Ujumbe Maridadi Kwa Wanaohoji au Kupuuzia Sababu Ya Kitwanga Kung'olewa

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,768
41,009
Hili Neno: Kwa watu wanaoupuuzia au kubeza sababu iliyotolewa na Ikulu juu ya kufukuzwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga ni kuwa ama hawajui uzito wa tuhuma hizo hasa kutokana na wadhifa alionao au hili ni aina nyingine ya goli linalotengenezwa. Wizara ya mambo ya ndani ndiyo inasimamia kati ya mengi sana usalama barabarani; ajali nyingi sana za barabarani Tanzania na sehemu nyingi duniani tu zinahusishwa sana na mtu kulewa. Siyo tu barabarani hata kwenye ajali sehemu nyingine za kazi au vituko vya kumuabisha mtu na wadhifa wake vimewakuta wengi sababu ya kileo.

Rais Magufuli alichofanya - na sijui kwanini wengine hawakioni - ni kuwa amenyanyua kiwango cha uwajibikaji kwamba haiitaji hata uwe 'fisadi' kuweza kutumbuliwa chini ya uongozi wake. Kwamba, hata kulewa kazini ni sababu tosha ya wewe kutokuendelea na kazi! Hili ni gumu kwa ndugu zetu wengine kuliona.

Tutawasaidia tu.. Dakika 5, Siku 5.. Mada 5...

NB: Niliandika juu ya probation ya mawaziri miezi kadhaa nyuma na nilidokeza itakuwa ni ya muda gani... well tick tock tick tock.. hakuna aliye salama... hizi ni ZAMA MPYA! Hofu yangu ni kuwa wale ndugu zetu wapendwa wahamisha magoli watakaposa magoli uwanjani wanaweza kung'oa majani wayahamishe...
 
Ni ngumu kueleweka japo kila siku hujinasibu "fulani aondolewe"..ila hawajui wanachokisema.Ikitokea mtu kaondolewa wao hawakubali sababu ya ikulu husema..ah ah amekurupuka!..laiti kizazi hiki kingekuwepo enzi za Nyerere watu kuondolewa uwaziri ilikuwa kawaida,RC kupelekwa kuwa DC ilikuwa kawaida Waziri mkuu kuwa waziri wa kawaid ilikuwa kawaida.Mwl.Nyerere aliwahi kusimulia kuhusu madaraka na uadilifu,akitoa mfano wa uingereza waziri alikuwa na tuhuma za kutoka na vimada...waziri mkuu uingereza aliteua mbadala bila hata kujibu barua ya aliyejiuzuru.
 
Ni mpuuzi tu ndo atakayeshabikia na kukubali sababu iliyotolewa na Ikulu...

Ina maana Magufuli hakuwahi kusikia hata siku moja kuhusu kashfa ya Lugumi inayomhusu pia mh Kitwanga kupitia kampuni yake ya Infosys?

Anataka kutuaminisha kuwa ulevi (wanaomsingizia) Ndio kosa kubwa la kustahili kutumbuliwa kuliko kashfa ya ufisadi?

Siwezi kuwa mpuuzi ktk hilo.
 
We ndio umehoji vya maana
 
Kuna siku viongozi wote watagomea teuzi, huezi toa sababu eti ya ulevi akat hata HUJAMPIMA KILEVI kisa tu kayumba yumba je kama ni njaa ilisababisha, kitwanga wala si wa kumsingizia ulevi ndo umtoe LUGUMI tu ilitosha kumtoa
 
Huyu Mwanakijiji ndio alikuwa anamtetea sana huyu Kitwanga na jamaa alimuhaidi kupigana kwa Magu...as his best friend ili apate kuteuliwa na Magu.....watu walisha-kustukia siku nyingi na undumila kuwili wako....so hakuna mtu siku hizi anavutiwa na mada zako unazoweka humu....beacause they are like....

Ulikuwepo....but you're credibility has gone.....no longer people believe on your rubish na ndo hivyooo jamaaa katumbuliwa sasa unakuja hapa na swagaaa za kitoto ili tukuone haupo upande wake.....Nonsense!!!!!!!!!!!
 
Ila Mkuu wewe Mwanakijiji ina maana masuala ya "Lugumi" hujasikia kabisa?? Na msimamo wako ni upi? Na unajuaje mtumishi amelewa?
 
Ni mpuuzi tu ndo atakayeshabikia na kukubali sababu iliyotolewa na Ikulu...

Ina maana Magufuli hakuwahi kusikia hata siku moja kuhusu kashfa ya Lugumi inayomhusu pia mh Kitwanga kupitia kampuni yake ya Infosys?

Anataka kutuaminisha kuwa ulevi (wanaomsingizia) Ndio kosa kubwa la kustahili kutumbuliwa kuliko kashfa ya ufisadi?

