Wapendwa wana JF, ningependa sana nianze kwa kuwapongeza kwakuwa na michango yenu mizuri na upeo mzuri katika kuchanganua mambo.
Clouds Fm especially kipindi cha Pb na Jahazi vimeanzakutoka nje ya mipaka yao na wamekosa has mwelekeo wao nini,Maana siku hiziwamekuwa watu wa majungu na matangazo ya wadhamini wa vipindi hivyo.
Nitatoa mifano ambayo imesababisha mi kusema hivyo.
Siku ambapo Dr.Mwakyembe alipotangaza kuwasimamisha baadhiya watendaji katika shirika la ATCL, vipindi hivi viliponda sana na kusemamaneno mengi sana bila kumfuata kwanza muhusika na kummuliza imekuwaje mpakaakafikia uamuzi huo.Waakati wa PB G.Hando na P.James waliongea sana kwa kumwitakiongozi huyo ni mkabila,amekurupuka nk. Kama waliona huyo kiongozi amekulupukawalipaswa wamtafute kwa wakati wao wamuulize maswali yao na baadae wangeletamajibu hayo katika station yao,kweli ningewakubali wanaijua kazi yao,Na kamakiongozi huyo walimwoma ni mkabila,anakulupuka basi ina maana hata aliyemchaguakuwa waziri ALIKULUPUKA NA NI MKABILA PIA.
Ilipofika jioni kwenye JAHAZI napo mambo yalikuwa kuwa yeyeni mkabila,ameonea watu,alipaswa aelewe ATCL kwanza,Kibonde aliponda sana. Cha kushangaza siku ambayo Mwakyembe alivyotoa sababu za yeye kufanya hivyo,Kibondealimsifia sana na kumuona kuwa ni kionmgopzi mzuri na alifanya maamuzi sahihi. Jehapo tunajifunza nini kwa Kibonde(mnafiki).
Mnyika aliposema bungeni kuwa Kikwete ni Dhaifu pamoja naserikali yake,next morning Gerald Hando aliongea sana kwa uchungu na kwa kuonakuwa UDHAIFU ni tusi,Mi nafikiri kwa mtu kama yeye angetafasiri maana yaudhaifu,na atambue kila binadamu ana udhaifu wake,kuitwa we ni dhaifu inapaswaufuatilie ujue udhaifu wako nini.Alitumia dakika 15 ye kumtusi pia Mnyika mbonamyika hajamfuata na kumuambia mbona umeniita mshamba,mjinga nk.Gerald handojaribu kulinganisha na Mnyika afu nadhani uatweza kuona Tofauti ya NYANYA naTENGA.
USHAURI WANGU
Kwanza mnapaswakujua siasa ya Tz inabadilika kila kukicha,leo unaweza ukawa mshabiki wa mtu auchama Fulani lakini kesho huyo mtu au chama kikakuona hufai au kikapoteza nguvuya utawala
Pili mnapaswamjue kuwa nyinyi ni sehemu ya jamii na jamii ni sehemu yenu,mnapoanza kuibaguajamii na kujifanya nyie ndio mna uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko wengine nakujiona nyie ni wasafi kuliko wengine mnakosea sana.
Tatu,Jaribuni kusomahistoria ya vyombo vya habari na watangazaji waliosababisha maafa Kenya,Rwandana kwingineko ambako matatizo kama hayo yalitokea
Nne mkumbuke kuwammeajiliwa na mtu binafsi hivyo likitokea na kutokea mtasimama wenyewekupigania haki zenu,kwa jinsi navyowafahamu waajili wa Kitanzania watakuachiakesi na itakusumbua wewe mwenywe na mwisho utafungwa,angalieni waandishi wahabari waliopata matatizo waajili wao wamewasaidia kwa muda mfupi tu na baadaekuwatumbilia mbali.
Tano ,kama mnakitu mnataka kukiongea muwaruhusu watu watoe michango yao kwa kupiga simu na sikwa MSG ambazo mnafuta zile zinazopinga mawazo yenu na kuacha zinazowasifia.