pwani

  Imedaiwa mume huyo hakupokea simu hiyo na aliiacha iite na aliporudi alimtaka mke wake aangalie simu hiyo ili ajue nani alikuwa akimpigia simu hiyo na aliweza kumjibu mumewe hakumtambua mtu huyo kwa kuwa ni namba ngeni kwake

  Baada ya dakika kadhaa namba ileile ilitumika kumtumia ujumbe mfupi wa maneno uliosema” Hallo dear mbona hupokei simu, Happy Valentine Day…..I love Uuu,msalimie huyo, usisahau muda” ulimaliza ujumbe huo”

  Ndipo hapo varangati kwa wanandoa hao likaanza na mume wa huyo alianza kutokwa n jasho la jazba na kupandwa na hasira kali na kumtaka afafanue vizuri hiyo namba ilikuwa ya nani, na mwanamke huyo akaanza kutetemeka na bila kujua aanzie wapi kujibu swali hilo”

  Kwa kuwa hakuwa na jibu la haraka alichangamshwa na ngumi moja na ndipo alipoanza kumjibu mume wake kuwa huenda alikuwa ni mdogo wake binamu aliyeahidiana nae kwenda nae Kwa mgonjwa huenda hakutumia namba yake

  “Labda atakuwa Asha ametumia namba si yake ngoja tumpigie mume wangu labda atakuwa yeye, alijibu Hamisa huku akibujikwa na machozi

  Hata hivyo mume huyo alijikuta akibadilisha shati lake alilolivaa kwenda nalo kazini na walijaribu kumpigia huyo Asha lakini namba yake ambayo alikuwa akiitumia ilikuwa ikiiita na ndipo mume huyo alimuomba samahani shemeji yake huyo kwa kuua soo asijue ishu hiyo

  Mume huyo alianzisha kibano kwa mke wake huyo na kasha kuobndoka na asimyu ya mke wake kazini na alipotoka kazini alipeleka ushahidi huo wa ujumbe kwa wazee ili wauone wasije wakamlaumu na maamuzi atakayoyachukua

  Siku hiyo usiku wakaitwa na wazee kila mmmoja kaitakiwa kutoa maelelezo yake lakini Hamisa alionekana kuwa na huzuni na kudai hakumfahamu mtu huyo, japo mtu huyo kila alipojkuwa akitafutwa kwenye namba hiyo ilikuwa haipatikani

  Kitu ambacho hakikuaminiwa na watu wengi mume huyo alipotoa maamuzi ya kumpa talaka mke ake kwa kuwa alionyesha sio mwaminifu na siku hiyo huenda alikuwa anakwenda kukutana na mwanaume wa nje kitendo ambacho mume huyo kilidaiwa kumtia uchungu

  “ Kwa kweli mimi nikigundua mke wangu anatoka nje ya ndoa wkangu ni sumu sana siwezi kuvumilia, ninavyojitahidi kukutunza halafu unataka kutoka nje ya ndoa siwezi naomba mnisamehe wazee wangu mimi nampa talaka moja mke wangu naona ndio nitapata nafuuu kwenye roho yangu ameniudhi sana” alilama

  Jana Hamisam mjaira ya usiku wa saa mbili alikabidhwia talaka yake moja huku akiiipokea kwa mahcungu sana na ali9jaribu kumuomba msamaha lakini haukukubalika

  chanzo. [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Ujumbe wa Valentine
   
 2. m

  mussamhando Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Za mwizi arobaini
   
 3. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dah..kisa kikali kweli.
   
 4. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  interestin'!
   
 5. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mmmmmh!tatizo watanzania wengi wanachukulia hii valentine vibaya,
  Siku ya wapendano haimaanishi ndio siku ya kufanya ngono jaman lol!
  Pole zake ngoja akatafakari vizuri akiwa kwao.
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  kwani talaka haiwezi kutolewa bila kumdunda mwenzie?? khaa
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  kha mtu unapewa kila kitu lakini bado hautulii, pole yake. ila talaka moja si anaweza tena kurudi kwa mumewe baada ya muda?
   
 8. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Jamaa alikuwa na haraka sana. Angetulia kwanza, aone issue nzima!
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mestod yaani aone kuku wake akinyonyolewa?............humtakii mema mwenzio wengine hatuna huo uvumilivu!
   
 10. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huyo mume anabahati sana-inaonyesha alikuwa akiliwa mali yake tangu muda tu
   
 11. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  haswaaaaaaaa
   
Loading...