Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
UJERUMANI YAZIDI KUFUKUZA WAKIMBIZI.
Mratibu wa masuala ya wakimbizi wa serikali ya Ujerumaini amesema kuwa, nchi hiyo inapaswa kuongeza idadi ya wakimbizi inaowarudisha makwao.
Peter Altmaier alisema hayo jana (Jumamosi) na kuongeza kuwa, kuna uwezekano idadi ya watu wanaoomba hifadhi ya ukimbizi na ambao maombi yao yamekataliwa, ikaongezwa maradufu kwenye zoezi hilo la kuwarudisha mwakwao wakimbizi.
Mwaka jana Ujerumani ilipokea wakimbizi zaidi ya milioni moja wanaokimbia mapigano na umasikini kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Aidha nchi hiyo imekuwa ikijaribu kuongeza kasi ya kufuatilia maombi ya ukimbizi ya watu hao ili kuendana na wimbi la watu wanaokimbilia nchini humo.
Wengi wa wakimbizi waliorejeshwa makwao kutoka Ujerumaini wanatoka nchi za Balkan ambao mara nyingi hukimbilia nchini humo kutafuta kazi. Ujerumani imekuwa ikifanya mazungumzo pia na baadhi ya nchi ili kuzishawishi zipokee wakimbizi wanaorejea. Kwa upande wake, Afghanistan imeahidi kuwapatia sehemu salama za kuishi raia wake wanaorejea nyumbani.
Mratibu huyo wa serikali ya Ujerumani katika masuala ya wakimbizi ametetea pia makubaliano yaliyofikiwa baina ya Umoja wa Ulaya na Uturuki kuhusu kurejeshwa nchini humo wakimbizi wanaoingia barani Ulaya. Hata hivyo, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limelalamikia mpango huo na kuilaumu Ujerumaini kwa kutoa mchango mkubwa katika suala hilo.