Ujumbe wa Mh Kingwangala kwa Umma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe wa Mh Kingwangala kwa Umma!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kituku, Feb 24, 2011.

 1. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [​IMG] Ujumbe wa Mh. Kigwangala kwa Wananchi

  Ndugu wana jamii
  Katika pita pita zangu kushangaa ulimwengu, nimekutana na ujumbe mahsusi katika wall ya Dr Hamis Kigwangala (mb) Nzega. (kwenye facebook)

  Ukisomeka hivi::
  Kuhamasisha na au hata kufikiri tu kwamba Tanzania itafika na kufaidika na maandamano na mapinduzi ya viongozi waliowekwa na umma kwa njia za kidemokrasia, ni ukosefu wa hoja, weledi na upotofu uliokithiri! Michango/mawazo ya namna hiyo tuikatae kwa nguvu zetu zote!


  na hizi chini ni miongoni mwa comments zake

  Dokta Hamisi Kigwangalla Tanzania ina matatizo yake lakini siamini kama yanatatulika kwa vurugu, kwa utovu wa nidhamu kwa sheria na kanuni zilizowekwa na vyombo vyetu vilivyotuongoza hadi kufikia hapa tulipo...kufikiria kuvunja amani na utulivu tulionao si sahihi na wala hatujafika na hatutofika huko kwa uwezo wa mungu inshaallah! Tuhoji, tubishane na tushindane kwa nguvu ya hoja bila kuhamasisha wala kufikiria hoja za nguvu...hazina nafasi na sote kwa pamoja tuzikemee! Leo hii walioandamana hizo nchi za huko bara arab wameanza kuzikimbia nchi zao...


  Dokta Hamisi Kigwangalla Kiva, mazingira ya huko ni tofauti na ya kwetu...Tanzania hakuna mtu anayeng'ang'ania kukaa madarakani kwa mabavu...viongozi na wawakilishi wetu tunawachagua kwa sheria na taratibu tulizojiwekea! na wananchi tuna haki ya kujadili na kudai mabadiliko kwenye chochote tunachokiona hakiendi sawa - kwa ufupi 'hakuna udikteta'. sasa iweje leo tusipambane kwa nguvu ya hoja ili kurekebisha mapungufu yaliyopo na badala yake tuanze kujadili siasa za mkumbo wa vurugu na uvunjaji wa amani??? Hili ndo ninalolikataa hapa mimi!


  Mimi binafsi, nimeamini kweli viongozi wetu tayari wamekuwa na hisia na imani ya woga juu ya mapinduzi yalioonyesha na yanayoendelea huko nchi za wenzetu. Inaonyesha dhahir kuwa sasa wapo viongozi tayari wameanza kupata vitumbo joto wakirefer yanayotokea Egypt, Libya, na kwengineko. SAsa kwa maelezo haya na comments hizi za Mbunge, wana jamii hamuoni hawa watu kweli wamelewa madaraka na wamekaa kwenye vyeo walivyonavyo kulinda maslahi ya o na mfumo walio nao?

  Kweli, baadhi wa wabunge wamegombea nafasi zao ili tu wakajinufaishe na kutajirika kwa mamilioni ya maposho na fedha na si kwa maslahi ya umma na mustakabali wa taifa..

  Wanajamii mnaonaje juu ya statements za huyu mbunge hapo juu?
   
 2. d

  dry seaman New Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anachokisema dkt. ni sahihi lakini ni hoja gani za nguvu zinatakiwa ziwasilishwe maana kama matatizo ya watz yanajulikana na hakuna strategic plan zilizokuwa implemented b4 and even now zaidi inflation inaongezeka may ni makosa yetu cc watz hatututmii haki yetu ya msingi vizuri ktk kupga kura ili tupate viongozi wataojali maslahi ya walio wengi hivyo dkt kwa fursa
  alionayo aonyeshe njia ili tuamini kuwa we can
   
 3. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona fursa zinaonyeshwa sana na wananchi? ila wanakatishwa tamaa na mfumo uliopo... kwa historia inavyooshesha, hata tupige kura vipi wenye nchi yao na wapenda madaraka wataendelea kutubana tu.
   