Siwezi kuwa mpuuzi ktk hilo.
Mtaona kila rangi miaka hii 5 ya magu
 
Kuna wakati Wapinzani tunaonekana kama hatuna akili..... Kilio chetu kilikuwa ni kuondolewa Kitwanga

Ameondolewa, Ushahidi uko wazi kuwa alikuwa amelewa... Lakini bado hatujaridhika..
 
Hili Neno: Kwa watu wanaoupuuzia au kubeza sababu iliyotolewa na Ikulu juu ya kufukuzwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga ni kuwa ama hawajui uzito wa tuhuma hizo hasa kutokana na wadhifa alionao au hili ni aina nyingine ya goli linalotengenezwa. Wizara ya mambo ya ndani ndiyo inasimamia kati ya mengi sana usalama barabarani; ajali nyingi sana za barabarani Tanzania na sehemu nyingi duniani tu zinahusishwa sana na mtu kulewa. Siyo tu barabarani hata kwenye ajali sehemu nyingine za kazi au vituko vya kumuabisha mtu na wadhifa wake vimewakuta wengi sababu ya kileo.

Rais Magufuli alichofanya - na sijui kwanini wengine hawakioni - ni kuwa amenyanyua kiwango cha uwajibikaji kwamba haiitaji hata uwe 'fisadi' kuweza kutumbuliwa chini ya uongozi wake. Kwamba, hata kulewa kazini ni sababu tosha ya wewe kutokuendelea na kazi! Hili ni gumu kwa ndugu zetu wengine kuliona.

Tutawasaidia tu.. Dakika 5, Siku 5.. Mada 5...

NB: Niliandika juu ya probation ya mawaziri miezi kadhaa nyuma na nilidokeza itakuwa ni ya muda gani... well tick tock tick tock.. hakuna aliye salama... hizi ni ZAMA MPYA! Hofu yangu ni kuwa wale ndugu zetu wapendwa wahamisha magoli watakaposa magoli uwanjani wanaweza kung'oa majani wayahamishe...
Well said Mzee Mwanakijiji
 
Kuna wakati Wapinzani tunaonekana kama hatuna akili..... Kilio chetu kilikuwa ni kuondolewa Kitwanga

Ameondolewa, Ushahidi uko wazi kuwa alikuwa amelewa... Lakini bado hatujaridhika..
Wewe siyo mpinzani, wewe ni gamba.
Wapinzani wana hoja zenye mantiki na wingi wa weledi.
Wapinzani si vilaza wanaojikomba kwa viongozi.
Hoja dhidi ya wahujumu uchumi (mafisadi) ni muhimu kuliko kulewa, hata Mkapa alikuwa mlevi na kakaa ikulu miaka kumi.
Haturidhiki na cosmetic changes tunataka amkamate Lugumi na waache kufunga mitambo ya biometric sasa, huo ni uhuni.
Kulitambua hili lazima uwe na moyo wa uzalendo si moyo wa ukada
 
Watu tunapenda siasa hatujali uwajibikaji Kitwana Katenguliwa kwa uwajibikaji mbovu manyumbu Wao kazi siasa za kilofa Na ndio maana wana mwenyekiti Kama mfalme miaka 20.siasa siasa Tu haya maswala ya uwajibikaji
 
Ni mpuuzi tu ndo atakayeshabikia na kukubali sababu iliyotolewa na Ikulu...

Ina maana Magufuli hakuwahi kusikia hata siku moja kuhusu kashfa ya Lugumi inayomhusu pia mh Kitwanga kupitia kampuni yake ya Infosys?

Anataka kutuaminisha kuwa ulevi (wanaomsingizia) Ndio kosa kubwa la kustahili kutumbuliwa kuliko kashfa ya ufisadi?

Siwezi kuwa mpuuzi ktk hilo.

Nakuunga mkono, nadhani tutumie ule msemo kamba hukatikia pa bovu. Haiingii akilini, labda wote walikuwa hawamtaki sasa sababu wataipata wapi? Wasije mwaga ugali akamwaga mboga.
 
Watu tunapenda siasa hatujali uwajibikaji Kitwana Katenguliwa kwa uwajibikaji mbovu manyumbu Wao kazi siasa za kilofa Na ndio maana wana mwenyekiti Kama mfalme miaka 20.siasa siasa Tu haya maswala ya uwajibikaji

Unajenga hoja nzuri kisha unaiharibu kwa kuweka vionjo vya kipuuzi vya kisiasa. Unashangaa kiongozi kukaa miaka 20 madarakani hushangai chama kukaa madarakani miaka 40? Kama hicho chama kiko madarakani kwa kuchaguliwa basi hata huyo mwenyekiti yuko madarakani kwa kuchaguliwa. Acha utoto kwenye hoja za msingi.
 
Back
Top Bottom