jamaikatz
JF-Expert Member
- Jul 11, 2023
- 369
- 1,252
Mambo vipi wana JF.
Matumaini yangu wote mko poa,
Uzi huu ni kwaajili ya watu wote, lengo ni kutiana moyo,kufarijiana,kusapotiana na kuleta maneno ya hekima, yenye misemo na methali mbalimbali yanayohusu maisha, mahusiano, afya, mapenzi, imani n.k..
Karibuni sana..
🌟 UJUMBE WA LEO: JIUMBE UPYA 🌟
“Maisha sio kuhusu kujitafuta, bali ni kuhusu kujiumba mwenyewe.”
– George Bernard Shaw
Kuna nyakati tunaishi tukijitafuta… tukiamini kwamba kuna "mimi halisi" aliyepotea mahali fulani duniani.
Lakini ukweli ni kwamba HUJAPOTEA. Ila tu Bado hujajiunda.
Usingoje mazingira yakutengeneze.
Usiwaachie watu wakuelezee wewe ni nani.
Chukua hatua. Andika hadithi yako.
Anza leo kuwa mtu unayetaka kuwa –na sio yule unayedhaniwa kuwa.
✍🏽 Jiulize:
“Nataka kuwa nani kwa miaka mitano ijayo?”
Kisha anza kuwa mtu huyo... kuanzia sasa.
Maisha ni ubao tupu. Kalamu iko mkononi mwako.
JIUMBE. USIJITAFUTE.
Aliyewahi kuwa Rais wa awam ya pili.
Mwinyi aliwahi kusema: maisha ni kitabu cha hadithi.
Na wewe ndo mwandishi wa hio hadithi hivyo style ya uandishi na aina ya mandishi, ndo itakayotoa picha kwa wasomaji wa kusome kama mtu wa aina gan.
Kila mtu ana kitabu chake kwenye haya maisha, na kamwe maudhui yaliyopo ndani ya hivyo vitabu hayawezi kufanana.
Kwa kutambua hilo, elewa kuwa maisha ni wewe sio wao, maisha sio kuhusu wanavyokutazama, bali unavyojitazama.
Mtazamo wako juu yako ndo unaoamua wao wakutazameje.
Kuna mtu wakati wengine wanalia msibani yeye huko alikuwa anachekelea kwa kumpata mwandani wake.
Unajua namaanisha nini?
Hatuwezi kufanana, kila mtu ananjia yake.
Usipoijua njia yako na kujitofautisha na wengine, utaendelea kuwa msindikizaji kwenye safari uliyopaswa kuiongoza.
Kuna kauli niliwahi kuiskia miaka zaidi ya 4 iliyopita kauli hio ilinipa wakati mgum sana kuielewa, niliitunza na kuendelea kuitafakari kwa mda mrefu sana bila jawabu sahihi..
Lakini nilikuja kupata majibu baada ya miaka zaidi ya 3+ ndipo nilipoweza kuelewa maana yake, kauli gani hio Mwalim??
Bora hata umeniuliza, kauli ni hii hapa👇
WATU WENGI SANA WANAKUFA WAKIWA NA MIAKA 20 LAKINI WANAZIKWA WAKIWA NA MIAKA 60🤔
Najua hata wewe ndugu msomaji umeshangaa na unajiuliza kivipi, sindio eeh?
Basi usijali nimeshakusaidia kuumiza kichwa na majawabu yapo hapa ndani ya dk chache tu utakuwa umepata majibu na maana halisi.
Bila shaka umewahi kusoma, kusikia kutoka kwa Waalim tofaut tofaut, wakisema jambo hili...
Hakuna mtu aliezaliwa kwa bahati mbaya, kila mtu amezaliwa kwa kusudi maalum, umewahi kusikia sindio?
Kama nikweli umewhi kusikia je ulichukua hatua gani baada ya kusikia?
Binadam wengi sana hasa wabongo, ni wavivu sana wakufikilia mambo muhimu.
Yaan mtu yuko radhi kusoma na kufuatilia udaku wa connection ya fulan lakini sio kujifunza, ni huzuni sana🥲
Na ndio maana hushangai kuona bara la Africa linaendelea kuteseka sana na kutegemea misaada kutoka bara la ulaya, yaan tunapewa misaada ambayo sisi ndio tulipaswa kuitoa kwa mabadala mengine
Au kama si hivyo basi tulipaswa kuwa tunajitegemea wenyewe, lakin bado tunaendeshwa, Trump, aliwahi kusema:
Hata leo kama itatokea, waMarekani wakaja kuishi Africa na waAfrica wakaenda kuishi Marekani, baada ya miaka michache Marekan Itakuja kuomba msaasa Africa.
Ukifikilia kwa haraka sana unaweza kuona kama alitutukana hivi eeh?
Lakini hajatukana aliongea uhalisia kabisa, alitukumbusha kuwa bara la Africa sio maskin ila akili za waAfrica ndio maskin
Ukiangalia kwa haraka unaweza kuona kama bara letu liko huru, si hata sisi Tanzania tumeshapata uhuru toka 61 huko?
Lakin ukifatilia kwa undani zaidi, utagundua tumebadilishiwa tu aina ya utumwa.
Zamani tulitawaliwa kimabavu, lakin kwa sasa tunatawaliwa kifikra.
Nyerere aliwahi kusema: kuna aina tatu za umasikin.
1. Kiuchumi
2. Kukosa maarifa
3.Ukosefu wa uongozi.
Kama tutafanikiwa kwenye namba 2 basi
Tutakuwa tumepata uhuru mkamilifu.
Ok tuachane na hilo, turudi kwenye point ya msingi..
Kusikia mambo ya muhimu na ukaendelea kuyapuuzia huo nao ni aina nyingine ya umaskin...
Nakumbuka miaka kadhaa nyuma iliyopita, nilikuwa napata kesi nyingi sana za ndoa na mahusiano..
Naletewa kesi na watu wazima alafu kesi nzito sana na wakati huo nilikuwa sijagundua kusudi langu, hivyo nilikuwa nasikiliza wee mwisho nawapa ushauri na kwel watu wanaona matokeo, sasa swali kwangu likawa ni moja, kwanin watu wanaleta case zao kwangu?
Wakati hata sijatangaza popote kwamba mim ni Mwalim wa mahusiano?
Sikuapata majibu
Nikaamua kumfata Mchungaji wangu kanisan
Nikamhadithia, akanisikiliza akanipa ushauri mzuri sana
Na kuanzia huo wakati ndipo nilijua mim ni nani, nikaamua kujifunza sana mahusiano kwa bidii kubwa, jumlisha matukio ambayo nimeshapiga na kupigwa huko nyuma..
Hivyo vyote vilikuwa chanzo chamim kulisogelea na kuamua kuliishi kusudi.
Sasa hebu jiulize leo:
WEWE NI NANI??
Ukiachana na jina lako umepata jibu gani lingine?
Je nikitu gan ambacho ukikfanya hua unasikia raha sana na unakifanya hata pasipo kulazimishwa?
Kaaa tuliza akili yako vizuri tafakari kisha' CHUKUA HATUA
AMUA KUISHI
KATAA KUISHIA
ISHI.
ISHI
ISHI
NARUDIA TENA ISHI
Somo hili sio kwaajili ya kila mtu, ndio maana sio wote watasoma mpaka mwisho ila kama umesoma mpaka mwisho basi kuna namna limekugusa
Chukua hatua tumia haya maarifa
Kataa kutumika au kuishi katika kusudi.
Hongera kwa kusoma na kutafakari naamin umejifunza kitu, muhimu fanyia kazi.