Ujirani mwema. . . ?Ama. . . .?

Hamna ubaya wowote mtu kuwa karibu na jiraniye maana ukaribu huo unaweza ukazaa urafiki sawa na undugu ukapata mtu wa kusaidiana nae.
Anyway kuna ambalo mie nimeshindwa kujua nia yake kwahiyo nataka kujua wanajamvi mnalionaje.

Kuna wanandoa wamehamia sehemu mpya hata mwezi haujaisha, wanapoishi ni ndani ya geti ambapo mwenye nyumba anaishi pamoja na mpangaji mwingine (mtu na mkewe, mtoto na dada wa kazi).

Hawa wapangaji wapya hawana dada wa kazi ila mke ni mjamwepesi kwahiyo kushirikiana muhimu. Sasa juzi jioni kaka alikua anamsaidia mkewe kuosha vyombo nje kwenye karo wakati ye anapika, mara yule mke wa jirani yao (mpangaji mwenza) akatoka nje na kumkuta yule kaka akiosha vyombo. Yule dada akamuuliza 'kheee unaosha vyombo'? Kaka akajibu 'ndio' tu alafu akaendelea. Dada akatoa offer. . .'acha nanii (dada wake wa kazi) atakusaidia'.

Sasa mhusika anajiuliza na kuuliza ni kwamba yule jirani aliona mumewe anaonewa kuosha vyombo akamuonea huruma ama? Au jirani anachokonoa tu ya watu akiwa hajui wanaishi vipi?Inahusu kutoa msaada kwa mume wa mtu bila kuombwa ikiwa mkewe yupo? Au ndio mafumbo ya "kwanini unaosha
vyombo na mwanamke unae?"

Mie nimeshindwa kujua kama ndo kujaliana kwa majirani au kuna jingine.

kwa kawaida penati anacheza mpigaji na mlinzi wa goli, acha wao wacheze penaati. wewe subiri matokeo
 
huyo jirani mnafiki....

Maisha ya wanandoa yanawahusu nini?

Kama nia yake ni msaada kwa nini asimfuate mke ampe msaada????

Huo ni uchimvi, unafiki, uchokochoko, na ufukufunyu.......

Kwanza kunatatizo gani mume akiosha vyombo au akimsaidia mkewe kazi??? Akimkuta anapiga deki atamwomba amsaidie? Na akikuta anaduu na mkewe ataomba asaidie?????
 
kweli kabisa ni vizuri kuwa mwangalifu ndoa huvunjwa na watu kama hawa wanao jidai wana huruma!

Duh!! ngoja na mie niwe makini maana husband huwa ananisaidia kazi nyingi za nyumbani, wasije wakampandikiza hizo mbegu za kishetani loh!
 
Kwa watu wanaoishi mitaa ya uswahilini hii siyo ishu sana kwa kuwa kule kwa sehemu kubwa mwanaume haoshi vyombo wala kupika. Kwanza kule ukioa mkeo akikuona unaosha vyombo anakushangaa. Kwa hiyo inawezekana huyo mke wa jirani ni mtu mwenye mtazamo huo na alitoa huo msaada kwa nia njema tu.
 
1. Kuna uwezekano huyo mwanamama jirani hakutambua kuwa Jibaba linalokosha vyombo lipo peke yake kwa muda huo, hivyo kwa heshima akaona bora amtoe bintiye wa kazi kwenda kusaidia.

2. Kuna uwezekano huyo mwanamama jirani kaitambua hali ya jiraniye(mama mjamzito), hivyo haikuwa busara kumwacha Jibaba akoshe mivyombo.

3. "....Yule dada akamuuliza 'kheee unaosha vyombo'? Kaka akajibu 'ndio' tu alafu akaendelea. Dada akatoa offer. . .'acha nanii (dada wake wa kazi) atakusaidia"
Hicho kifungu unaweza kutambua kuwa mwanadada jirani anaamini mwanaume hapaswi kukosha vyombo, yu radhi mjakazi wake asaidie hiyo shughuli...maana tunaona kaanza kwa kushangaa halafu ndio swali likafuata.
 
Mi naona hapo huyo jirani alifanya jambo la busara sana sana. Alikuwa anapeleka msg kwa wote wawili, bw na mke kuwa "Katika mazingira ya kitanzania, baba (sio mwanaume), kuosha vyombo ni kusigina maadili ya kitanzania.
Hakuna cha makubaliano hapo... Hivi wakikubaliana kufanya mapenzi hadharani, wangewaacha tu, eti ni makubaliano?!!!
Mwanaume kuosha vyombo, tena hadharani ni kukiuka maadili ya Kitanzania, na adhabu yake ni kuabishwa kama alivyofanyiwa na huyo jirani...
 
Back
Top Bottom