Taifa Letu Tanzania!!
Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana hela.
Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma sana
Taifa ambalo bank haikutafuti wewe ndio unaihonga ili ikukopeshe fedha.
Taifa ambalo ukifeli mtihani wa unapewa kazi ya kufundisha wengine.
... Taifa ambalo kila mtu anataka ajue bei ya kitu ulichonunua!
Taifa ambalo usipoiba mali ya umma unaonekana unaonekana wewe ni mshamba
Taifa ambalo kila mtu analalamika hakuna kazi, mpe kazi sasa, anaanza kulalamika kazi ngumu
Taifa ambalo ukisema upo ofisini saa tatu usiku wanakushangaa ila ukisema upo club saa nane usiku wanakusifia.
Taifa ambalo kusema jana nilikula bata saaaaana unaonekana mjanja
Taifa ambalo kila anayehojiwa anasema "Naiomba Serikali iliangalie suala hili"
Taifa ambalo mvua ikinyesha dakika 10 tu foleni ya magari ni masaa manne
Taifa ambalo hata bomu likilipuka anajichagulia jina la Mlipuaji
Taifa ambalo hata Rais naye analalamika
Taifa ambalo, viongozi wake wameruhusu akili ndogo itawale akili kubwa..
Taifa ambalo walipa kodi ni wafanya kazi tu na si wafanyabiashara
wala wawekezaji
Taifa ambalo limeweka rushwa mbele kwenye kutafuta kazi na chaguzi.
Taifa ambalo viongozi wake wanaamini kuwa magari yakiwa mengi ni maendeleo
Taifa ambalo linaamini watoto wa kike wakipata ujauzito ni vihele hele vyao
Taifa ambalo wanafunzi wasio jua kusoma na kuandika hufaulu
mitihani ya kidato cha kwanza
Taifa ambalo watu wakiandamana polisi wanatakiwa kuwapiga risasi na mabomu ila wala rushwa ni jukumu letu sote
Taifa ambalo liko mbele kusuluhisha migogoro ya jirani zake lakini migogoro yake ya ndani ni ua ua tu.
Taifa ambalo lina viongozi wasiopenda kuambiwa ukweli
Taifa ambalo kuteswa ni kunyofolewa Meno na Kucha
Hili ndio Taifa la .........
Mengine malizia mwenyewe...!
Source: Mdau wa Mbezi Beach