 4. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kweli huyo kingwangwala kama jina lake, yeye na wenzake hawataki vurugu because maisha yao ya juu waliyowadhulumu wadanganyika watapokonywa.
  kwahiyo anatuambia ni bora wengi wetu tuendelee kuishi maisha marefu yenye shida na dhiki na raha za msimu wa uchaguzi,,, kuliko taabu ya muda mfupi na neema a muda mrefu?
   
 5. Kituku

  Kituku JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bado tuna safari ndefu
   
 6. s

  smz JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kingwangala anaogopa kivuli chake
   
 7. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anachokiongea Dr. ni sahihi kwa nafasi yake lakini si sahihi kwa maslahi ya taifa. Nani anahamasisha uvunjaji wa amani Tanzania kama si wao walioshiba na kutusahau sie wanyonge. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwananchi wa kawaida na Mh. Mbuge!!

  Ajiulize vyema kama yeye anataabika kupata sukari dukani. Sisi hata uji hatuujui ulivyo na hii ndo hamasa kubwa ya uvunjaji wa amani. Hawawezi kuzungumzia amani bila kuwa na misingi ya hiyo amani ambayo ni usawa, haki n.k
   
 8. s

  smz JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa watu wa aina ya Kigwangala yaani wah Wabunge, kwao AMANI na UTULIVU wanavyo kwa asilimia mia. Hebu angalia unapewa mkopo wa sh. mil 90 kununulia gari!!! oh crazy!! mwingine alikuwa hata hajawahi kumiliki Bajaj.

  Kwa waTZ tulio wengi tulichobakiza ni UTULIVU tu, lakini kitu kinachoitwa AMANI kilishatoweka zamani. Labda dr alikuwa hajui. Nimpe mfano Dr na wengine wenye mtizamo kama wake: Hebu imagine mko ndani ya benki, mara jambazi akavamia na kuwaamrisha wote mlale chini na kutulia. "LALA CHINI, TULIA"!!!!!!. Niambie pale kuna nini: kilichopo ni utulivu tu tena wa kulazimishwa, lakini AMANI haipo.
   
 9. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  @Kituku, mimi siyo mtawala, mimi ni muwakilishi wa wananchi kwenye Bunge, sihofii chochote kutokana na maandamano ya CHADEMA na hata yale ya kule Kaskazini mwa Africa. Na mimi mtazamo na msimamo wangu kwenye masuala ya vurugu uko wazi kabisa, ni kitu nisichokitaka na nitakipinga siku zote. Naomba ifahamike hapa wazi kabisa kuwa 'sipingi maandamano' - hata mimi nimeishatoa mwaliko wa maandamano ya amani kupinga uwepo wa mgodi Nzega, na wewe nakukaribisha ushiriki. Sema nasikitishwa sana na kauli ya kiuchochezi iliyotolewa na mmoja wa viongozi wa CHADEMA kuwa Tanzania 'haitotawalika' na pili nasikitishwa sana na tafsiri potofu ya watanzania wenzangu, tena wengi wasomi wazuri kabisa, wanaojaribu kufananisha hali yetu kisiasa na kiuongozi na ya kule kaskazini na pia kufananisha maandamano safi kabisa ya CHADEMA na maandamano ya watu wenye hasira kali wa kule. Tatu, nasikitishwa na tafsiri potofu ya 'nguvu umma' - kwa kawaida nguvu ya umma haitegemewi ihamasishwe na chama cha siasa, maana yenyewe huibuka ghafla pale wananchi wanapochoshwa na mfumo wa kisiasa na kiuongozi unaotawala nchi au ukandamizaji unapozidi. Sasa hapa watu wanaongelea nguvu ya umma inayohamasishwa na chama cha siasa...kwa vyovyote vile hawatofanikiwa kuungwa mkono na watanzania walio wengi badala yake watabaki wao wachache na wanachama wao.

  @SMZ, kama kuna mtu anahitaji gari kubwa aina ya 4WD basi ni Mbunge...mimi kabla sijawa Mbunge nilidhani kwamba kumpa gari
  Mbunge ni anasa na matumizi mabaya ya pesa za umma, lakini baada ya kugombea tu nikaanza kuuona umuhimu wa uamuzi huu (wengine watasema kuwa nasema haya kwa kuwa mimi kwa sasa ni beneficiary! lakini mimi hupenda kusema ukweli na huu hapa ni ukweli tupu). Hebu jiulize Mbunge anafikaje kwa wananchi wa jimboni kwake? Barabara mbovu, huwezi kwenda na gari ndogo, wananchi wanataka Mbunge ufike kuwasikiliza kero zao, ushiriki kwenye kazi za maendeleo na matatizo na majanga ya kijamii, ukague miradi, n.k. Hivi utafikaje bila kuwa na gari? Sijui kwa nini walifikia maamuzi ya kutoa mikopo ya pesa hizi badala ya kuwapa wabunge magari, lakini naamini katika umuhimu wa kuwa na gari kwa kweli.

