Habari
Kwa wale wanaume wanachuo wote ambao wamepanga na wamechukua mabinti za watu wanachuo na kuishi nao. tunaomba muwe wastaarabu na wenye huruma, watoto wa watu wamekuja kusoma nyie mnawafanya wake zenu,wanawapikia, kufua, kudeki na hata kuwaogesha, lakini bado mnawanyanyasa kwa kuwapiga utafikiri mmeshaoa kabisa.
Akichelewa tu kurudi kosa vibao na mateke, akisema leo sitaki naniliii vibao na kumlazimisha, yani mnapiga kama vile mmeshalipia mahali. mnasababisha hata maendeleo kimasomo kushuka.Tafadhali jamani msiwanyanyase kuweni na huruma au msubiri kuja kuwapiga wake zenu.
Kinachosikitisha zaidi mnawapiga na mkimaliza chuo ndio imetoka hiyo eti unaenda kutafuta mke mwema mbele ya safari vibaya sana,sijabuni nimeona sana jinsi wadada wanavyonewa.
Be kind you men.