Ujumbe wa siku

Mkristo kuwa na mke mmoja naona ni mpango wa hao waliotuletea imani hiyo ili kubana population. Mungu alituumba ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho turudi kwake juu. Na mke anabeba mimba kwa miezi 9 na mume anawezesha mimba zaidi ya moja kwa miezi hiyo 9 kwa wanawake zaidi ya mmoja. Mpango wa Mungu ni tuwe wengi to the maximum, sasa huo ukomo unatoka wapi kwenye maandiko?
Kwa mfano mfugaji wa tija atafuga mbuzi jike labda wanne na dume mmoja kwamba kwa mwaka atapata vitoto mbuzi vinne. Lakini siyo afuge mbuzi jike mmoja na dume wanne eti apate kitoto mbuzi kimoja kwa mwaka, ni hasara.
Yupo Elikana (baba wa Samwel) alikuwa na wake wawili Hanna na Penina na alikuwa akitoa sadaka yake vizuri tu.
Nature haipingwi ona tunavyochepuka. Ninae mke lakini michepuko kibao.
Mwanaume hajaumbwa wa mke mmoja ila mke ni wa mume mmoja. Nature proves
 
Wakristo wanaamini ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja..na hivyo si sahihi kiroho kwa mkristo kuhani msiba kwa mume au mke wa pili kwa mtu..!
Muwe na jumapili ya Baraka.
Vipi kuhusu ambaye hajaoa au kuolewa; naye haifai kuhani msiba?

Nini hasa maana ya kuhani msiba? Sio kumpa pole aliyefiwa bila kujali hali yake ya ndoa? Kwenye misiba haifai kubagua kwa kigezo chochote hali ya mfiwa!
 
Wewe kama si mkristo hata ukipewa mistari haitakusaidia..wakristo wanaelewa na kukubali wito wa mume mmoja na mke mmoja, wewe km hukubaliani hulazimishwi kuwa mkristo unao uhuru wa kuamini vyovyote unavyoona inafaa kwako.
 
Vipi kuhusu ambaye hajaoa au kuolewa; naye haifai kuhani msiba?

Nini hasa maana ya kuhani msiba? Sio kumpa pole aliyefiwa bila kujali hali yake ya ndoa? Kwenye misiba haifai kubagua kwa kigezo chochote hali ya mfiwa!
Kimaandiko imani ya kikristo haisemi, kutooa au kutoolewa ni kosa..na hivyo hakuna tatizo kuhani mtu aliyefiwa na mtu ambaye hakuoa au kuolewa..
Kuhani msiba ni kumfariji na kumtia moyo mfiwa..si sahihi kumhani mtu ambaye kiimani hakuwa sawa ni km kuhalalisha kile alichokuwa amefanya.
 
Neno WEMA na UPENDO ni kati ya keywords muhimu kwenye Bible na yamesisitizwa sana kuyaishi.

Mfano tendeni WEMA kwa watu wote (bila kujali hali zao). Pia, wapendeni watu hata adui zenu.

Kumpa pole aliyefiwa sio kutenda wema kwake? Maana hapo kinachozingatiwa ni ubinadamu wake kwanza!

Kumpa pole aliyefiwa sio kutekeleza amri kuu ya UPENDO ambayo haibagui hali ya mtu?

Unaukumbuka ule mfano wa MSAMARIA MWEMA kuhusu JIRANI YANGU NI NANI? Tenda mema kwa wote ndugu ili kujiwekea hazina isiyoharibika.
 
Ukitafsiri wema kwa muktadha huo basi hata mlokole kumnunulia pombe mlevi alie na kiu ya pombe utasema ni wema..haiko hivyo, nini kinatangulia kabla ya kutenda wema kwa mtu..matukio ya msiba yana mafunzo mengi kwa mfiwa na wafiwa yale wanatendewa wakati wa msiba yana mafunzo kwenye maisha yao kuwafanya wajirekebishe pale walikosea, ulichujua mume/mke wa mtu then unatarajia Padre au Mchungaji afike kwako kukufariji..haiko hivyo..juna namna nyingi za kuonyesha wema na upendo kwa mtu/watu, si lazima kuhani msiba kwa mfiwa.
 
... kinachotangulia kabla ya kutenda wema ni kipi ndugu? Kinachotangulia upendo ni kipi? Yaani conditions zinazotakuwa kuwa fulfilled ili utende wema au upendo ni zipi? Ukristo wa wapi huo?

