Ujinga na maajabu ya watanzania!!

Ujinga na maajabu ya watanzania!!

VUVUZELA

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2010
Posts
3,103
Reaction score
800
Taifa Letu Tanzania!!
Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana hela.
Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma sana
Taifa ambalo bank haikutafuti wewe ndio unaihonga ili ikukopeshe fedha.
Taifa ambalo ukifeli mtihani wa unapewa kazi ya kufundisha wengine.
... Taifa ambalo kila mtu anataka ajue bei ya kitu ulichonunua!
Taifa ambalo usipoiba mali ya umma unaonekana unaonekana wewe ni mshamba
Taifa ambalo kila mtu analalamika hakuna kazi, mpe kazi sasa, anaanza kulalamika kazi ngumu
Taifa ambalo ukisema upo ofisini saa tatu usiku wanakushangaa ila ukisema upo club saa nane usiku wanakusifia.
Taifa ambalo kusema jana nilikula bata saaaaana unaonekana mjanja
Taifa ambalo kila anayehojiwa anasema "Naiomba Serikali iliangalie suala hili"
Taifa ambalo mvua ikinyesha dakika 10 tu foleni ya magari ni masaa manne
Taifa ambalo hata bomu likilipuka anajichagulia jina la Mlipuaji
Taifa ambalo hata Rais naye analalamika
Taifa ambalo, viongozi wake wameruhusu akili ndogo itawale akili kubwa..
Taifa ambalo walipa kodi ni wafanya kazi tu na si wafanyabiashara
wala wawekezaji
Taifa ambalo limeweka rushwa mbele kwenye kutafuta kazi na chaguzi.
Taifa ambalo viongozi wake wanaamini kuwa magari yakiwa mengi ni maendeleo
Taifa ambalo linaamini watoto wa kike wakipata ujauzito ni vihele hele vyao
Taifa ambalo wanafunzi wasio jua kusoma na kuandika hufaulu
mitihani ya kidato cha kwanza
Taifa ambalo watu wakiandamana polisi wanatakiwa kuwapiga risasi na mabomu ila wala rushwa ni jukumu letu sote
Taifa ambalo liko mbele kusuluhisha migogoro ya jirani zake lakini migogoro yake ya ndani ni ua ua tu.
Taifa ambalo lina viongozi wasiopenda kuambiwa ukweli
Taifa ambalo kuteswa ni kunyofolewa Meno na Kucha
Hili ndio Taifa la .........
Mengine malizia mwenyewe...!

Source: Mdau wa Mbezi Beach
 
taifa ambalo ukitongoza demu una do bila condoms
 
Hayo mambo ni ya kweli kiongozi, Je tufanye nn ili tuondokane na hayo majanga?
 
taifa ambalo yule muuaji kagame anamtukana amir jeshi mkuu halafu hatoi kauli ya kutia moyo
 
Taifa ambalo halijawahi kuwa na waziri mkuu "mkulima" kama pinda.
Taifa ambalo linajisifia kupitia chama tawala kuwa limeleta maendeleo wakati ni wajibu wao kitu ambacho siyo kazi yao kujisifia ni kazi ya wananchi.
Taifa ambalo chama tawala limeasisi ugaidi na udini.
 
Taifa ambalo watu wanafikiri kazini ni mahali pa kupata pesa tu bila kufanya kazi
Taifa ambalo ukiwa na elimu nzuri hupati kazi
Taifa ambalo polisi wanahamasika kwenda kazini ili kula rushwa
 
Taifa ambalo wafanyakazi serikalini hata afanye kosa gani hawezi kufukuzwa kazi! kuiba ruksa, toroka miezi 10 mshahara uko palepale, fanyakazi chini ya asilimia 5, mshahara uko palepale na promotion juu!
 
Taifa ambalo linaunda tume tukio lolote likitokea na hamna feedback inatolewa(wanazuga)

Taifa ambalo migodi ya madini inapewa misamaha na mwananchi wa kawaida wanakula nae sahani moja!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Taifa ambalo wanafunzi wakifeli wanaongezewa alama za ufaulu

"To know the enemy is half the victory"
 
Taifa ambalo viongozi hujiona Miungu watu,
Taifala wasahaulifu(Richmond leo Symbions, watu kimyaaaa...
Taifa ambalo matukio ya ajabu ajabu huibuliwa na kuwapoteza watu attention hata katika masuala ya msingi.
Taifa ambalo mtu anaweza kubuni kituko hata cha kugharimu maisha ya watu na serikali ikaangalia tu rejea Babu wa Loliondo na kikombe chake.
 
Taifa ambalo kiwanda kidogo cha pombe ya kienyeji-Chibuku kinalipa tax nyingi kule TRA kuliko mgodi mkubwa wa dhahabu ama telecom giants kama Airtel or Vodacom!!

Taifa ambalo wananchi wanaambiwa wamsaidie raisi kazi!
Taifaifa ambalo raisi hajui kwanini nchi yake ni maskini!
...Ambalo raisi hajui na anaogopa maswali ya waandishi!

Taifa ambalo fisadi mkubwa anautafuta uraisi kwa nguvu hadi misikitini na makanisani anahonga mipesa!
 
Back
Top Bottom