Mwandishi wa Habari Samson Chacha , ametishiwa Maisha na wafuasi wa Chama Cha Demkorasia na Maendeleo Chadema Wilayani Tarime , kwa kile walichodai kuwa asingepaswa kutangaza kuhusu Kushambuliwa kwa Mawe kwa Mbunge wao Godbles Lema kutoka Arusha katika mji mdogo wa Sirari wakati akiwashawishi Vijana wa Mji huo kuungana na Chadema kwenda kufanya Vurugu Nyamongo na Tarime,
Tukio hilo la kutishiwa Maisha na Wafuasi hao wa Chadema waliokuwa wakiongozwa na Chacha Heche Suguta ,akiongozana na kundi la vijana zaidi 10 wakiwa na Sare za Chadema akiwemo Diwani wa Viti Maalumu kata ya Sirari kupitia chama hicho cha Chadema Veronika Sando, Amos Mondawela,Keraryo Mwita, wakiwa na Mutangazaji wa Chanel Ten Mkoani Mara Mabere Makubi ambaye amekuwa akiongozana na kundi hilo linalopita katika miji ya Watu na kuwashawishi Uchochezi wa kwenda Nyamongo kuvamia Mgodi Wakitumia Kivuli cha Watu 5 kuuawa na Polisi wakati wa kuvamia Mgodi wa North Mara Barrick hapo Mei 16 mwaka huu,
Akisimulia tukio hilo kwa vyombo vya habari , Mwandishi huyo bw, Samson ,alisema kuwa "Nakumbuka mnamo Mei 22 mawaka huu saa 12 Jioni nikiwa maeneo ya Nyumbani huko Sirari, tukiwa tunakunywa Soda na wengine wakila Chakula katika Hotel ya Robart Ndugu , Walifika Wafuasi wa Chadema wakiwa wamevalia Sare zao wakiongozwa na Chacha Heche na wenzake , walitukuta nje ya Hotel katika Veranda na kutuzunguka Meza yetu ambapo Chacha Heche alianza kuniuliza kuwa kwa nini nimemwandika Mbunge wao Godbles Lema kuwa alirushiwa Mawe hapo Sirari ",
Mwandishi huyo bw, Samson Alisema kuwa "Mwandishi wa habari wa Chanel Ten Mabere Makubi naye alianza kuuliza kuwa "Nasikia kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime alishiriki kumrushia mawe Mbunge Lema ?, nilimjibu kuwa mambo ya Mwenyekiti Kamuulize Mwenyewe akupe uhakika , na jaribu kufata maadili ya uandishi wa habari usitumiwe na kikundi cha watu kushawishi na kuchochea vurugu , Sheria zipo kwa nini uungane na wafuasi wa Chadema kupitapita katika miji ya watu kuwashawishi kwenda kuvamia Magodi ?, hapo ndipo kundi hilo la Wafuasi hao wakiongozwa na Chacha Heche walianza kutoa lugha ya Matusi kwangu na kunitishia maisha , hali iliyosababisha Uvunjivu wa amani katika maeneo hayo ya Hoteli hiyo ,"
Katika Meza hiyo Mwandishi Samson Chacha alikuwa amekaa na Mwanasheria ambaye pia ni Afisa Ardhi wilaya ya Tarime bw, Sebastian Mangenyi, Afisa Usalama wa taifa wilaya ya Tarime bw, Nyambita , na Wakazi wengine 4 wa mji wa Sirari , ambao waliwaonya Wafuasi hao wa Chadema na Mtangazaji wa Chanel Ten Mabere kwa vitendo vyao vya kuchochea watu kutaka kufanya vurugu na kuvamia katika maeneo ya Mgodi , ambapo kundi hilo na Mwandishi huyo lilondoka huku likitishia kupambana na Mwandishi Samson ,lakini watu waliokuwepo walisema kuwa Habari ambazo zimeandikwa na Mwandishi Samson ni za sahihi sasa wao wanataka Waandishi wa kununuliwa kama Mabere Makubi kitendo ambacho kinakiuka maadili ya Uandishi wa Habari, kwani hata Mbunge Nyambari Nyangweni CCM na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tarime waliporushiwa Mawe na kuharibiwa magari Samson aliitangaza iweje ya Lema isitangazwe waliuliza wananchi wa Sirari,
Mwandishi Samson Chacha alikwenda kituo cha Polisi Sirari na kufungua Jarada la kutishiwa Maisha namba SIR/IR /743 /2011, ambapo Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Uchunguzi unaendelea , alisema Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Costantine Massawe .