Ujumbe wa Dr. Shein una walakini

Wakati Dr Shein anasoma risala yake ndefu, aliamua aisitishe kwa kuwa jua lilikuwa linawawakia wananchi pale uwanjani.Lakini akasema ngoja amalizie kwa kusoma mambo muhimu.

Akaanza kuzungumzia mishahara ya wafanyakazi, wakati Dr Shein anajisifu kwa kuboresha mishahara ya watumishi wa umma na akawaahidi tena kuwa wasione ajabu na mwaka huu tena akawaongeza mishahara, ndipo kamera za TBC zikamuelekea Rais Magufuli, nikamuona kama anagwaya vile, kwa kile anachokifanya cha kutokuongeza mishahara watumishi wa umma wa serikali yake kwa miaka mitano sasa.

Marais wote wastaafu walikuwepo pale kiwanjani wakati Shein akitoa taarifa za majigambo ya serikali yake,, kwamba anatoa matibabu bure, kuna shule hadi za ghorofa zanzibar, wanafunzi wa chuo wanapata mikopo, wanaofaulu Div 1 za form 4 husomeshwa bure zanzibar, uchumi umeimarika sana Zanzibar.

Nilikuwa namuona Shein kama anamuambia Magufuli kuwa kubana mishahara hakumaanishi kuwa pesa za serikali zinamalizwa kwa mishahara, zaidi sana unaharibu uchumi kwa vile pesa ni mzunguko, uliongeza hela mtaani kwa mishahara unamuongezea asiyeajiliwa na serikali pesa yaani wafanyabishara bidhaa zao zitanunuliwa, mafundi wa mtaani watapata kazi nk.

Anachokifanya Magufuli ni kama una duka la bidhaa mtaani, wewe unajua kuuza tu, hununui bidhaa mpya za dukani mwisho wa siku duka linaduwa halina bidhaa na wateja wakija kuulizia bidhaa wewe unasema hakuna.

Hivyo nakushauri Rais Magufuli mwaka huu ongeza mshahara kwa zaidi ya asilimia hamsini kwa kuwa hata mapato ya TRA yameongezeka hadi kufikia TRilioni 1.9 kwa mwezi wakati mishahara kwa mwezi si zaidi ya Bilioni 600 yaani mapato ya TRA kwa mwezi yanalipa mishahara ya serikali kwa miezi mitatu.

Hebu Mheshimiwa fanya majaribio ya kuongeza mishahara kwa asililia 100 kwa miezi mitatu tu then roll back kwenye scale ya kawaida halafu sikilizia mapato ya TRA kwa miezi hiyo, utashangaa.

Hata Yesu alisema pandeni mbegu, mbegu moja huzaa mbegu mia, hiyo ndo formula ya kiuchumi, kwa vile ume control mapato ya serikali hakuna tena wizi fungulia mipesa hiyo.

Kwa kuwa hakuna sehemu pesa za serikali zinatumika kwa wingi kama mishahara kwa wafanyakazi, hiyo ndo simple way ya kusababisha upepo wa pesa kukimbia, hawa wafanyakazi hawakai na hizo pesa bank, wataanza kujenga, kununua magari na hivyo tozo ya petrol kuongezeka, japo ukimwaga sana pesa kwa wingi pia itaharibu uchumi, un afungulia pesa kwa discipline.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu tumepata Rais mshamba kuliko awamu zotee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kuongeza mshahara hadi ufanisi wa wafanyakazi ulingane na wa sekta binafsi. Mfano rahisi ni wafanyakazi wa NIDA wapewe nyongeza ya mshahara kweli?

Aongeze mishahara ya nini ? Wakati vijana wengi wamemaliza vyuo na hawana ajira, bora pesa hizo awape kama 'capital' wafanyie biashara .Kwanini aliyenayo aongezewe?
 
Back
Top Bottom