Ujima ulitufundisha ukakamavu

Niliwahi kupanda hii kitu upon a time, kwa wenyeji wa handeni kutoka bomani kuelekea chanika mtaelewa hii, eneo hilo pana down kali sana, aisee!!
 
Na tuliozaliwa miaka hiyo tulikakamaa kwelikweli.
 
mmenikumbusha mbali..nilikula henzerani za kutosha kwa kuchana kaptula. hata hivyo ni ubunifu mzuri.
 
Niliwahi kupanda ya mtu tukiwa watoto basi tukaanguka, niliumia sana hasa kwenye paji la uso. Nilikula bakora kwa mama hatari, then akanikanda. Alikuwa anatukataza kuyachezea hayo maana yameuwa sana watoto
Hahahaa mkuu nilihisi tu, maana ndio jina ninalolijua pia. Nimeendesha sana bagadu hasa kimtelemkoni
 
Zamani sana hii kitu. Zinaitwa bagadu kule kwetu


Hakuna cha zamani...mpaka sasa huko vijijini bado zipo, ingawa zimepungua kuliko ilivyokuwa zamani...ubunifu wa aina hii nao umepungua
 
Niliwahi kupanda hii kitu upon a time, kwa wenyeji wa handeni kutoka bomani kuelekea chanika mtaelewa hii, eneo hilo pana down kali sana, aisee!!
Yap ukitoka pale bomani breki ni pale seuta grosary sio
 
Aisee, mbona unakumbushia vidonda vilivyokwisha pona?? Dah! Nilipoteza kidevu changu kwa hii kitu. Ilikata kitu iloitwa "S". Msumari wa kuunganisha "body" na "Stelingi". We. nadhani ilikuwa kwenye speed ya 20 Kpm. Ikakata hiyo "S" yaani msumari wa inchi 6 uliopindwa mfano huo. Nilipiga chini. La haullah! Kidevu hakuna na kupoteza faham. Nilipo amka nikakuta napepewa, umati umenizunguka, mama yangu analia kuwa nimekufa. Sintasahau, na mshana jr umenitonesha kidonda changu.
Shigha du avae!
 
Vigaberi wee tulitumia migomba kutengeneza matail. mteremko unakwenda bila kupenda. Haya magari ni kwa sehemu zenye milima na miteremko tu! Digitali imeua ubunifu wetu nalia na kusikitiaka.
 
Hivi vitu niliviona Makambako Mji Mwema kitambo sana mi mwenyewe nilikuwa bwana mdogo mno nafikiri ilikuwa '89. Jamaa walikuwa wanabebea madumu ya maji halafu wakifika kwenye mteremko wanajiachia kinoma
 
Ubunifu tuliutupa wapi wakuu kama kila mtu anadai kuendesha hiyo kitu na hata kubebea muzigo?!
 
vijana wa zama za VILAZA hawawezi jua hizo mambo,sisi kwetu tukiziita ngolongojo kila mtoto makini zama hizo lazima awe na hiyo kituu😵
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…