Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,085
Nchi hii haitakuja kupata maendeleo kwa sababu wananchi tumekuwa wajinga. Na viongozi kwa sababu wanajua wanatawala Taifa la wajinga, hawana wasiwasi kabisa wala woga kwa sababu wanajua udhaifu wa watu wanaowatawala.
Pesa zinaibiwa, sisi cha kwanza tunaangalia ni nani anayetuhumiwa kuiba, nani aliyefichua huo wizi, nani aliyelalamika, au nani anayetuhumiwa kuiba, ni wa kundi gani na wa chama gani, kama vile kodi inapokusanywa kodi inaangaliwa wewe ni wa mlengo gani, na ni wa chama gani, na ni shabiki wa nani, na hivyo ulipe au usilipe kodi.
Viongozi wa upinzani na baadhi ya wananchi wa kawaida, mara kadhaa wamelalamikia matumizi mabaya na ya anasa ya Serikali, kama vile kununua magari ya kifahari, kuwa na ofisi za Serikali ambazo zingeweza kufutwa na mambo yakaenda bila matatizo, lakin kwa sababu labda hoja imetolewa na viongozi wa upinzani au kundi hasimu ndani ya CCM, basi wapenzi na mashabiki wa CCM au kundi jingine hawaangalii uzito wa hoja, wao ni kupinga tu kwa sababu watu wao wapo ndani ya Serikali, kama vile hayo matumizi ya anasa yanafanywa kuwakomoa wapinzani na yatawaathiri wapinzani pekee.
Pesa imeibiwa na kuporwa na utawala wa marehemu Magufuli, lakini kwa sababu ametajwa Marehemu Magufuli, kwa ujinga tu, mashabiki wa marehemu kwa sababu tuhuma zimetolewa na utawala wa Samia, wanasema ni uwongo. Yaani watu wameamua kupigania kulinda wizi na uporaji kwa sababu ulifanywa na wanayempenda.
Leo kuna tuhuma za upoteve au wizi dhidi ya Serikali ya Samia kuhusiana na pesa za mikopo, kwa sababu inaguswa Serikali ya kiongozi tunayempenda, basi weledi wa kujadili ili kuupata ukweli unakuwa hamna. Kitakachofanyika ni kupigania kuitetea Serikali na Waziri wa fedha.
Wakati wa utawala wa Mkapa, yeye mwenyewe marehemu kwenye kitabu chake amekiri kuwa CCM iliiba pesa ya umma dola milioni 100, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 230, kwa sababu hoja imeibuliwa na Lisu, na tuhuma ni dhidi ya CCM, basi wanaCCM, na maadui wa Lisu na CHADEMA, wataungana kutetea ule wizi kwa sababu ulifanywa na chama chetu au chama tunachokipenda.
Kwa upumb.avu wetu huu wa sisi wananchi; viongozi na watendaji wa Serikali wataendelea kuchezea pesa zetu kama wanavyotaka maana kila anayefanya hivyo ana walinzi na watetezi. Hatima ya Tanzania daima imekuwa mashakani kutokana na kuwa na jamii ya watu wanafiki, waongo, walaghai na wasio na misimamo, wasiojielewa wanapigania na kutaka nini.
Mbaya zaidi hizi tabia mbaya unafiki, uwongo, ulaghai na kukosa misimamo, tunawarithisha na wazaliwa wetu. Mtu yupo UVCCM, bado hajawa kiongozi wala kupevuka sawasawa akili, anaanza kufundishwa namna ya kuwa mnafiki, mlaghai, mwongo na mtetezi wa uovu alimradi uovu huo umefanywa na mwenzetu ndani ya chama au ndani ya Serikali ya chama chetu.
Hatuwarithishi watu wetu matendo mema kama ujasiri, ukweli, uaminifu, kuchukia rushwa, kuchukia uobevu, kupigania haki na kuwa watu wenye maadili mema. Chipukizi wanafundishwa kuabudu na kusifia watawala, na siyo kuhoji.
Laiti kama tungekuwa na Taifa ambalo, MWIZI huwa ni mwizi bila ya kujali ni wa chama gani, kundi gani, au mwelekeo gani, hakika watawala wangeogopa na kuiheshimu hela ya umma maana wangejua kuwa wananchi wote ni adui wa wizi, tukifanya wizi au kutapanya pesa ya umma tunakuwa maadui wa Taifa zima.
Kama kuvunja katiba, au kugandamiza haki za watu au kugandamiza demokrasia na haki za watu, kwa sisi wananchi wote tungeyaona matendo hayo ni uovu dhidi yetu na jamhuri yetu, bila ya kujali anayefanya au kufanyiwa uovu huo ni wa chama gani, kundi gani au mwelekeo gani; hakika watawala na vyombo vya dola, wote wangeogopa kutenda uovu maana wangejua katika uovu wao hawana wa kuwatetea, na hawana rafiki katika huo uovu.
Lakini ujuha wa wananchi ndio unaofanya watawala na vyombo vya dola wasione shida kukanyaga haki za watu maana wanajua wakikanyaga haki za kundi fulani, kuna kundi litafurahia sana. Akishambuliwa au kutekwa au kuuawa mtu wa mlengo fulani, anajua atapongezwa na pengine kupandishwa hata cheo na kundi jingine.
Na hayo tuliyaona wakati wa awamu ya 4 kuhusiana na kifo cha Mwangosi, kamanda wa polisi alipandishwa cheo na kupelekwa makao makuu ya polisi kama vile akahakikishe nchi nzima inafanyiwa uovu ule, tumeyaona mengi zaidi wakati wa awamu ya 5, kwa polisi na mahakimu waliopandishwa vyeo kwa sababu waliwatesa na kuwakomoa wapinzani.
Tunaoongozwa, ndio tunaotakiwa kui=shape Serikali. Hata huko tunakoona kuna utawala mzuri, siyo kwamba watawala wanazaliwa ni watu wema sana, hapana, bali wananchi hawakubali kutendewa yasiyo sahihi na viongozi wao.