Baba mtakatifu91
JF-Expert Member
- Apr 25, 2026
- 3,627
- 7,531
Age Go ndo tatizo unafikiri watu hatupendi kujifunza skills mpya tunatamani sana ila tatizo umriUjumbe kwako wewe mwanaume wa leo, mwanaume mramba lipsi, mwanaume mrembuaji, mwanaume unae amini eti mabadiliko ya sayansi na technologia yatakubadilishia maisha yako (sayansi na technologia scam tu kama scam nyingine) 👊
Hebu sikia!!!... Mwanaume wa kweli hapaswi kujilegeza, kuzubaa zubaa tu (hasa wale wanaojitia wasomi, eti wafanya biashara).. Jifunze ujuzi wa mikono — hata kama ni kujenga banda la mifugo, kupiga plasta, kushika nyundo au kurekebisha vitu vidogo nyumbani. Haya mambo ni muhimu sana na ni sehemu ya maisha.
Inasikitisha kuona mwanaume mzima anamwita fundi aje kumfungia pazia. Kila kitu simu kwa fundi (halafu sasa sio fundi ni mtu tu wa mtaani). Mtoto akiharibu kitu kidogo ndani ya nyumba, suluhisho ni simu kwa fundi. Sasa watoto wanajifunza nini kutoka kwa baba wa namna hiyo?
Uanaume sio kuvaa vizuri na kupost picha mtandaoni (tena inasikitisha sikuhizi wanaume mnarembua na kuramba lips) au kujitia unajua kuongea vizuri na kupangilia maneno. Ni uwezo wa kusimama kwenye majukumu, kutatua changamoto na kuwa msaada kwa familia yako.
Wanaume wa zamani walilea familia kwa kutumia akili, nguvu na ujuzi wa mikono. lakini wanaume wa sasa wanakimbia majukumu ya msingi kwa kisingizio cha usomi, utajiri na techologia, hii tabia ikiendelea tutajikuta tunazalisha kizazi tegemezi.
Kushika nyundo sio fedheha wala aibu. Kujifunza kazi ndogo ndogo au kazi za mikono sio kushuka hadhi. Mwanaume anayejitambua anajua kufanya kazi ndogondogo za mikono na anjifunza kila ujuzi mpya.
Tuache uvivu wa kujifunza kazi mikono. Maana hiyo ndiyo asili ya Uanaume sio kuwa na maneno mengi, kufanya ngono hovyo na kushinda tiktok, facebook au instagram kwa kujifanya content creator. AMKA MWANAUME
Nabisha mkuu mana udongo ni tororli 3 kwa mfuko na unachanganya tepe wa plasta. Kuna kupiga rati hapo kupiga konabao ukuta unyooke mana rati haitakiwi iache tobo!Unakubali au unabisha?
Sasa ugumu upo wapi hapo Mimi sio fundi Lakini kwa maelezo yako tayari nimeelewa na ninaweza kupiga plasta. Maana kazi zingine inabidi ufundishwe practically Lakini hii ya plasta nyepesi tu mkuu.Nabisha mkuu mana udongo ni tororli 3 kwa mfuko na unachanganya tepe wa plasta. Kuna kupiga rati hapo kupiga konabao ukuta unyooke mana rati haitakiwi iache tobo!
Alafu kuna kunyoosha kopla! Koplasenta 😅
Oke oke mkuu, my aim was not to change your mind. Bakia ulipo ila uwe unaelewa unachokiongeaSasa ugumu upo wapi hapo Mimi sio fundi Lakini kwa maelezo yako tayari nimeelewa na ninaweza kupiga plasta. Maana kazi zingine inabidi ufundishwe practically Lakini hii ya plasta nyepesi tu mkuu.
Kutokujua sio sifa lakiniWanaume wengi wenye kazi za maana au biashara za kueleweka hizo kazi za mikono hawajui kabisa,
Kwa upande wa sayansi ya technology Sina maana hiyo.. ukipata time ingia youtube sikiliza hotuba ya jack ma... utanielewa vizuri hapoKoote huko naunga mkono, mwanaume inabidi uwe unajua vitu tofauti tofauti, idea ya umeme kidogo, ujenzi kidogo, mechanics kidogo, useremala kidogo etc..
Lakini hapa unaposema sayansi na teknolojia ni scam nakushangaa napingana na wewe, ama labda mimi ndio teknolojia siijui..
Mfano mie nikichukua ODB nikapima gari yangu na kubadili kifaa, hapo sijatumia teknolojia, kutoka kugonga msumali nikatumia drill hapo sijatumia teknolojia, ama mimi ndio sijaelewa..
Ni kweli mtoto wa kiumr haiwezekani kubadili bulb mpaka uite fundi, lakini teknolojia haikwepeki. Vipi badala ya kupanda kwenye kistuli nikatumia ngazi, hii ngazi sio teknolojia wala sayansi?
Na hapo lazima mke wake akuite Fundi maikoSasa vp na sisi wanaume tunaofanya hizo kazi za kuwatengenezea wanaume Vitu vidogo vidogo vilivyowashinda, tukale wapi
Najua fika kuwa sio sifa, Mungu hakupi vyote,Kutokujua sio sifa lakini
Nielezee hata kwa ufupiKwa upande wa sayansi ya technology Sina maana hiyo.. ukipata time ingia youtube sikiliza hotuba ya jack ma... utanielewa vizuri hapo