  Nawasilisha,
  Kigwangalla.


   
 10. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  We bwana wewe mh kweli unasahau, tena we kwavurugu mh labda kama umeacha siku hizi, nakumbuka ulivyongoza mgomo wa madaktari muhimbili leo unadai sijui nini. Kuhusu mgodi wa nzega ni kwamba wako kwenye kumalizia tu then mwakani miezi ya katikati mgodi utafungwa, kwahiyo usiseme kwamba unahamasisha maandamano ya amani kupinga uwepo wake muheshimiwa, kama taarifa hazijakufikia ni kwamba mgodi utafungwa. Endelea na shughuli za kujenga taifa usipoteze muda wa kuhamasisha kwani ipo kwenye ratiba ya wawekezaji hawataendelea tena kuchimba.
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  ukitaka kujua nchi kutotawalika rejea ibara "8.-(1) jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
  misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
  (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;"
  (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
  (c) Serikali itawajibika kwa wananchi;"


  a=0
  b=0
  c=0
  kutotawalika kutaanzia hapo.   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Ndugu mbunge ( kwa sababu mimi kwangu hakuna muheshimiwa ) humu humu JF kuna thread iansema ofisi yako imeandaa maandamano huko Nzega tarehe 3 mwezi wa nne kama sikosei, kupinga kuwa na mgodi jimboni kwenu ambao hamna maslahi nao, sasa swali hauoni kwamba bungeni ndio sehemu sahihi ya kwenda kupeleka hoja zako, kwa nini maandamano? hauoni kwamba unataka kusababisha uvunjifu wa amani na usalama wa Taifa? na je hauoni unataka kuonesha taswira mbaya kwa wafadhili na wawekezaji kwamba Tanzania si sehemu salama na kuaminika kuwekeza?
  Turudi kwenye swala la magari, hivi mtu kama musa Zungu ambaye jimbo lake la ilala anaweza kulitembelea lote tena kwa miguu ndani masaa mawili kwa nini kila baada ya miaka 5 apate gari jingine?
  Haya gari sio issue lakini nina uhakika magari yenye samani ya shilling millioni 30 kila moja yangewatosha kabisa, kwa nini umchukuwe millioni 90! nina ushaidi usio na shaka with supporting document wabunge wawili wameagiza magari ambayo waligarami sh millioni 30 kila mmoja na wakabaki na sh millioni 60 kila mmoja mifukoni mwao, hivi mnadhani mnamuibia nani?
  Msidhani huu umma unavyoamka ni kwa sababu ya CHADEMA, NOP, bali ni umma uliokata tamaa halafu nyinyi mnadhani ni binadamu ambao mnaishi sayari nyingine. wananchi watakapoamuwa hatutoangalia maswala ya vyama ninyi na wabunge wa upinzani wote tutawapa hukumu moja ya haki kwa kushiriki uovu dhiki ya pesa za umma.
   
 13. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Matola, ni wazi kabisa unafahamu kuwa serikali inawajibika kwa wananchi. na hawa ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. mimi kama muwakilishi wa wananchi nimeishafanya jitihada mbalimbali za kutafuta suluhu ya mambo mengi yanayohusiana na mgodi huu bila mafanikio, nimeshawasilisha bungeni hoja yangu binafsi bila majibu - nasubiri labda kuna lolote litakalotokea, sasa nimeamua kwenda kwa wananchi ili waelewe jitihada zangu, wajadili suluhu, wapaze sauti, na mimi ntawasilisha kwa wahusika!

