Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
SHIRIKA la misaada ya Kijerumani la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) limeiumbua serikali kwa kile ilichoita, kuudanganya ulimwengu kwamba baadhi ya nchi wafadhili zimekuwa zikisaidia vyama vya upinzani kuangusha serikali. Mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo nchini, Stefan Reith, alisema shutuma za serikali kwamba wanavifadhili vyama vya siasa vya upinzani ni ya kusikitisha kwani nchi yao na taasisi za misaada hazijawahi kufadhili mambo kama hayo.
Taasisi za Kijerumani zinafanya kazi na vyama vyote vya siasa nchini. Tunafanya kazi na CHADEMA, tunafanyakazi na CCM (Chama Cha Mapinduzi) na tunafanyakazi na CUF (Chama cha Wananchi). Kote huko hatutoi fedha moja kwa moja bali tunasaidia kuendesha semina, warsha, mikutano, mafunzo na ushauri. Basi, alisema Reith.
Kauli ya mwakilishi huyo wa moja ya nchi zinazotoa misaada mikubwa kwa serikali ya Tanzania, imekuja baada ya kuwapo shutuma za muda mrefu kutoka kwa viongozi wa serikali na CCM, kwamba baadhi ya nchi wahisani zinasaidia CHADEMA kuangusha serikali. Alisema, Kitendo cha serikali kusema CHADEMA inafadhiliwa na Ujerumani si sahihi na pengine ni jambo lisilo na maana kwa sababu kinachopata CHADEMA kutoka KAS ndicho hicho hicho kinachopata CCM na CUF kutoka FES, alisisitiza.
Reith alitoa kauli hiyo jana katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, aliyedai kuwa chama chake kimekuwa kikishambuliwa na serikali kwamba kinapokea fedha kutoka kwa wahisani ikiwamo Ujerumani kwa nia ya kuiangusha serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wakati ambapo madai hayo hayana ukweli. Dk. Slaa alisema hawajawahi kupewa fedha kwa ajili ya maandamano ya kupindua nchi bali wamekuwa wakipata fedha kwa ajili ya kuendesha semina, makongamano na warsha.
Nasema mbele ya wafadhili wetu Wajerumani waseme kama wametupa hata senti kufanya maandamano hawa wanasaidia shughuli kama hizi za semina ya mabadiliko ya tabia ya nchi, alieleza Dk. Slaa huku akimtolea macho mwakilishi huyo wa taasisi ya Kijerumani. Tusipumbazwe katika siasa zisizo na tija, mbona serikali inasaidiwa kwenye bajeti yake asilimia 34, wakisaidiwa wao sawa CHADEMA ikisaidiwa nongwa, alieleza Dk. Slaa.
Katika mkutano wa Bunge la bajeti, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania, Benard Membe, alizituhumu nchi wahisani kuvisaidia baadhi ya vyama vya upinzani nchini kutaka kuiangusha serikali; madai ambayo yaliibua mjadala mkubwa bungeni. Akichangia kauli ya Membe, Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, alimtaka kiongozi huyo wa serikali kuthibitisha madai yake, kutaja nchi ambayo alisema inafadhili upinzani au kufuta kauli yake. Membe aligoma kufuta kauli hiyo, wala kutaja nchi aliyoituhumu, badala yake alisema, Wahusika wanajijua.
Source: Tanzania Daima