Ujinga unaoendelea kwenye mtandao wa twitter.

Ujinga unaoendelea kwenye mtandao wa twitter.

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
5,082
Reaction score
20,806
Mimi ni muumini na mtumiaji wa mitandao mingi ya kijamii(sio muandikaji sana), moja wapo wa mtandao wa twitter.

Ule ujinga ulio facebook umehamia twitter sasa, ule ujinga wa kulike na kukoment mara nyingi kwenye tweet ya mwanamke. Kule siku hizi binti akiandika tu kua anahisi mkojo umembana, basi hata kama ana followers 200, atakula like 800, retweet 280, comments zisizo na idadi.

Mbaya zaidi kule kuna makundi, wao wanajitag tu, kama hauko kwenye circle yao hata ukitweet jambo la maana namna gani utaishia kuisoma mwenyewe. Kuna makundi kama ya kina Maria Sarungi na timu yake, wao ni wao tu, kama hawakujui hata ukiwatag utaishia kula bloku ya maana.

Kuna makundi ukiwa mtazamo tofauti tu unaishia kublokiwa fasta, kule watu wanapenda kulikiwa tu, ukiwachallenge unaishia bloku tu, sio wanasiasa wala watu wa kawaida.

Pamona na kwamba nina account kule na sijawahi kutwet wala kulike wala kuretweet wala coment kwa miaka yote 7 ambayo niko twitter ila hali ya sasa inasikitisha. Twitter umbea unapigwa kama instagram.

Awali nilidhani ni hawa div 5 wamevamia mitandao, ila sasa hata watu waliosoma enzi za mwalimu ujinga ni ule ule.

Acheni tu magu aendelee kutunyoosha.
 
Cha muhimu tenda matendo mema uende Mbinguni. As long as upo duniani utaendelea kukutana na yasiyofurahisha.
 
Jf tu ndio iliyosalia kwenye simu yangu kama social network

Nakumbuka mwaka jana rafiki yangu alininunia hadi kitaa et sijapost picha yake kweye siku yake ya kuzaliwa
 
Back
Top Bottom