Ujio wa Google Site Kit ndani ya Wordpress community

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,248
34,197
Kawaida ukiwa na Website baada ya kutengeneza lazima uunge Website yako kwenye searches kama Google, Bing n.k.

Pia ilikuwa lazima ujiunge na huduma kama Google Analytics, Google Console, Site Page Speed Insight lakini kwa sasa huna haja ya kujiunga na huma moja moja ukiwa na Google Site Kit.

Hii imejaribu kuunga huduma zote za Google kuanzia Google Analytics mpaka Google Console in one plugin. Ukiwa na hii plugin huna haja ya kupitia process ngumu ya kusajili huduma hizo.

Ukiwa na hii plugin kila huduma unaipatia kwenye dashboard ya website yako huna haja tena ya kwenda kwenye website za huduma hizo ujisajili.

Kitu kingine, huna haja ya ku intall plugins kama "Monster Insite" iliyokuwa inatumika kuunga Google Analytics kwenye website yako. Kwa sasa hii plugin na nyingine kama hizi zitabidi zitafute shughuli nyingine ya kufanya.

Baada ya Google Site kutolewa mwaka huu around July, updates zinaendelea kutolewa kuhakikisha inakuwa more stable.

Nini maoni yako kwenye hii plugin ya Google?
 
Itarahisisha kazi hasa kwa sisi developers ambao tulihitaji kuunga tools nyingi wakati wa kuset-up websites
 
Back
Top Bottom