Ujinga au upumbavu wa watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujinga au upumbavu wa watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Jul 31, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Migomo inayotokea sasa ni kutokana na watanzania wenyewe kutojitambua. Wakati wa mgomo wa madaktari baadhi ya watu walikuwa wanawalaumu madaktari baadala ya kuilaumu serikali.

  sasa walimu wamegoma watanzania waliowengi hawaoni kama mgomo huu unawahusu. Wanatakiwa kuandamana na kuishinikiza serikali iwasikilize walimu. serikali haiwajali walimu kwa vile tu watoto wao hawasomi shule hizi. Hivyo basi wanaweza kuwanyanyasa waalimu kwa vitisho kwani mgomo hauhusu!

  Walimu wamesemwa ooh wao ni waoga kuliko madaktari hawagomi, leo hii walimu wamegoma nchi nzima. wakati madaktari waligoma mikoani tu.

  Ombi langu wazazi na jamii nzima tuungeni mkono.

  Utashangaa wakimsikia Kikwete akihutubia kuwa walimu wakitaka waache kazi utasikia watu wanaandamana kuunga mkono upuuzi huu.

  Hata kama tutalazimishwa kazini basi hatutafundisha hata tukiingia darasani hatutafundisha tuone nani atakayeumia.
   
Loading...