  Kuhusu gari sidhani kama kuna haja ya kumpangia Mbunge anunue gari gani, maana ni mkopo wake na anakatwa kwenye mshahara wake. Na kwanza naomba ifahamike hapa kuwa mkopo huu wanapata na wafanyakazi wengine wa serikalini na wala siyo wabunge peke yao. Mimi binafsi ningependa zaidi kuona napewa gari Mpya, inayosevisiwa na serikali, na dereva wa serikali, ili nikiondoka kwenye kiti mwingine anaendelea navyo. lakini nadhani walifanya hivi ili kuifanya ofisi ya Mbunge iwe independent - katika jitihada za ku-create checks and balances kati ya pillars tatu za uongozi wa Taifa letu. Maana ingetakiwa Mbunge sasa awe na wafanyakazi kadhaa, idara ya accounts and management - ambao wange-manage hesabu za pesa na mambo mengine yote ya kitawala kwa ajili ya Mbunge na wangetakiwa ku-comply na kanuni mbalimbali za fedha n.k, na pengine na wafanyakazi wengine kama waratibu wa shughuli za Mbunge kwenye michezo, vijana, ajira, utamaduni, kilimo n.k. Lakini ili kubana matumizi, waliona wamuache Mbunge aiendeshe ofisi yake yeye mwenyewe jinsi anavyotaka ila wampe posho na mishahara ya wafanyakazi wake, wampe posho ya mafuta na vifaa vya ofisini n.k. Ungeniuliza mimi, nadhani ni bora wangeweka ofisi permanent ya Mbunge yenye facilities zote stahiki including management structures fit for the office tofauti na walivyofanya sasa! leo hii ofisi ya Mbunge ni ndogo, haina hadhi, haina privacy, haina wafanyakazi professional (kwa sababu Mbunge kwenye maelezo ya mchanganuo wa posho unazopewa, wanapendekeza umlipe dereva wako TZS 100,000 na Katibu wako naye around hiyo hiyo, hebu imagine ni professional gani utamlipa mshahara huo na akakubali kufanya kazi kweli?
   
 14. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Matola, ni wazi kabisa unafahamu kuwa serikali inawajibika kwa wananchi. na hawa ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. mimi kama muwakilishi wa wananchi nimeishafanya jitihada mbalimbali za kutafuta suluhu ya mambo mengi yanayohusiana na mgodi huu bila mafanikio, nimeshawasilisha bungeni hoja yangu binafsi bila majibu - nasubiri labda kuna lolote litakalotokea, sasa nimeamua kwenda kwa wananchi ili waelewe jitihada zangu, wajadili suluhu, wapaze sauti, na mimi ntawasilisha kwa wahusika!

  Kuhusu gari sidhani kama kuna haja ya kumpangia Mbunge anunue gari gani, maana ni mkopo wake na anakatwa kwenye mshahara wake. Na kwanza naomba ifahamike hapa kuwa mkopo huu wanapata na wafanyakazi wengine wa serikalini na wala siyo wabunge peke yao. Mimi binafsi ningependa zaidi kuona napewa gari Mpya, inayosevisiwa na serikali, na dereva wa serikali, ili nikiondoka kwenye kiti mwingine anaendelea navyo. lakini nadhani walifanya hivi ili kuifanya ofisi ya Mbunge iwe independent - katika jitihada za ku-create checks and balances kati ya pillars tatu za uongozi wa Taifa letu. Maana ingetakiwa Mbunge sasa awe na wafanyakazi kadhaa, idara ya accounts and management - ambao wange-manage hesabu za pesa na mambo mengine yote ya kitawala kwa ajili ya Mbunge na wangetakiwa ku-comply na kanuni mbalimbali za fedha n.k, na pengine na wafanyakazi wengine kama waratibu wa shughuli za Mbunge kwenye michezo, vijana, ajira, utamaduni, kilimo n.k. Lakini ili kubana matumizi, waliona wamuache Mbunge aiendeshe ofisi yake yeye mwenyewe jinsi anavyotaka ila wampe posho na mishahara ya wafanyakazi wake, wampe posho ya mafuta na vifaa vya ofisini n.k. Ungeniuliza mimi, nadhani ni bora wangeweka ofisi permanent ya Mbunge yenye facilities zote stahiki including management structures fit for the office tofauti na walivyofanya sasa! leo hii ofisi ya Mbunge ni ndogo, haina hadhi, haina privacy, haina wafanyakazi professional (kwa sababu Mbunge kwenye maelezo ya mchanganuo wa posho unazopewa, wanapendekeza umlipe dereva wako TZS 100,000 na Katibu wako naye around hiyo hiyo, hebu imagine ni professional gani utamlipa mshahara huo na akakubali kufanya kazi kweli?
   
