Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,507
Chama chochote cha siasa chenye mtandao wa kitaasisi kina safu ya wanachama ambao waingereza wanawaita big gun. Hawa ni wanachama ambao ukiwaona kwenye kikao au mkutano wa hadhara, lazima uelewe kuna umuhimu wa juu sana katika chama hicho kwa wao kuwepo hapo. Wanachama ambao ni big gun mara nyingi huwa ni viongozi wakuu wa vyama.
Katiba ya CHADEMA katika Ibara ya 7.7.3 inasema Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao: (a) Mwenyekiti wa taifa, (b) Makamu Mwenyekiti Bara, (c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar, (d) Katibu Mkuu, (e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, (f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Nilishangaa sana kuona safu nzima ya Viongozi Wakuu wa CHADEMA na pia Kurugenzi za Utendaji Makao Makuu ya Chama ikihamia Mwanza ili kujaribu kupambana na hoja za Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli ambaye alipita Jijini Mwanza na kusalimia wananchi akiwa njiani kuelekea Jimboni kwake Chato ili kuwashukuru wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla katika safari zake za kisiasa.
Baadhi ya Viongozi Wakuu walitumia muda mwingi kumwongelea John Magufuli na wale wengine hawakuweza kujizuia kulitaja jina la John Magufuli katika hotuba zao. Kwa ujumla ninaweza kusema mkutano ulikuwa maalum ili kukabiliana na ujio wa John Magufuli katika Kanda ya Ziwa kama mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
Kwa mwananchi anayeangalia siasa kwa mapana na marefu anapoona chama kikuu cha upinzani kinakusanya Viongozi Wake Wakuu wote na kuwapeleka kwenye jukwaa moja ili kujibu kwa kiwango kikubwa mapigo ya hoja ya kiongozi mmoja wa CCM, lazima atajiuliza maswali kama kweli hiki chama kina nguvu na uwezo wa kukabiliana na CCM.
Kwa sasa viongozi wa CHADEMA wako tayari hata kula matapishi yao ili kupata nguvu ya kisiasa kupambana na ujio wa John Magufuli kama mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
Mwandishi mmoja wa gazeti la RaiaMwema aitwaye Lula wa Ndali Mwananzela katika makala yake iitwayo ''Wananchi waanze kutambua CCM imeshindwa'' alishawahi kusema,
CHADEMA iliwekeza sana katika kanda ya ziwa ambayo kwa sasa CCM iko mbioni kutumia turufu ya John Magufuli ili kupambana na CHADEMA katika kanda hiyo.
Kwa sasa CHADEMA kinaingia katika uchaguzi kikiwa katika defence mode, ndiyo maana kwa sasa wanajaribu kufuta nyao za Magufuli kila anakopita.
CHADEMA is throwing "both of their kitchen sinks" at trying to get rid of Magufuli exemplary work records.

Lula wa Ndali Mwananzela aliendelea kusema,CHADEMA wana kazi kubwa zaidi sasa kuweza kuiondoa CCM madarakani kuliko ilivyokuwa mwaka 2010. Mwaka 2010 CHADEMA ingeweza kuiondoa CCM kama vile kumsukuma mlevi njiani; sasa hata hivyo, ni kama kujaribu kumpiga ngwala beki mzuri ambaye ameweka miguu yake imara. Haanguki zaidi ya kusukumwa sana.
Niliwahi kusema, Ujio wa Magufuli unaifanya CCM isiwe katika kile kinaitwa defence mode badala yake itaingia katika kampeni ikiwa katika offensive mode. Ujio wa Magufuli umekuwa ni mshangao/butwaa ndani ya CHADEMA kwa sababu hoja za uwajibikaji na ufisadi kuhusu mgombea wa CCM hazitauzika sana katika Uchaguzi Mkuu.Kwa mtu yeyote anayefikiria kuwa itakuwa rahisi kuiondoa CCM madarakani hajajifunza katika historia. CCM haitoondolewa kwa kuombea, kwa kunuia, au kwa kutamania bali kwa mikakati sawia ya kisayansi (si ya kishirikina). Na dalili ambazo zinaonekana sasa ni kuwa bado CHADEMA haijajipanga na haionekani kujipanga kuiondoa CCM madarakani. CHADEMA isipoangalia (na hili nimelisema mara kadhaa nyuma) inaweza kujikuta inajisifia kupendwa na kukubalika na watu wengi.