Mangi flani hivi
JF-Expert Member
- Jan 2, 2016
- 2,026
- 3,104
Salaam,
Kwanza nikupe pole mh. Mwigulu Nchemba kwa starehe za krismas. Nimekuona leo unazurura Huko timu wasafi hongera.
Labda nianze kwa kusema tumechoka kuzika vijana wetu na hasa nguvu kazi ya taifa hili changa kwa sababu tu ya kitu MADAWA ya KULEVYA. Kama hawa watu wasio na majina huku mitaani hawakushtui sasa nitakutajia majina ya vijana wachache ambao walikuwa na nguvu ya kulichangia pato la taifa na kupeperusha jina la Tanzania nje ya mipaka lakini kwa sababu ya hayo madawa hawapo au hawawezi tena;
Ngwea- RIP
Langa- RIP
Fanani- Sijui
Ray C- hakuna kitu
20%- Tia maji Tia maji
Na sasa Chidi Benzi
Mheshimiwa, hivi ni vifo ambavyo wizara yako kwa umakini wake inaweza kabisa kuzuia. Mbona umekuwa kimya juu ya hili mkuu??? Una watoto baba, unajua hujavuka mto. Hebu usiwe sababu ya machozi kututiririka mashavuni kila siku Mheshimiwa.
Hivi unajua mama Makwiro anajisikaje akimwangalia mwanae??? Najua kuna watakaosema kajitakia ila mkuu usipouzuia huu unga kwa nguvu, let "ancestors wrath" rain on (na laana ikuangukie) tumechoka.
Nimeangalia pich za chid zinazozunguka mitandaoni nikashindwa kuelewa nani atatuimbia wimbo Kama: Dar stand up, nipe raha ya dunia na nyingine nyingiiiii.
Namaliza kwa kusema tumechoka, usipozuia kifo cha chidi una Kesi ya kujibu mbinguni na duniani.
Ngoja nikimkumbusha chid ninayemjua.