Huo mfano wako wa mlokole kumnunulia pombe mlevi ni off point!
 
Mfano wa mlevi sio off point..maana yangu, ulevi kiimani ni kosa na hivyo hakuna wema wa kumnunulia mlevi pombe wakati anahitaji pombe..tafsiri ni ile ile, kuoa/kuolewa mume/mke wa pili ni kosa kwa wakristo na hivyo hakuna wema wa kumhani mtu wa aina hiyo.
 
..kinachotangulia kwa mtu ni matendo yake, mtume Paulo anawaambia wakristo wa korintho..kutofungiwa nira/kutokushiriki na watu kwenye matendo/matukio isivyopaswa..2wakor 6:14
 
Wakristo wanaamini ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja.
Una uhakika gani juu ya madai yako hayo? Unamfahamu jamaa mmoja aliyezawadiwa zawadi kubwa ya kuwa Mtu mwenye Hekima zaidi aliyewahi kuishi hapa duniani?(Soma Biblia 1Wafalme3:12). Huyu Suleiman (Mfalme) alikuwa na wake 700 na masuria(Concubines) 300.
Naomba nikuulize kaswali kadogo tafadhali; Je, wewe umeoa i.e.Unaishi kwenye ndoa?
.na hivyo si sahihi kiroho kwa mkristo kuhani msiba kwa mume au mke wa pili kwa mtu..!
Mbona habari ya Kuhani msiba haina uhusiano wowote na mambo ya ndoa? Ni sawa na kuhoji eti mbona Wakristu wanakwenda kuhani msiba wa Waislamu au Wahindu au Wasio na dini yoyote? Kumbuka Jamii yoyote mahalia inao utaratibu wa kumpa pole mtu YEYOTE aliyefiwa, aliyefikwa na madhara e.g. kuunguliwa nyumba, kufiwa n.k. Sasa kama katika Jamii unamoishi ww huo utamaduni haupo kama kwa wenzetu huko nje e.g Ulaya etc; jirani yako amefiwa ww unaendelea na hamsini zako -hakuna shida na wala hutodaiwa au kulalamikiwa. Inakubalika hiyo.
Mwisho: Jitahidi usichanganye mambo ya Kiroho na mambo ya Ubinadamu/Utamaduni na Desturi za Watu au Jamii.
Zingatia: Ndoa zipo hapa duniani na ni Jambo la kidunia-Ukifa huendi na ndoa yako- ndo kusema ndoa imekomea hapo broo. Roho, (tunavyoamini) ndo inaenda kwa Muumba wetu. Usitegemee kwenda kwa Mungu na lundo la wake zako, michepuko yako n.k. kwa Muumba wako sijui eti wakakutetee n.k.n.k-Utasimama na Kuhukumiwa peke yako broo.
Muwe na jumapili ya Baraka.
Amina, na iwe kwako pia.
 
..kinachotangulia kwa mtu ni matendo yake, mtume Paulo anawaambia wakristo wa korintho..kutofungiwa nira/kutokushiriki na watu kwenye matendo/matukio isivyopaswa..2wakor 6:14
... matendo ya yupi? Anayefarijiwa au anayefariji? Kwenye ule mfano wa MSAMARIA MWEMA yule aliyesaidiwa matendo yake yalichangiaje yeye kupata msaada? Haikuandikwa wapendeni adui zenu?
 
... kilichokatazwa ni kutenda dhambi. Kama unaamini kunywa pombe ni dhambi basi hupaswi kumnunulia mlevi pombe.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, kwani walioenda kumpa pole walienda kumfariji au kumuoza?
 
