Ujinga huu unaoitwa Limbwata! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujinga huu unaoitwa Limbwata!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 18, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wanasayansi hivi sasa wanakiri kwamba, huwa inatokea mpenzi akamshika mpenzi wake kwenye akili, yaani akili yako inaweza kushikwa na mpenzi wako na ukasumbuka sana. Kwenye lugha za mitaani hali hiyo inaitwa kushikwa au wengine huita Limbwata.

  Kwenye kitabu kiitwacho, Why we Love: The nature and Chemistry of Romantic Love, mtafiti Helen Fisher anasema, kuna usugu ambao hujengwa kwenye akili ya mpenzi, sawa na usugu unaojengwa na sigara kwenye akili ya mvutaji kiasi kwamba, ni vigumu sana kukubali kuachwa au kuachana naye, hata kama anakutesa na kukuuwa.Eneo la ubongo ambalo linakuwa na mabadiliko pale mtu anapomwona na kumfikiria mpenzi wake, ni eneo hilo hilo linalokuwa na mabadiliko wakati mtu anapotumia madawa ya kulevywa.

  Hii ina maana kwamba, kama inavyotokea mtu akashindwa kutoka kwenye ulevi hadi anakuwa sugu, ndivyo inavyotokea kwa baadhi ya watu wanapopenda.
  Hivi sasa tafiti zinathibitisha kwamba, mtu anapoingia kwenye hali ya kupenda kusiko na kizuizi, yaani kushikwa, sehemu inayohusika kwenye ubongo huonesha dalili zote ambazo hujionesha mtu anapobwia dawa ya kulevywa aina ya Cocaine, kama vile kukosa usingizi, kushindwa kujua hata muda au kutojali kuhusu muda na kuweka nguvu kwenye penzi, kiasi cha kutojali maumivu yake au ya wengine wanaomzunguka.

  Inaelezwa kwamba, mtu anapoathiriwa kwenye eneo hilo la ubongo na mapenzi, anakuwa hawezi kupambanua mambo, kwani eneo la mantiki ubongoni linakuwa limezuiwa kufanya kazi. Ndio maana mtu anaposhikwa kwenye mapenzi anaonekana wazi hatumii akili, kwani hushindwa kuona ukweli hata ule mdogo kabisa.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo hakuna dawa wala uchawi ila ni wewe mwenyewe kwa nini sasa kuna waganga wanasema kuwa anadawa ya mapenzi?..
   
 3. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Very likely! Unakuwa kama msukule mbele ya mpenzi anayekutesa. Kwa hiyo strategy ya kutoka itakuwa ni kama ile ile ya kuachana na madawa ya kulevya, Bangi au ulevi wa kupindukia wa pombe. Yaani unapunguza pole pole. Sasa kwenye mapenzi naona hii ni ngumu sana, unapunguza pole pole kitu gani? Kuonana na huyo mpenzi, kushirikiana naye kimapenzi, kuwasiliana naye? This is tricky!

  Akiwa ni mke/mme you are in more trouble kwa sababu you see each other every now and then! But I guess you may start by living in different rooms! Then differrent houses. Problem is usually the resources! Kwa wale wenye mshiko wa kutosha, it is not a very big issue. Mpenzi akisumbua una-sepa. Kama ni Mke/Mme, unahamia nyumba ya Tabata; unamwacha aendelee kukaa Kinondoni and the story ends there!

  Yeah, it is really very difficult. But it is not impossible if you are determined!
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Alaaa! Kuumbe! sikamatiki tena!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,088
  Trophy Points: 280
  misukule ya mapenzi kumbe tuko wengi, mi nlidhani niko peke yangu
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndiyo hapo utie akili sasa.................
   
 7. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JD alipoimba teja wa mapenzi sina uhakika kama alilijua hili, but she got it right! Kuna uteja wa mapenzi na unakuwa teja haswaa!! Yaani kama ni mke anaweza kuwa anachukuliwa nawe unajua kuwa anachukuliwa lakini umo tu, sana sana utapambana naye halafu unamuomba msamaha akikununia. Ohhh gosh, this is real man!!