 15. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kingwangala, ninakushangaa kusema kuwa wewe kama mbunge umefanya jitihada mbalimbali ili kupata suluhu ya matatizo ya jimboni kwako. Je unafikiri chama chako (CCM) kina uwezo wa kuwatattulia wananchi matatizo yao kama hayo uliyoyataja. It is obvious kuwa umekata tamaa na utekelezaji wa uliyowaahidi wana nzega. Kwa kweli haitawezekana kundi la watu wachache (serikali ya ccm ukiwamo wewe) wanoneemaka na huku wananchi wengi wakilala kwenye nyumba za tembe lifanye jambo la kuwaokoa., with ccm this thing is impossible. Najua unajifanya kuwatetea wakati ukweli ni kwamba unapalilia masilahi binafsi yakiwemo yale ya WAMA (waliokushika mkono kwenye kinyanganyiro baada ya kumchakachua bashe na selelii). Pia ulinukuliwa wewe pamoja na makada wa chama chako kikongwe (watu waliofilisika kifikra) mkiiponda chadema kuwa kinachochea mauaji. Je chadema ndiyo waliwaambia kuilipa dowans, vipi kuhusu epa, deep green, meremeta, kagoda, kuchakachua matokeo ya uchaguzi, maandamano ya wanafunzi baada ya kunyimwa hela za kujikimu, umeme, inflation etc. Nadhani mtakuja kusingizia kuwa chadema wanasabbisha hata mvua isinyeshe. Mnasahau kuwa mnaowaongoza ni bianadamu na wao wanaihitaji kuishi. Na ili waishi kama wanadamu serikali yao lazima iwajibike kwao na siyo kwa mafisadi na akina aydialawi (mwarabu feki wa dowans). Hapa ccm wanatakiwa kujibu hoja na siyo ni lini watarekebisha haya matatizo ili watu wapate nafuu ya maisha. chadema wanacho kifanya is pushing the government to resume its responsibility to it people.And the fact that people comes in great number during chedemas rallies threatens you (ccm) and your allies. Mjibu hoja and not jumping like wild cats. Shame on ccm, viva Tanzania.
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Nami naomba kuchangia kidogo kuhusu magari, kwamba mbunge anhitaji 4wd kwakuwa bara2 ni mbovu! Je halmashauri za wilaya ambao to me ndio wanaopaswa kushirokiana na jamii katika kuleta maendeleo, je wanahayo Magari ya kutosha?

  Na kwa mtazamo wangu, shida ni mfumo usiofaa wala kujali! Hakuna kitu kinachoniboa kama maendeleo yanayokuja baada ya bwana mkubwa kutembelea sehemu na kuahidi kitu! Kwanini development plans zisifuatwe (kama zipo)? Instead of waiting favors from mkubwa fulani.

  Tukirudi kwa wabunge, role yao ni ndogo sana ktk maendeleo, kwakuwa system ni poor ndio maana wanaonekana kama tumiungu fulani, hence titles like "mheshimiwa"
   
 17. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  thanks nyamagaro.

  Dk hamisi ameingia mitini
   
 18. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ungekuwa karibu ningekutwaga ngumi, kwa taarifa yako kwenye maandamano yako vurugu itakuwa no.moja.
  ubovu wenu wote viongozi wa ccm mmefungwa kwenye kamba moja na mnamfuta huyo aliye mbele hata akinya nyie mnakanyaga tu kwa sababu mnakokotwa. usingekuwa na maandamano ya vurugu kifikra kichwani usingekuwa Dr. Usibeze wanaojiua nao ni viumbe wa Mungu ila kumfaata mtu bila kufikiri kama ccm mnavyofanya mtabaki kama maji ya mto tu.
   
 19. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tabora na ya mwisho sie wenye neema kidogo kuzidi nyie tunawaamsha wewe na udakitari wako una wambia ni sawa wengine waendelee Tabora ibaki kama wakati wa waarabu. Ulidesa au ulikuwa dr.kisawasawa maana siamini kama kun dr anawaza kama wewe .Tabora mtajivunia nini?
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika Kama ni yeye au mtoto wake, kama ni yeye ni mganga wa kienyeji, anakaa Ipuli Tabora. So uDr wake ni wa kienyeji kama ni Dr kigwangala wa Ipuli Tbr!
   
Loading...