Ujio wa Rais wa China, Xi Jinping nchini Tanzania - Machi 2013

mimi sioni kama huyo rais wa china anatupenda!jamani,NO PERMANENT FRIEND BT THERE IS PERMANENT INTEREST!....na HAZINA YA MTU ILIPO NDO MOYO WAKE ULIPO!...jamani waTZ its tym now,ifike sehem wananchi wanufaike na rasilimali zao sio kutegemea wahisani wakati tuna kila kitu,hakuna cha bure,na wala hawatupendi nao wanangalia nini watapata kutoka kwenye rasilimali zetu!
Inshort c wawekezaji bali ni wachukuaji!
...tuna sera nzuri,bt hatuna viongozi wa kuimpliment,wala wenye vision!
 
Ziara hii haitakuwa na jambo jipya lolote.Hii ni kwasababu,Tanzania huwa hatujifunzi kitu kipya kutokana na ziara za viongozi wetu nje wala viongozi wa nje hapa kwetu. Tunacheza mchezo wa kidiplomasia tu bila faida yoyote.Huo ndio ukweli.
 
Inaonyesha Wazi Tanzania Ni Nchi Inayopendwa Na Mataifa. Wengi Wanavutiwa Na Asili Mali 2lizo Nazo. Pamoja Na Aman Iliyopo Tanzania. Ujio Wa Rais Wa China Tanzania Ni Fursa Kwa Watanzinia Wote Kujuwa Kwamba China Na Tanzania Ni Marafiki Tangu Enzi Za Mwalim Nyerere. Si Mnakumbuka Sera Ya Ujamaa Tuliipata China. Anakuja Kuudumisha Zaid Urafiki Wetu.
 
Hivi ziara ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping, ni kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au kwa ajili ya Tanganyika?

Inasikitisha kuona ule utaratibu wa Wakuu wa Nchi na Wakuu wa Serikali za kigeni wanapozuru Jamhuri ya Muungano kufika kote Tanganyika na Zanzibar ambao ulikuwepo tokea 1964 hadi miaka ya karibuni ya mwanzoni mwa 2000 sasa unapuuzwa. Zanzibar iliyoweza kumkaribisha Chou En Lai mwaka 1965 zama za Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume leo hii inalazimika kumpeleka Rais wake, Dk. Ali Mohamed Shein, ende Dar es Salaam kumpokea Rais Xi Jinping akiwa ni sehemu tu ya viongozi wengine wengi waliopo Uwanjani. Haya hayakuwa malengo ya Mzee Karume.

Tunaisubiri kwa hamu kura ya maoni tufanye maamuzi ya kurudisha mamlaka kamili ya Zanzibar kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika.
 
Ushirikiano katika UCHUMI, UJENZI, ELMU, na UTAMADUNI uwe hivi;

UCHUMI: Uvunaji wa rasilimali zetu kama watawekeza mtaji kwa kiasi chochote umiliki na faida ya uwekezaji iwe ni 50/50 basis, Watanzani wawe na full access to audit, accounts and management ya biashara husika.

UJENZI: Wajenge viwanda vikubwa vya Chuma kule Kiwira na Liganga (Mtallurgical Industry) kwa ajili ya kusanifu mitambo mbalimbali. Pia tushirikiane katika uanzishaji na uendeshaji wa viwanda vya usindikaji (Processing Industry) wa gesi, madini, pamba, mkonge, korosho n.k.


ELIMU: Makubaliano yafanyike kuruhusu wanafunzi wa elimu ya juu wa Tanzania waende Uchina kujifunza Teknolojia katika masuala ya Uhandisi kwenye fani za jiolojia, kemia, mitambo, maabara na utabibu.


UTAMADUNI: Ili elimu ipatikane kwa ufanisi miongoni mwa wanafunzi wa Kitanzania, pawepo na utaratibu wa maandalizi ya wanafunzi watakaotakiwa kwenda Uchina, kupatiwa fursa ya kufundishwa Kichina mapema kabla ya kwenda huko. Hii itawajengea uwezo wa kujifunza teknolojia zinazokusudiwa kwa wepesi.
 
Ziara hii haitakuwa na jambo jipya lolote.Hii ni kwasababu,Tanzania huwa hatujifunzi kitu kipya kutokana na ziara za viongozi wetu nje wala viongozi wa nje hapa kwetu. Tunacheza mchezo wa kidiplomasia tu bila faida yoyote.Huo ndio ukweli.
Unaweza kuwa sahihi mkuu. Nimejaribu kufuatilia press conference aliyoitisha JK kuzungumzia ujio huu nimesikitika sana. Kwanza anasema alipoelezwa juu ya ugeni huu hakuamini masikio yake. Na akaongeza yuko so exited na ugeni huu. Kwa mtizamo wa haraka wa maneno haya tayari katika negotiation tumejishusha na hatuna hadhi mbele ya Wachina. Ni kama Rais wetu si rais mbele ya Xi Jinping.Real sad. Lakini kingine wakati Congo atakakotembelea pia aliyezungumzia ujio wake ni Waziri wa Habari hapa kwetu JK mwenyewe kashika mikoba mwenyewe. As if press Conference ya Mh. Membe haikutosha. Ni wazi kuona kosa la kistrategia katika ugeni huu. We will always loose kama Rais ambaye anapaswa kuwa final ndiye ataapia mwanzo na katika diplomatic battles.
 
