Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 24,703
- 44,059
Rais wa Yanga SC Engineer Hersi Said kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe wa kuwashukuru Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo baada ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya NBC Msimu huu
Injinia Hersi ameandika ✍🏿
"ALHAMDULILLAH!!!
YANGA BINGWA WA NBC 2024/25
Shukran za dhati kwa mola muumba wa mbingu na ardhi kwa neema hii ya ubingwa wa NNE mfululizo.
Pongezi kwa wadhamini wetu, SPORTPESA, GSM GROUP, NIC, HERO, VISIT ZANZIBAR, SILVER GENERAL, AZAM TV na AIR TANZANIA.
Wananchi, nyie ni mashabiki bora sana na mlio imara. Isingekuwa rahisi kupata mafanikio haya bila ya umoja na mshikamano wenu.
Makamu wa rais na kamati yetu ya utendaji imekuwa ni msaada mkubwa katika uongozi wangu huku timu ya utendaji ikifanya kazi usiku na mchana katika kufikia malengo yetu.
Kwa familia yangu, mke wangu na watoto wangu nawapenda na kuthamini mchango wenu siku zote katika kufikia malengo yangu.
“YANGA BINGWA” ni neno maaruf la Mr. Ghalib likibeba dhana nzima ya malengo ya uongozi wetu huku akiwa na msukumo mkubwa katika mafanikio haya. THANK YOU!!!!!!!!"