  Knowing this helps alot!
   
 8. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mkuu kiukweli nakubaliana na wewe kuwa wakati mwingine haya tunayoyaita 'malimbwata' ni suala la 'love addiction'...
  Tatizo linakuja hasa mule nilipobold..mfano unaposema 'mtu kumshika' mpenzi..ofcoz hapa ndipo pale watu huwa tunachanganyikiwa..manake hilo neno liko 'too general'..kumshika kivipi???..kwa maoni yangu lazima kuwe na kitu katika mapenzi ambacho mmojawapo katika wanandoa anajua kabisa mwezangu is 'fond' wa hii kitu sasa hapo ndipo 'unapozidishiwa dozi'..
  Na pia Usugu unaousema sijauelewa unakujaje hasa kama tutayatazama mapenzi au maisha ya ndoa 'in practice' zaidi kuliko nadharia...to me there should be something from kwa mwenzako in imperical wise ambayo itlaeta huo usugu..je ni nini??..Limbwata???..au something else?..
  Lastly unasema mtu anapoingia kwenye mapenzi pasi na kushikwa/kizuizi..Hivi kumpenda mwenzio bila mipaka ni suala la 'hiari' au 'there is an 'invisible hand'??...na kwa nini hii 'love addiction' sio suala la kudumu??..manake ni rahisi kuwaona watu waliopendana sana kuchukiana ndani ya kipindi kifupi..na watu kushangaa..je? hii inakuwaje manake mateja huwa hawatoki mapema kwenye uteja wao..why not kwenye mapenzi??..do we need rehab?????....nakubaliana na hawa wanasayansi kwa kiasi kidogo, however on the other side naamini limbwata lipo..though sio lazima liwe katika dhana ya 'ushirikina'....
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  wanasema kua uyaone; this is JF bana!
   
 10. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  thenx mtambuzi!!!
   
 11. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hao waliopendana wakachukiana hakuna anayesema kuna aliyelishwa limbwata hapo!! Limbwata huwa linasemwa hasa pale mmojawapo wa wapenzi, mara nyingi mpenzi wa kiume, anapoonekana kunyanyaswa ila haonekani kujali. Yaani, mwanamke anaweza kuwa mapenzi yake kwa mme yameshaisha, haonekani tena kumjali mme wake. Pengine ana wanaume wengine na mme ameshaona! Jamii inatarajia mme huyu ajitoe kwenye mapenzi yale, ila wanashangaa bado yupo tu na hatoki. Hapo ndo jamii husema, huyu kalishwa LIMBWATA. Sasa inaonekana huyu ndo kawa teja, mwenzie mapenzi yameisha, ila yeye ndo hivyo tena!
   
 12. F

  Ford89 Senior Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  daah,kosa lake yeye,msamaha unaomba wewe! Inauma sana.
   
 13. F

  Ford89 Senior Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jaman haya yametukuta,inafikia hatu mpenz wako anakuudhi alafu wewe unajifanya hajakuudhi,unakuwa unaogopa kuonyesha hasira zako....daaah baadh ya wanaume tunakuaga wajinga...
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kushikwa ni tofauti kidogo na mapenzi haya ninayoyafahamu mimi, hebu pitia hizi thread nilizowahi kuziweka hapa, nadhani utapata tafsiri ya kile nilichomaanisha:

  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/180851-wanawake-hukubali-kufa-huku-wakiona.html
  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/173465-ndoa-yako-mwenyewe-ikupeleke-kaburini.html
  https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/167749-nikiwaita-wanawake-wenye-tabia-hizi-kuwa-ni-vichaa-nitakuwa-nimekosea-kweli.html
   
 15. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni maamuzi kama vile uavyohangaika kuingiiza kipato cha siku.
   
Loading...