Ujumbe muhimu kwa wanaume wote

Ujumbe muhimu kwa wanaume wote

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,712
Katika maisha mwanaume inakupasa kufahamu mambo ya msingi yatakayo fanya maisha yako yawe ya furaha, mambo hayo ni pamoja na:

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa changamoto za maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu sawa

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza.

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni na kubadili badili wanawake.

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina yako ya baadae.

Nawasilisha!!
 
Chakuongezea....kama huna pesa yote hayo hayatakua na msaada kwako kwani japo pesa hainunui furaha umaskini nao haununui chochote..tafuta pesa tafuteni pesa..
 
[emoji23][emoji23][emoji23] sa unadhani sangap natunga haya mashairi
Akwambie na alipoikopi

hawa ndo wale waigiliziaji wa mitihani halafu tokeo likitoka amemzidi hadi aliyemuigilizia
 
Back
Top Bottom