Ujumbe muhimu kwa wababa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,704
Mpende mke wako mzuri
Usimkaripie mke wako ukiwa unaongea nae. Inamuumiza sana.
Mithali 15:1

Usimuongelee ubaya kwa mtu yeyote. Mke wako atakua kile ambacho unamuita
Mwanzo 2:19

Usimpe mwanamke mwingine upendo anaostahili mke wako. Huo ni uasherati.
Matayo 5:28

Usimlinganishe mke wako na mwanamke mwingine. Kama huyo mwanamke alikua anakufaa basi Mungu angekupa umuoe
2wakorinto 10:2

Uwe mpole, mvumilivu na msikivu. Amevumilia mengi na amejitolea na ameacha vingi ili awe pamoja nawe. Inamuumiza sana unapokua mkali na kumkera
Waefeso 4:2

Usimfiche chochote. Mmekua kitu kimoja na hivyo ni msaidizi wako, usiweke siri yoyotr kati yenu
Mwanzo 2:25

Usiseme kitu kibaya kuukosoa mwili wake. Amejitolea uzuri wake na mwili wake kukuzalia ww watoto. Ni binadam pia mwenye moyo, sio mwili tu.
Mithali 18:22

Usiulinganishe mwili wake na thamani yake. Mthamini hata pale mtakapofikia uzee
Waefeso 5:29

Usimkaripie kwenye umati wa watu. Suluhisheni matatizo yenu chumbani mkiwa wenyewe.
Matayo 1:19

Mshukuru kwa kuwalea watoto wenu vizuri, nyumba yako pamoja na wewe. Kwani amejitolea kufanya hayo yote.
1wathesalonike 5:18

Mapishi ya wanawake hayafanani. Furahia mapishi ya mke wako. Sio rahisi kumpikia mtu milo mitatu kwa siku kwa siku 365 kwa mwaka kwa miaka mingi mlioishi wote
Mithali 31:14

Usiwaweke ndugu zako kabla yake. Yeye ni mke wako. Ndiye anaekaa na ww. Lazma umpe kipaombele kabla ya ndugu zako.
Mwanzo 2:24

Wekeza katika ukuaji wake kiroho. Mnunulie vitabu, na chochote ambacho kitamsaidia kukua kiroho atembee na Mungu siku zake zote. Hicho ndicho kitu cha pekee unachoweza kumfanyia mke wako.
Waefeso 5:26

Tumia mda wako ukiwa nae kujifunza bibilia na kusali
James 5:16

Tenga mda wa kukaa nae, kucheza nae na kufurahia uwepo wake. Kumbuka, utakapofariki, yeye ndiye ataaesimama pembeni ya kaburi lako. Huenda marafiki zako wakawa na kazi nyingi na kushindwa kuhudhuria.
Mhubiri 9:9

Usitumie pesa zako kumrubuni au kumpelekesha. Pesa zako ni za kwake pia. Mmekua kitu kimoja na ni mrithi wa kila ulicho nacho ulieunganishwa nae na Mungu.
1peter 3:7

Usifichue madhaifu yake. Utakua unajifichua na ww. Mlinde.
Ephesians 5:30

Waheshimu wazazi wake na kuwa na moyo wa upole kwa ndugu zake.
Wimbo ulio bora 8:2

Usiache kumuambia ni jinsi gani unampenda kila siku ya maisha yake. Mwanamke hachoki kusikia hilo.
Ephesians 5:25

Kua katika njia ya Mungu, ndicho kitu kitakacho kufanya uwe mume bora na mwenye hofu ya Mungu.
Warumi 8:29.

OKOA NYUMBA LEO.... Mpende mkeo kwa dhati ya moyo.. Mjali hisia zake na kuheshimu utu wake...!!!

Jr
 
Wewe leo umevaa mabuti ya wanatheolojia

Anyway achana mambo ya msata kilingeni endelea na hii kazi ya wana theology unafiti kinoma, asante sana kwa huu ujumbe
 
Tangu lini giza na nuru vikakaa pamoja?
Uchaw na ushirikina hayo ni mambo ya giza, lkn mafundisho yenye kujenga kama ulivyotuletea leo hayo ni mambo ya Nuru.

Chagua njia moja tu bro
Asili ya dunia ni giza ndio nuru ikafuata

Jr
Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji. Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema.
 
Hayo yote huwa yanaweza kufanyiwa kazi na ku-expire baada ya miaka mitano ya Ndoa.

Baada ya hapo kuna kuonana wakawaida, kuzoeana kunakosababisha kuanza kutamani vitu vipya vya nje. Kisha kiburi na dharau huchukua nafasi hadi kupelekea kunogewa huko nje.
 

Similar Discussions

26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom