Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
NIngependa kutoa wito kwa Mkuu wa MKoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aongeze bidii katika kuufanya mkoa wa Dar es Salaam uwe wa kijani zaidi kwa kufanya kampeni ya upandani miti na maua eneo la ndani ya jiji. NImeangalia kwa mfano, hili eneo la flyover Tazara na kuona kwamba linaweza kupendezeshwa hata zaidi. Sehemu nyingi duniani barabara inayokwenda airport huwa inapendezeshwa sana kwa miti ya maua.
Ningependa kumkumbusha Makonda kwamba kwa kuwa jiji la Dar es Salaam linazidi kujengwa mchana na usiku, jitihada hizi zifanywe kupanda miti pamoja na ile ya maua ili isije ikatokea jiji letu likageuzwa kuwa concrete city.
Na pia bwana Makonda, ikibidi basi amri na itolewe kwamba nyumba zote za Dar es Salaam ziezekwe kwa mabati ya rangi au yaliyopakwa rangi. Unapoingia Dar kwa ndege nyumba zinaonekana chafu sana, unachoona ni kutu tu ya mabati. Inatia aibu sana kwa sababu kwa wageni wengi hiyo inakuwa first impression ya Dar es Salaam, kwamba sisi ni wachafu hatu-fanyii nyumba maintanance. Na huenda mabati yenye kutu yana athari kiafya kwa maji yanayotiririka toka kwenye bati.
Kwa ujumla ningependa Raisi Magufuli ahimize jambo hili kwa wakuu wote wa mikoa na wilaya. Kuna miji ukienda inatia aibu kwa kuwa unachoona ukiwa mjini ni majengo tu hakuna miti ya kupendezesha mandhari. Majengo ni machafu hata rangi hayapakwi na wala hakuna miti wala maua.