Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,461
Jana nimekutana na binti mmoja! Binti ambaye miaka takriban kumi na mmoja iliyopita alifunga ndoa ambayo nilishiriki kwa 100% lakini baada ya mwaka na nusu ndoa ile ilivunjika!!
Sikujua ni nini kilisababisha sababu hatukiwa na mawasiliano thabiti mpaka jana ndipo kanipa story halisi! Kwangu nimehisi hii story yaweza kuwa ujumbe murua kwa vijana mnaotaka kuoa na kuolewa!!
Kwa madai yake! Ndoa yake ya kwanza ilivunjika sababu za ulimbukeni wa maisha na mali alizomkuta nazo mumewe!! Aliolewa na kijana ambaye tayari alikuwa anamiliki nyumba nzuri na gari nzuri kwa wakati huo na miradi kadhaa yeye alijua michache tuu!!
Kama mke alijikuta hana say ya hizo mali, mume ana mdharau, hamjali kihisia japo kimwili alimpa kila kitu!
Mbaya zaidi mume hakuwa muwazi kwa shughuli zake za kichumi na alikuwa anaondoka na kurudi muda wowote hata iwe saa kumi na moja alfajiri na hataki aulizwe wala kutafutwa kwa simu!! Kifupi mienendo, mali na shughuli za mume yeye zilikuwa hazimuhusu kabisaa kitu ambacho kama mke hakukubaliana nacho!
Na kero nyingine nyingi ila kifupi alimkuta jamaa tayari ana system ya maisha yake ambayo ilishampa mafanikio hivyo hakuwa tayari kubadilisha baadhi ya system kwa kuijali ndoa yake. Mume akawa anaishi kama bado hajaoa na hajali kama kuna mtu wa karibu yake mwenye wajibu kujua mienendo yake ya kila siku.
Binti akaona ujinga huu, mbona mi nimeacha yangu kwa ajili yake then yeye hataki kuondoa yanayonikirihisha!? Akaondoka kwa kuaga kuelekea Arusha!! Then alipofika huko akatoa taarifa ya kutokurudi tena ndoani!!
Baada ya mwaka mmoja wa kutafutana bila mafanikio akarudi kudai talaka yake ndoa ikafa rasmi!!
Aliamua kupambana na ujasiria mali huku akitafuta ajira, akawa pia na kanuni mpya ya kupata mume!! Asiwe tayari na mafanikio 😲😩😂.
Baada ya miaka kadhaa akapata kijana mwenzie ambaye hakuwa na maisha pia ila alikuwa na elimu na maono!! Wakaanza kupambana pamoja na kufunga ndoa yao!
Actually nilionana nae for the first time siku tatu nyuma tukapanga kuonana jana!!
Jana nilipoonana nae, anasema kwa sasa ana nyumba kadhaa magari kadhaa waliyonunua pamoja na mumewe pamoja na miradi midogo midogo huku wote wakiwa waajiriwa tayari!! Anaheshimika kama mke, kama mama wawili na hisia zake zinalindwa!!
Tuliongea mengi lakini mwisho nikataka kujua mtazamo wake kuhusu ndoa! Nikamuuliza, Unawashauri nini wanaotaraji kuoa na kuolewa!!
Alisema!! Better kuingia kwenye uhusiano na mtu mkaanza maisha pamoja kuliko kukimbilia mahusiano na mtu mwenye mafanikio tayari ambaye keshajijengea mifumo ya maisha yake ambayo huwezi kumbadilisha, mali zake hazikuhusu ndo ile ukigusa kitu anakwambia unajua thamani yake hiyo??
Nikawaza vijana hawa wanaokimbilia ndoa kwa wenye nazo! Lakini mwisho wa siku kila mtu na bahati yake!!
Vijana mpo? Experience matters ndiyo hii sasa, mzoefu katoa yeke. Nauleta ujumbe kwenu watarajiwa mchanganue na kupima vyema mahusiano yenu pengine unaweza kujikuta unarekebisha mahali!!