Ni kwanini bidhaa za China hazikidhi viwango vya ubora hasa hapa kwetu Tanzania?. Miradi mingi ya kichina haidumu! Angali uwanja wa taifa ukikalia kiti tu kinang'oka, angalia ukumbi wa bunge unavyovuja sasa. Je, Tanzania kuwa ya kwanza ni kuifanya kuwa dampo la bidhaa feki za Uchina?
 
Enzi za Urafiki Tanzania Nyerere time - China, kulikuwa na faida.

Viwanda na Reli zilijengwa. Viongozi wetu kipindi hicho walikuwa kwa faida ya Taifa.

Ila kwa sasa viongozi wetu ni wabinafsi, wakipewa chao 10% wanaachia malighafi zenye thamani ya matrilion kwa rushwa ndogo tu. VIONGOZI WETU NI WASALITI, WABINAFSI.

Viongozi wetu wamechukua mikopo WB na wakawapa Wachina wajenge barabarani duni kabisa. Barabara zitaharibika kabla hatujalipa mikopo. Sasa hivi wachina wanainyonya Tanzania kwa sababu viongozi wetu wamelisaliti taifa.
 
Hakika iyo ziara ya uyo rais wa China ni muendelezo tu wa kuweka mazingira mazuri ya unyonyaji wa rasilimali zetu. China inaogopeka sana hata nchi za Ulaya kama Ujerumani kwa wizi mkubwa wa Teknolojia. Wote mataifa ya magharibi kwa jina la mabepari na wachina kwa jina la wajamaa ni wezi watupu hawana nia yoyote njema kwetu.

Ole wetu sisi mambumbu kwa maana tumebarikiwa viongozi wabinafsi,wenye uchu wa madaraka na wala rushwa wakubwa ambao wapo tayari kuiweka rehani nchi yao kwa tamaa zao mbaya.

Tujiulize, kama kweli hao wachina na hao wadudu wengine wana nia nzuri na sisi kwanini wasingejenga vyuo na kutuwezesha kupata ujuzi ili tuweze ku-utilize wenyewe resources zetu?
 
shift from western bloc to eastern bloc. Ni kama ule mchezo wa olympic wa kupokezana vijiti. Hakuna jipya...watia sahihi mikataba ya kinyonyaji ni wale wale.
 
Mimi ningekuwa mojawapo ya panelist wa kupanga maeneo ya ushirikiano ningetaka tuwe na long run plan ya transfer of technology through education. yaani wale wanafunzi wenye uwezo, upeo au akili za pekee yaani VIPAJI MALUMU kama inavyojulika. awapelekwe china wakasome then warudi tz kuendeleza kwa vitendo mambo waliyosomea. nadhani kwa hili tutaweza kutransform our ecomomy as per tanzania vision 2025
 
hivi kwa nini kila kiongozi akija hapa kwetu nchini huwa wanasaini tu mikataba! JE, nawewe mweshimiwa ukienda uku huwa unasaini mikataba au kufuja kodi za wananchi?
 
Binafsi ujio wa rais Xi mteule wa China, ni vema ktk kuendeleza mahusiano ya kimaendeleo na kibiashara baina yetu na wao. Hapa sijaona tatizo la kimahusiano na China, bali tatizo lipo kwa viongozi wetu km wawakilishi wetu hasa ktk negotiation mbalimbali.

Nasema hivi kwani wachina wanafanya kazi za viwango na wanateknolojia kubwa sana, hvyo wapo wanakumbana na viongozi wetu wasiotaka uhalisia wa thamani kama taifa ila wanataka kupata percent fulani wao ili kuwapa unafuu wa kisheria.

Sasa km watz tukubali kuwa wachna ni wema na hawataki shortcurt way kwa mambo ya maendeleo na hii itatusaidia kuachana na nchi za magharibi km marekani n.k. Ila tuwasisitize china wawekeze teknolojia hapa kwetu pamoja na kujenga viwanda kutokana na malighafi zilizopo. Hebu watz tuchangamkie fursa hii.
 
Tunapenda ujio huo. Lakini ni lazima aambiwe kuwa Tz si damping place kwa vitu feki hata kama sisi ni maskini.
Pia aambiwe kuwa Tz kunawatu weng wasio na ajira pia wapo wenye elimu wenye uwezo. So wanapokuja kuwekeza wajue Tz kuna skilled & non.skilled labour.
Si lazima watoke china.
Pia sirikali ya china kama vp itusaidie kuanzisha viwanda hapahapa nchini kama wanataka kutusaidia kweli.
 
Nimeshiriki katika negotiation ya itakayopelekea kusainiwa mkataba wa kibiashara mkubwa sana kuwahi kutokea nchi hii katika ujio wa huu wa Rais wa China.

Uzoefu mdogo niliopata kuhusu China ni kuwa China is an emerging window for opportunity, there is a huge untapped market which it can take very little effort to tap it as compared to Europe and America

Matharani, tunaambiwa kuna soko kubwa sana la mahindi nchini china, Kwa sasa huwa wananunua mahindi mengi kutoka US. Soko la US ghali ukilinganisha na Africa (Tanzania), If can assure them kwamba tunakiasi cha kutosha wakulima wa tz watapata soko la uhakika la mahindi yao kwa bei mara dufu!

Wizara ya Kilimo Mpo?????
 
Back
Top Bottom