UJUMBE KWA VIONGOZI WA DINI

UJUMBE KWA VIONGOZI WA DINI

Antonio Conte

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2017
Posts
1,089
Reaction score
1,748
Kiongozi wa dini kama atakuwa mfungwa wa mfumo hataweza kumwakilisha Yesu au dini yake bali ibilisi, kiongozi wa dini anapaswa kufanya haki na si kukaa upande mmoja. Taifa linapaswa kujifunza maarifa kwake ‘’Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi. Malaki 2:7. Kiongozi wa dini kama atakuwa mjumbe wa serikali hafai kuwa mjumbe wa Mungu, maana hakuna hawezaye kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Siasa na dini si mapacha, mpe ya Kaisari yaliyo ya Kaisari, na mpe Mungu yaliyo yake. Kiongozi wa dini ukichanganya hayo mambo mawili sharti utamchukia huyu na kumpenda huyu, ama utashikamana na huyu na kumdharau huyu. Mungu alitenganisha ukuhani na ufalme, daima hizo ofisi hazikushimana, maana Mungu alijua athari za kuchanganya, ni mfalme Uzia aliyetaka kuchanganya hizo ofisi mbili, na Mungu akampiga ukoma kama kemeo kwake na hakuzikwa katika makaburi ya wafalme. Leo viongozi wa dini wana ukoma wa maarifa na hawafai kuwa viongozi wa dini, maana wanazitumia mimbari za NENO kisiasa badala ya kulisha kondoo za Yesu, agizo la Yesu ni hili ‘’…LISHA KONDOO ZANGU. (Yohana 21:17).

Lakini leo viongozi wa dini wametawanya kondoo wa Yesu kwa kuwagawa kichama, ccm vs ukawa, na neno limetupiliwa mbali, wamekuwa wana siasa katika joho la uaskofu ni hatari sana. Kiongozi wa dini unapaswa usiwe na upande, unapaswa kuwa huru ili uweze kukemea dhambi za mtu, kundi,chama ama taifa. Tujifunze kwa nabii Yohana Mbatizaji, huyu bwana alikemea dhambi za watu wote, wakiwemo maskari, viongozi wa dini, na wakusanya kodi(TRA ya wakati huo) na mwisho alikemea dhambi za watawala mpaka akafungwa. Nitanukuu sehemu hiyo:- ‘’BASI, KWA MAONYO MENGINE MENGI ALIWAHUBIRI WATU. LAKINI MFALME HERODE ALIPOKARIPIWA NA YEYE KWA AJILI YA HERODIA, MKE WA NDUGUYE, NA MAOVU YOTE ALIYOYAFANYA HERODE, LUKA 3:18-19. Aliweza hivyo kwasababu yakutofungamana na upande wowote, ila wale viongozi wengine wa dini walikuwa ni watumwa wa Herode(serikali) maana walipata maji ya kunywa hapo, hawakuwa na sauti zaidi ya kuwa watumwa wa watawala. Waliishia kujifanya watetetezi wa taifa na watawala kwa kigezo cha Amani, hata wakati Yohana anakamatwa walipiga kimya maana alikuwa kero kwao, Yohana akauawa uwenda wakafikiri sauti ya karipio imekoma, maana aliharibu dili zao hasa pale alipokuwa anawaita wanafiki na kuwatangazia hukumu. Lakini mda wasio dhani aliibuka zaidi ya Yohana, yaani Bwana Yesu naye akawa mwiba kwa maslahi yao, wakatafuta namna ya kumkamata na kumshitaki kwa watawala kwamba Yesu anapotosha taifa, na kuzuia ulipaji kodi, ebu soma hapa ‘’WAKAANZA KUMSHITAKI, WAKISEMA, TUMEMWONA HUYU AKIPOTOSHA TAIFA LETU, NA KUWAZUIA WATU WASIMPE KAISARI KODI, AKISEMA KWAMBA YEYE MWENYEWE NI KRISTO, MFALME. LUKA 23:2.

Hawa viongozi wanafiki hawakujua matokeo ya kuwahujumu viongozi wenzao wa dini kwa kujipendekeza kwa serikali dhalimu, matokeo yake taasisi ya dini ilidharauliwa na watawala, na kutawalia na serikali, na mwisho serikali hiyo ya Kirumi iliwaangamiza hata hao viongozi wajipendekezao, maana walijiuza na kuuza uhuru wa dini kwa serikali, wakafikiri watakuwa salama, kumbe walijichimbia kaburi lao wenyewe na kupotezwa. Wewe kiongozi simama na Bwana na uwe mwanana ‘’TENA HAIMPASI MTUMWA WA BWANA KUWA MGOMVI; BALI KUWA MWANANA KWA WATU WOTE, AWEZAYE KUFUNDISHA, MVUMILIVU; AKIWAONYA KWA UPOLE WAO WASHINDANAO NAYE, ILI KAMA IKIWEZEKANA, MUNGU AWAPE KUTUBU NA KUIJUA KWELI;..2 TIMOTHEO 2:24-25. Tena hupaswi kutukana wala kuonya kwa matusi. ‘’Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Wakolosai 3:8
 
Back
Top Bottom