Ujumbe kwa Rais John P. Magufuli...

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
"..Serikali ninayoiongoza, ilichaguliwa na masikini...Kama matajiri walifikiri nitakuwa upande wao basi wamenoa. Mimi nilichaguliwa na masikini na nitawatumikia masikini na si matajiri."-Rais John Pombe Magufuli.

Kwa heshima na taadhima kwa kiongozi wangu wa nchi. Sidhani kama hii ni kauli sahihi au ulifikiria kwa umakini wakati ukiitoa.

Msheshimiwa raisi, wewe ni raisi wa wote hupaswi kuwa kwa maskini wala matajiri, bali jukumu lako ni kusimamia sheria na taratibu katika nchi. Na kuongoza nchi kwa haki na uadilifu bila kuchagua kina nani walikuchagua na Kina nani hawakukuchagua.

Kuwa tajiri si dhambi na ni sifa kuwa na matajiri ili mradi wanalipa kodi na kuchangia maendeleo ya nchi. Sisi kama nchi bado tunahitaji uwekezaji na mitaji. Ili nchi yetu iendelee.

Unawahitaji matajiri kama wao wanavyokuhitaji wewe. Hupaswi kuwa upande wowote. Wote hao ni watanzania na wananchi wako. Na wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi hii.

Ijulikane kwamba matajiri sio maadui wa nchi hii. Na wala yasitengenezwe mazingira ya kujenga uadui huo kati ya wasio nacho na walionacho. La msingi ni watu kufuata sheria.

Serikali itengeneze mazingira mazuri ya biashara ili mitaji iliyopo isiondoke na ili kuvutia uwekezaji wapya. Na kuwapa imani wawekezaji wengine usalama na mazingira bora ya kuwekeza.

Naomba awe makini sana katika kutatua changamoto mbali mbali zinazotukabili. Tunahitaji busara zaidi kuzitatua.

Tunatatizo kubwa la ukosefu wa ajira, hii mitaji iliyopo ikiondoka hali itakuwa mbaya. Uwekezaji ukipungua tutaleta shida kwenye nchi.

Tunatakiwa tuheshimu michango ya watu ambao wanasaidia nchi hii kukua kiuchumi sio kuwa maadui wao.

Tukae chini tujadiliane ni namna gani tutaweza kuondoa tatizo la ajira nchini kwetu ndio la msingi. Ni namna gani tutalinda mitaji iliyopo na kuvutia mitaji mipya na uwekezaji.

Kodi za watu hawa ndio zinachangia kwenye huduma mbalimbali za kijamii na hata ulinzi wa taifa letu. Na tutaweza kupunguza tatizo la ajira kama tutakaa pamoja na kujadili mbinu za kukabiliana na tatizo hili .

Nchi nyingi zinatafuta watu wenye mitaji kwaajili ya uwekezaji tusiwatupe. Maskini hawana mitaji. Lakini pia hatupaswi kuwaabudu matajiri. Lazima kuwepo na pata nipate na kuheshimiana kwa pande mbili ikiwepo kulipa kodi.

Vyombo vyetu vya kusimamia sheria kama takukuru na polisi viimarishwe na pamoja na mamlaka ya mapato kwa kuongeza ufanisi, nidhamu na maadili yake.
 
Mkuu Shayu,

Kwanza nakupongeza kwa kumkosoa mh. Rais kwa sababu pamoja na kazi nzuri anayoifanya kumekosakana watu wa kumkosoa katika baadhi ya maeneo. Rais anaongozwa na azma njema but lazma njema lazima ifuate taratibu zinazokubalika.

Hata hivyo viongozi hutoa kauli maalum kwa mazingira maalum. Historia inatuonesha miaka michache iliyopita uhusiano wa BAADHI matajiri na viongozi ulileta dhiki kwa maskini. Hivyo ilijengeka picha kuwa Rais ni wa matajiri sio wa maskini.

Maana inatia shaka tajiri ambaye hajawahi kununua hata andazi moja na kumpa maskini lakini wakati wa kampeni anatoa hadi milioni 500; kuchangia kampeni. Wakati fulani tajiri moja alifahamika kama rais anayeishi nje ya ikulu!

Ilikuwa ni muhimu kwa wakati huu rais kutoa hiyo kauli. Cha muhimu ni kuwa hakusema atafukua madhambi yaliyopita.
 
Mkuu Shayu,

Kwanza nakupongeza kwa kumkosoa mh. Rais kwa sababu pamoja na kazi nzuri anayoifanya kumekosakana watu wa kumkosoa katika baadhi ya maeneo. Rais anaongozwa na azma njema but lazma njema lazima ifuate taratibu zinazokubalika.

Hata hivyo viongozi hutoa kauli maalum kwa mazingira maalum. Historia inatuonesha miaka michache iliyopita uhusiano wa BAADHI matajiri na viongozi ulileta dhiki kwa maskini. Hivyo ilijengeka picha kuwa Rais ni wa matajiri sio wa maskini.

Maana inatia shaka tajiri ambaye hajawahi kununua hata andazi moja na kumpa maskini lakini wakati wa kampeni anatoa hadi milioni 500; kuchangia kampeni. Wakati fulani tajiri moja alifahamika kama rais anayeishi nje ya ikulu!

Ilikuwa ni muhimu kwa wakati huu rais kutoa hiyo kauli. Cha muhimu ni kuwa hakusema atafukua madhambi yaliyopita.
Ukweli ni kwamba hapaswi kuwa upande wowote bali kuongozwa na mizani ya haki kwa watu wote na kutumia busara katika maneno. Nasema tena hapaswi kuwa upande wa maskini wala matajiri. Anawajibika kufuata sheria na taratibu za nchi bila kujali kipato cha mtu.
 
kamili nadhani hukuipata vema hoja ya Shayu , napenda nichangie kidogo

Shayu anasema ukweli, Rais ni kiongozi wa wote hata waliopo magereza
Ni mlezi wa kila mmoja, si masikini , si tajiri si mfungwa n.k.

Kauli yake hayupo upande wa matajiri ni ya kibaguzi. Je, atasemaje kuhusu wafungwa?

Utajiri si kosa au dhambi. Hivi Bill Gate, Warren Buffet, Bakheresa au Dangote wana makosa gani kutumia bongo zao kupata utajiri! Ni nani asiyetaka utajiri dunia hii?

Matajiri ndio wanaoitwa wawekezaji, wawe wa nje au wa ndani.
Kuwatenga kwa lugha ni kuwatisha na hiyo haifai kwa mlezi wa Taifa

Tujiulize, matajiri wameajiri watu kiasi gani?
Na mchango wao kupitia kodi ni kiasi gani, au kupitia biashara zao ni kiasi gani?

Tusisahau moja ya sifa za matajiri ni uwezo wa kushawishi 'lobbying' kwa masilahi yao.
Kwa bahati mbaya viongozi wamegeuza hilo kuwa rushwa.

Ndio hao anaosema mkuu wanatoa pesa za kugharamia siasa.
Swali, wale wanaopokea wana maadili gani ya kufanya hivyo?

Hatari ya kauli ya Rais ni aliyosema Nyerere,dhambi ya ubaguzi haikomi inaendelea

Akimaliza matajiri atawatenga wapinzani.
Nako akimaliza atawatenga watu kwa kitu kingine. Fikiria itakapofika ktk ukabila au dini

As long as Tajiri anatimiza wajibu wake, hakuna sababu wala kosa la kuwatenga
 
Back
Top Bottom