Ujumbe kwa Watanzania. Nawatakia Usiku Mwema

Ujumbe kwa Watanzania. Nawatakia Usiku Mwema

Avith almachius

Senior Member
Joined
Aug 20, 2022
Posts
167
Reaction score
170
Hadharani una furaha, sirini unalia.
Hadharani ni maarufu, sirini ni mpweke.
Hadharani ni jasiri, sirini mnyonge.
Hadharani una hekima, sirini ni mjinga.
Hadharani ni mwema, sirini ni mwovu.
Hadharani ni mcha Mungu, sirini ni mshirikina.
Hadharani umeridhika, sirini una roho mbaya.
Hadharani una utu, sirini ni mnyama.
Hadharani unapenda familia, sirini umeitelekeza.
Hadharani ni mwaminifu, sirini unachepuka.
Hadharani una bidii, sirini ni mzembe.
Hadharani umefanikiwa, kwa siri huna uhakika na kesho.

Tunatumia nguvu kubwa kujenga ukamilifu tusiokuwa nao. Tunatumia nguvu kubwa kuonesha sura za mafanikio tusiyokuwa nayo.
 
Back
Top Bottom