1. Haya si madai, imani ya kikristo inaelekeza hivyo.
2. Unafahamu sabab ya mfalme sulemani kuwa na wake na masuria kwa idadi hiyo? Mojawapo ya sabab ni hii, hekima ilimwelekeza kuwa atakapooa mke kutoka kwenye koo zote zilizokuwa jirani na taifa lake ataweza kuishi kwa amani na jirani zake muda wote wa utawala wake, na ndivyo ilivyokuwa..suleman hakuwah kupigana vita hata moja wakat wa utawala wake..na si kwamba maadui hawakuwepo..lkn sisi hatuwez kuishi mfano wa suleman.
3. Neno msiba lina mfiwa au wafiwa, huyo aliyekufa ni nani kwao..baba, mama, mume, mke..mjomba nk unapokwenda kuhani unamhani nani..baba/mama wa mtoto, mume/mke, mtoto nk hivyo huendi kuhani bila kufahamu UHUSIANO wa mfìwa na aliyekufa..
4. Kwenye imani ya kikristo hakuna habari ya utamaduni kufunika mambo mema au mabaya.
5. Uwepo wa ndoa ni maelekezo ya Mungu tukiwa hapa duniani, ni sawa tu na maelekezo ya kuhudhuria ibada jumapili..tunaishi ktk mwili tukiwa hapa duniani, na kiimani mwili ni hekalu la Kristo..hekalu halipaswi kuchafuliwa, baada ya maisha ya duniani tunaishi ktk roho..haya ni maelekezo kiimani.
6. Tunaishi kwa kumpendeza Mungu kwanza na si jirani, kiongozi au binadamu yeyote..na matendo yetu yanasomwa km barua na hao wanaotuzunguka ili yawasaidie kujua, kujirekebisha na kujifunza vile Mungu anataka sisi sote tuwe tungali hapa duniani.
 
... matendo ya yupi? Anayefarijiwa au anayefariji? Kwenye ule mfano wa MSAMARIA MWEMA yule aliyesaidiwa matendo yake yalichangiaje yeye kupata msaada? Haikuandikwa wapendeni adui zenu?
Wote..mfano wa msamaria mwema una mafunzo tofauti, ni utaratibu ulikuwepo wayahud kutochanganyika na kabila zingine..funzo hapa ni tenda wema kwa mtu kulingana na uhitaji wake.
 
... kilichokatazwa ni kutenda dhambi. Kama unaamini kunywa pombe ni dhambi basi hupaswi kumnunulia mlevi pombe.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, kwani walioenda kumpa pole walienda kumfariji au kumuoza?
Kuoa/kuolewa mume au mke wa pili ni kosa, na kiimani kosa linarekebishwa na mkosaji kwa kujirudi, bila hivyo kosa linabaki..
Unapokwenda kumfariji mtu, unamfariji kwa kufiwa na nani? Baba, mama, mjomba au nani..?
 
1. Haya si madai, imani ya kikristo inaelekeza hivyo.
Imeelekeza hivyo wapi? Nipe vifungu mkuu.
Mkuu, Mbona hapo naona kama umechapia/umeongeza vya kwako? Taz. eneo lenye kupigiwa mstari
3. Neno msiba lina mfiwa au wafiwa, huyo aliyekufa ni nani kwao..baba, mama, mume, mke..mjomba nk unapokwenda kuhani unamhani nani..baba/mama wa mtoto, mume/mke, mtoto nk hivyo huendi kuhani bila kufahamu UHUSIANO wa mfìwa na aliyekufa..
Sawa. Huyo anawekwa kwenye kundi la Jirani. Jirani ni mtu yeyote yule ambaye ni Mhitaji na ww unayo nafasi ya kuchangia Hitaji lake.
4. Kwenye imani ya kikristo hakuna habari ya utamaduni kufunika mambo mema au mabaya.
Kwa mfano??
Kumbuka maelekezo yote ya Mungu yapo Summarized kwenye Amri kumi za Mungu i.e. The 10 commandments. Zaidi ya hayo yanatoka kwa wanadamu au kwako.
6. Tunaishi kwa kumpendeza Mungu kwanza na si jirani, kiongozi au binadamu yeyote..na matendo yetu yanasomwa km barua na hao wanaotuzunguka ili yawasaidie kujua, kujirekebisha na kujifunza vile Mungu anataka sisi sote tuwe tungali hapa duniani.
Mkuu; Unathubutu kusema eti Tunaishi kwa kumpendeza Mungu? Tunampendeza Mungu ili iweje? Kwani Mungu atapungukiwa na nini kama asipopendezwa na sisi?
 
Tusibishane na kuulizana maswali ambayo mengine yanahitaji wewe unayeuliza uwe na ufahamu wa mambo kadhaa kabla ya kuuliza..siko tayari kuanzia huko, wewe endelea na unachokiamini kwenye maisha yako..ombi langu Mungu akujalie neema ya kufahamu njia sahihi ya kufuata kwa maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…