Ujue mji wa Kahama na viunga vyake

Ujue mji wa Kahama na viunga vyake

Nilikwenda Kahama nikiwa na lengo la kutalii kwa siku mbili tu, nikajikuta nimekata wiki nzima. Kamji kamechangamka sana
 
Kahama Tunduma Babati ni miji midogo inayoongoza kwa kuwa na gesti lodge nyingi
 
Kahama inakata roho..mgodi umeshafungwa
Garii limeishawaka Kahama, kufungwa kwa migodi mikubwa haina impact kubwa kwa mji, Kahama haitegemei migodi mikubwa tu. Kuna migodi midogo ya wananchi ambao wakichimba mapato yao yanaingia kwenye mzunguko palepale mjini (Mwime, Mwabomba, Nyangarata). Kilimo cha mpunga, tumbaku, pamba, mahindi na Karanga ni moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya mji. Biashara za mifugo hasa ng'ombe wa kunenepesha, biashara za maduka makubwa ya jumla ambayo asilimia kubwa ya wateja ni wakulima wa kahama na baadhi ya miji ya karibu na mipakani.
 
Mji wa Kahama ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi Tanzania. Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara ya Mazao, maduka ya jumla na rejareja, uchimbaji wa madini, kilimo na ufugaji. Idadi ya watu inaongezeka kila siku.

Shughuli za kiserikali

Kuna baadhi ya taasisi mjini hapa zina hadhi sawa na Mikoa au Manispaa. Taasisi hizo ni Mamlaka ya Maji KUWASA, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na TAKUKURU.

Pia Mji wa Kahama umeingizwa katika orodha ya miji inayofadhiliwa na mfuko wa Benki Kuu ya Dunia kujenga miundombinu kwenye Manispaa na Majiji. Chanzo cha habari hii ni Kwizera FM ilipokuwa ikifanya mahojiano na Meya wa mji wa Kahama bwana Abery Shija.

Viwanda

Katika kuunga mkono juhudi za Rais katika sekta ya Viwanda, Kahama inakua katika sekta ya viwanda huku tukishuhudia ujenzi wa viwanda na ufunguzi.

Tumeshuhudia ufunguzi wa kiwanda cha Mabati, Nondo n.k. Pia kiwanda cha kutengeza bidhaa za plastiki na kiwanda cha kukamua Mafuta. Pia kuna ujenzi mwingine unaendelea wa kiwanda cha kutengeneza Mifuko.

Mawasiliano na Uchukuzi

Kahama ni kati ya miji nane Tanzania ambayo ina viwanja vya ndege. Hivyo ukiwa Kahama unaweza safiri kwa basi au ndege.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kahama imekua manispaa naona kuna sehemu umetaja meya, kiuhalisia halmashauri za wilaya na miji zina wenyeviti sio meya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom