Ujumbe kwa WAZALENDO wote wa Taifa hili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujumbe kwa WAZALENDO wote wa Taifa hili.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mcheza Karate, Feb 19, 2012.

 1. Mcheza Karate

  Mcheza Karate JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 691
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu wana CCM, Taifa letu linapotea, Ndio hakika linaangamia, Kimya tumekaa nani ataliokoa, Vipi uzalendo umesafiri au umepotea, Ukweli kueleza nani aibu twamwonea, Tunawalaumu CHADEMA nini wamekosea, Kwa zao nzuri sera kuwapuuza tumeamua , JKT iko wapi imepotelea, CCM sera nzuri nilizifuatia, Sijui wapi zimepotelea, Ndugu zangu nalia, Dira ya Taifa imepotea,

  Nape nipe jibu maswali nakupatia, Kikwete utampatia, Kabla kadi sijawarudishia, Vipi gamba mmelivua, Au bado mmeamua kusubiria, Vipi uvumi tumesikia, Rais ajaye eti amjua, kwa katiba ipi amjua, Nisisahau Mwakyembe kumsemea, Mbona rais kimya kajikalia, Waziri wake mbona aumia, Au wabaya awajua, Nape naomba jibu kunipatia, CCM dira imepotea, Mafisadi au rais wetu nchi atuendeshea, Tuambie ni nani nchi anatuendeshea, Mbona imani imenipotea, CCM nini nitajivunia, Vijana tamaa wanajikatia,

  Maisha magumu yamewakalia, Hakika hili ni bomu tumelikalia, Wanaweza kuasi tukiwapuuzia, Mbona sielewi kinachoendelea, Yenyewe nchi inajiongozea, kwa machache niliyoulizia, Nape jibu utanipatia. ,,,...,,,...,,,...Ndugu zangu mimi si mshairi ila nilikuwa najitahidi kuelezea hisia zangu tu ktk mfumo unaofanana na ushairi. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1991(kukiwa na ulazima wa kutaja namba yangu ya kadi nitaiandika hapa jamvini).

  NAWASILISHA!!!
   
 2. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Pole ndugu yangu. Nape, kama uaweza, uwanja ni wako.
   
 3. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umewasilisha nini?
  Rudi shule kajifunze jinsi ya kuandika mashairi. nina hakina u miongoni mwa 90% ya form IV result 2011.
   
 4. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Pole mcheza karate, hata sisi tulikuwa huko tukaona mambo si yenyewe tukatoka kutafuta njia mbadala ya kujenga taifa letu. Wengi tumeimba sana nyimba za Chama chetu chajenga nchi kumbe kinajenga watu wachache ndani ya chama. Tokeni huko njoo tuangalie Plan B tuone itakuwaje nayo.
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  umekuja kwa kasi na utapotea kwa kasi vile vile, waulize wenzio akina FF na MS
   
 6. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Unadhani wazalendo wote wapo ccm?
   
 7. T

  Tewe JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Pole kama bado unasubiri majibu ndio urudishe kadi, kwa wenye akili tulipo waangalia tu tulushapata majibu tukawarudishia mikadi yao.
  Hujui sisiemu ni janga la taifa?
   
 8. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hongera kwa kuchagua fungu jema
   
 9. Mcheza Karate

  Mcheza Karate JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 691
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  ahsante kwa ushauri, natazama uwezekano wa kukijenga upya chama chetu. Itakaposhindikana nitachukua uamuzi mwingine tofauti. Tumekutanishwa CCM kwa itikadi na mtazamo tu. Wakiendelea hivi wanavyofanya ah! Ah! Ah! Ah! Ah!
   
 10. Mcheza Karate

  Mcheza Karate JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 691
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  pole sana mdogo wangu, Samahani kwa kukukwaza, kwa nini unataa asili yako? Wewe mtumwa? Tazama lugha uliyotumia. Ni vituko tupu. Mimi binafsi sijasoma sana, lakini mwenzangu msomi hebu ona lugha zote ulizotumia hapo? Je uko sahihi? Mpigie simu yule mwalimu wako aliyekupa DIV. 0. Nakupongeza kwa kutoa mawazo yako kijana. Lakini nasikitika sana kwa kijana kutokuwa na mawazo na fikra pevu. Vijana kama ninyi mnanifanya niamini kuwa hamfai kutegemewa kupatiwa nafasi ya kuongoza
   
 11. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hahaaaa, FF bwana ni mjanja sana, mi huwa nasoma sana postings zake hapa jf. Anaonekana mtu wa ciciem lakini sometimes anaonekana anakula kote kote, tawala na upinzani. Na kwavile M/kiti wake alishasema ukitaka kula sharti nawe uliwe, sielewi kama huwa anakula kote kote atueleze hapa naye huwa analiwa kote kote??. FF bwana!
   
Loading...