ze big
JF-Expert Member
- Apr 27, 2015
- 382
- 350
Habari za mda huu wana jamiii. Juzi niliona tangazo kuhusiana na Mall mpya iliyofunguliwa pale kariakoo ambayo ndani yake kuna maduka zaidi ya mia moja yanayohusika na uuzaji wa simu Original pamoja na maduka ya watoa huduma kama Vodacom na Halotel. Kiukweli nilipata fursa yakuzunguka kwenye vaadhi ya maduka takriban maduka 36 nilivutiwa sana na huduma na bei za simu kwasababu ukilinganisha a simu tunazouziwa kule kariakoo kwenye maduka ya wahidi kwa bei za kulaliana sana huku mambo si mabaya bei ni reasonable na unapata simu mpya kabisa.
Nilichunguza zaidi kutaka kujua kwanni wao wanauza bei yenye nafuu nikamegewa siri kuwa kwa sasa like jengo ukienda kwaajili yakupangisha unapewa mwezi mmoja wakufanya biashara pasilo kulipa kodi ndipo utakapoanza kulipa kodi ya pango. Japo sikuweza kujua gharama za upangishaji ila ningewashauri kama mtapata walau muda kidogo mkatembelee pale mjionee wenyewe na pia ukiuziwa simu wanathibitisha kabisa kwa TCRA kutumia IMEI namba yako pale pale. Ni muda wa mabadiliko kwenye nyanja ya mawasiliano.