Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 21,397
- 15,498
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amewaasa wananchi kuacha kugombana kwa sababu za siasa kwani kitendo hicho kinasababisha maafa, yatima, wajane na kukosekana kwa amani.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo kwenye kilele cha Makambi alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista (Wasababato) Mjini Katoro, Mkoani Geita.
Dkt. Nchemba amewaasa waumini hao kuepuka kujihusisha na siasa za fujo na vurugu kwa sababu zinaleta madhara makubwa kwa familia moja moja na nchi kwa ujumla hivyo kuathiri uchumi, umoja na mshikamano wa taifa.
Aidha, Dkt. Nchemba amewataka waumini hao kuendelea kumwombea Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili aendeleze kudumisha maelewano, mshikamano na kusikilizana ambazo ndio zimekuwa falsafa zake tangu aingie madarakani
===
Ndugu zangu Watanzania,
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.