Wimbo mzuri kwa harakati za mabadiliko. Naweza kuupataje kwenye CD?
Kuna nyimbo nyingi sana nzuri za ukombozi lakini hazipati hasaa wa kusikika redioni.
Kuna Msanii toka Chunya wanamuita Nabii- ana wimbo wake wenye maneno 'ni marafiki wanapohitaji kura, kuiba na kujiuzulu ndio yao staili' unasadifu sana maneno ya wimbo huu. Kuna mtu anao huu pia kwenye CD?
Halafu kuna nyimbo za vyama vya upinzani nazo hazipati kabisa fursa ya kusikika redio; mathalani CHADEMA kuna msanii anaitwa Mwana-Cotide naye kuna nyimbo zake kadhaa.
Kuna haja ya nyimbo kama hizo kuwepo kwenye radio na televisheni za mtandaoni na kusambazwa pia kwa wingi vijijini kwa njia mbalimbali.
JJ