Kikwete alipotosha umma wa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete alipotosha umma wa Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Mar 13, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kikwete akiongea na wazee wa DSM aliwalaumu wanaharakati kuunga mkono mgomo wa madaktari!

  Huu ulikuwa upotoshaji mkubwa kwa kuwa wanaharakati wakiongozwa na Ananelia Nkya waliandamana kuishinikiza serikali kuingilia kati mgomo wa madaktari ili kuokoa wagonjwawaliokuwa wanateseka kutokana na kadhia hiyo. Wanaharakati katika mgomo wa awamu ya kwanza waliishangaa sana serikali kwa kutowasikiliza madaktari na madai yao! Rais wa nchi kwa upande wake aliamua kwenda Davos na Addis Ababa kushughulikia mambo ambayo hayakuwa kipaumbele cha Watanzania.

  Aliporudi kutoka Addis Ababa aliamua kwenda kula kuku na wawekezaji wa benki moja ya kigeni!

  Rais hakuwatendea haki Watanzania kwa kutowajali. Baada ya maji kumfika shingoni anawalaumu wanaharakati ambao kiukweli walikuwa wanamhimiza kuchukua hatua za kuokoa wagonjwa.

  Kweli wahenga walisema " Mbaazi ulikosa maua husingizia jua!" hawakukosea.
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ukifuatilia ya Jakaya Utalala Mlango wazi ngoja apite na kitabu chake tukifunge
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Alitaka waandamane kama wale walio-valishwa T-shirt na Kapelo za njano na kijani kulaani harakati za madaktari!
   
 4. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kama JK angeingilia mapema mgomo wa kwanza wanaharakati wasingeandamana. Lakini kwa kuwa serikali iliwapuuza madaktari kulikuwa hakuna namna isipokuwa kuikumbusha wajibu wake kwa wananchi na kuokoa maisha ya wagonjwa.
   
 5. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani JK hajui majukumu yake ndiyo maana nusu ya maisha yake ya Ikulu anashinda nje kuzurura na kuacha pending issues kibao kwenye meza yake.
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  mimi naanza kuamini kuwa jk ana nguvu ya ziada nyuma yake, ama ni nguvu ya upako wa Mwenyezi Mungu aliomjalia au kama sio hivyo basi ni ile nguvu ya Sheikh Yahaya na kwa staili hii inabidi tusiidharau!

  Hivi fikiria Madaktari na msimamo wao na kwa jinsi walivyokuwa wamejieleza vizuri kiasi kwamba wengine wetu tulikuwa tunachukua muda mwingi kuangalia tutawasidia vipi madaktari ili wafanikisha madai yao.

  All over the sudden, wakakubali kurudi kazini bila hata masharti! Na si hivyo tu, kaja na kuwaponda hadharani mbele ya wazee wasiojulikana wanamwakilisha nani katika hili sakata!

  Nasubiri kuona mwisho lakini maswali ni mengi kuliko majibu juu ya ushawishi wa huyu bwana!

   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sioni ushawishi wowote katika hili zaidi ya ukweli kwamba Rais kaairisha matatizo na kuyarudisha mabegani mwa wananchi waendelee kuyabeba.

  Madaktari waligundua kwamba wanaongea na mtu asiye elewa ukubwa wa tatizo na umuhimu wa kuingilia kwa busara.

  Ukiamua kupunguza uzito wa madai ya Madaktari na ku sum up kwamba wanadai Mshahara wa 17Milioni huku ukitupilia mbali madai muhimu ya mazingira ya kazi na vitendea kazi hutumii ushawishi bali unafumbia macho tatizo.

  Muhimbili au hospitali yeyote pakikosekana dawa anayeumia ni mwananchi, madaktari wakigoma anayeumia ni mwananchi.
  Rais akipuuzia tatizo la mgomo wa madakitari anayeumia ni mwananchi.

  Inaonekana wengi tunaamini kwamba matatizo ya hosipitali zetu yameisha baada ya mgomo kwisha.
  Au hatuamini kabisa kwamba yalikuwepo kabla ya mgomo.
  Serikali ya CCM inaweza kugharimia chumba cha kulala Naibu Waziri usiku moja akiwa na Changu kwa USD 400.
  lakini serikali hiyo hiyo haiwezi kuwa na fungu la kununua vitanda vya wagonjwa.

  Standard ambayo sisi wananchi tumeset katika huduma ya Tiba iko chini sana kiasi kwamba hatuoni umuhimu wa kuliangalia suala la mgomo na madai ya madaktari kwa undani zaidi. Pia hatuoni umuhimu wa kuyatafakari majibu na ahadiza Kikwete ambayo kwa kiwango chochote hayatoi hata hint ya namna alivyo na ari ya kutatua matatizo yaliyopelekea mgomo.


  Katika madai ya madaktari kulikuwa na madai muhimu sana ambayo wananchi tulitakiwa ku ya paraphrase na kuyamiriki na kuishinikiza serikali kuyatatua.
  Pia,Katika madai kuli orodheshwa Tabia ya viongozi kwenda kutibiwa India na kuacha kutibiwa nchini Tanzania. hili la kutibiwa nje wananchi wengi hata hatuoni kwaba ni tatizo kwa sababu tuna amini ndiyo marupurupu ya uheshimiwa.

  Ni aibu ya Kitaifa, nchi ina miaka 50 ya Uhuru, kiongozi wa nchi na waambata wake bado wanatibiwa nje ya nchi wakati tuna madaktari vichwa sana lakini tumewaweka katika mazingira ya kimahoka. Ni nini miango yetu katika sekta ya afya miaka 50 mingine ya uhuru?? Kutibiwa na akina Maji Marefu??

  Ni kujidanganya kudhani kuwa kikwete ni mu mwenye ushawishi.

  Naamini busara za madaktari wenyewe hasa baada ya kuhakikisha Rais amepata malalamiko yao wenyewe moja kwa moja kutoka kwao na Rais akaonyesha kwamba bado haelewi, kulikuwa hakuna haja ya kendelea na mgomo.
  Kama Rais wa nchi haelewi na wananchi tulio wengi hatuelewi ni bora kusitisha mgomo na kurudi katika meza na kuchora dira upya.

  Ni mpini tu wa hii nyenzo umevunjika si mwisho wa mapambano,huu ni mwanzo wa mwanzo.   
Loading...