Ujumbe: Baba anasahau

Humilis

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
882
1,038
BABA ANASAHAU.
(Kwa wazazi,walezi na kila mmoja)

Sikiliza,mwanangu.
Nasema hili ukiwa umelala,mkono wako ukiwa umekunja na kuuweka chini ya shavu lako na nywele zako zenye unyevu,za kahawia zikiwa zimenasa katika paji la uso wako.
Nimeingia kwenye chumba chako kwa siri,peke yangu.Dakika chache zilizopita,nikiwa najisomea,mawazo ya majuto yalinipitia.Nikajiona mkosaji,nimekuja kwako.

Hivi ni vitu nilivyokuwa nafikiri mwanangu.Nimekua msalaba kwako.Nilikukaripia ulipokuwa ukijiandaa kwenda shule kwa sababu ya kusafisha uso wako kwa kufuta na taulo tu,bila kunawa.
Nilikuadabisha kwa kutosafisha viatu vyako.Nilikaripa kwa hasira nilipokuta umerusha vitu vyako sakafuni.

Katika mlo wa asubuhi,niliona makosa yako pia.Ulimwaga vitu ovyo.Ulikua ukila vibaya.Ulikua ukikaa vibaya mezani wakati wa chakula.Ulipaka siagi nyingi kupita kiasi katika mkate wako.Na ulipokuwa ukitaka kucheza,wakati wa mimi kuondoka,ulinipungia mikono ukisema,"Kwa heri baba",lakini nilikunja uso nikijibu,"shusha mabega yako chini".

Pia wakati wa mchana kuelekea jioni,niliporudi,nilikuchunguza chini ya magoti yako,ukichezea golori za marumaru.Kulikuwa na matobo katika soksi zako.Nilikudharirisha mbele ya rafiki zako kwa kukulazimisha uingie ndani,nikifuata nyuma yako."Soksi ni gharama - kama ungekuwa unanunua wewe,ungezitunza".Vuta picha mwanangu,maneno kama hayo kutoka kwa baba yako.

Unakumbuka,baadae,nilipokuwa najisomea,ulipokuja kwa woga,ukionesha sura ya maumivu,sura ya kuumia??
Nikaendelea kuangalia karatasi zangu,ukasimama kwa hofu mlangoni."Unataka nini?,nilifoka.

Hukusema chochote,lakini ukanikimbilia ukirusha mikono yako kuizungusha katika shingo yangu na kunibusu,mikono yako midogo ukiikaza kwa hisia za upendo ambazo Mungu ameujalia moyo wako,ambazo hata puuzo haliwezi kuzikataa.Halafu ukaondoka,ukipanda juu ya ngazi kuelekea chumbani kwako.

Ndio mwanangu,punde baada ya kuondoka,karatasi ziliniteleza mikononi mwangu na hofu kubwa ya kutisha ilinijia.Ni tabia gani nimekuwa nayo?Tabia ya kutafuta makosa,tabia ya kulaumu,hii ndo ilikuwa zawadi yangu kwako kwa kuwa mvulana mdogo.Sio kwamba sikukupenda,ni kwamba nilitegemea makubwa ya ujana kutoka kwako.Nilikupima na kukuhukumu kutokana na namna nilivyoishi miaka yangu yote.

Lakini kulikuwa kuna mengi mazuri,ya kweli na ya kupendeza katika tabia yako.Moyo wako mdogo ulikuwa mkubwa kama machweo ya jua katika vilima vikubwa.Hii ilionekana katika upendo wako mkubwa,uliponikimbilia na kunibusu kunitakia usiku mwema.Mienendo yangu yote haina maana,mwanangu.Nimekuja pembeni ya kitanda chako katika giza,nimepiga magoti,nikiona aibu.

Najua usingeelewa haya kama ningekuambia ukiwa macho ukinisikiliza.Lakini kesho nitakuwa baba mwema na mzuri.Nitakuwa rafiki yako na nitateseka ukiteseka na kucheka ukicheka.Nitauma ulimi wangu pale ambapo maneno mabovu yatakapotaka kunitoka.Nitarudia kusema;"Yeye si chochote bali mvulana mdogo".

Naogopa nimekuwa nikikuchukulia na kukuona kama mwanaume,mtu mzima.Lakini nakuona sasa,mwanangu,ukiwa umejikunja na mchovu ndani ya shuka lako.Nakuona bado mtoto.Ni jana tu ulikuwa katika mikono ya mama yako,kichwa chako kwenye mabega yake.Nimeomba mengi,mengi sana.

Na W.Livingston Larned

Tafsiri na Innocent J. Kadono

Badala ya kulaumu,tujaribu kuelewa watu.Ebu tujaribu kuelewa ni kwa nini wanafanya hicho wanachofanya.Kufanya hivyo ni kuzuri na kwenye faida kuliko kulaumu.Kunaleta huruma,uvumilivu na wema.
"Kujua yote ni kusamehe yote"
 

Attachments

  • IMG_20160723_160801_067.JPG
    IMG_20160723_160801_067.JPG
    11.6 KB · Views: 41
Back
Top Bottom