ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,685
Kwa hakika mahitaji ya formwork na falsework (hizo mbao, mirunda uliyotaja nk) ni moja ya gharama kubwa katika ujenzi wa nyumba za kawaida. Ingesaidia kiasi wakitokea wajasiriamali watakokusanya mbao used sehemu mbalimbali na kuwauzia wajenzi wapya kwa bei nafuu.
Ngoja waje wenye nazo!
Idea nzuri sana umetoa. Hapa tunaona kuwa Bongo business opportunities bado ni nyingi sana.
Wadau changamkieni idea ya Mwasyoke hii, ameitoa bila patent kwa nia njema...
You never know ndugu yangu. Kesho unaweza kuamka na wewe unazo.
Follow this space closely.
Lakini hapa sio kwa wenye nazo, hapa ni kwa wale wanaotaka kusave. Wenye nazo wanaajiri kampuni liwafanyie kazi, wao wanaenda kuchukua funguo tu.
Nitarudi tena baadae
"VV"
Ukitaka kujenga hakikisha unayo pesa sio kuleta ubangaizaji ndio mwishowe ni kuuwana; vifaa chakavu vya ujenzi haviwezi kuwa na strength ileile kama vikiwa vipya sasa unapovifanyia biashara ya kuvizungusha na kuvizungusha gorofa hadi gorofa mwishowe ni misiba na kuishia jela. Kama huna pesa kapange usilete biashara kichaa kwenye uhai wa wenzio
Jamani tukae tukijua kuwa mbao si re usable materia hasa kwenye ujenzi.....kwani uimara wa structure yako ni pamoja na uimara wa form works ulizotumia.......
MODs, naomba thread hii msiiunganishe na nyingine.
Lengo la thread hii ni kupeana maarifa ya jinsi ya kupunguza gharama za ujenzi wa SLAB ya ghorofa.
Gharama ya ujenzi wa slab "inatia uchungu" kwa vile inahusisha mahitaji ambayo ni disposable lakini ni ya gharama kubwa. Mahitaji hayo ni support ya kubeba zege (mbao, plywood au iron sheet), mirunda, vyuma na misumali. Gharama hizi zinakadiriwa kuwa asilimia 20 ya materials za slab nzima. Hii si gharam ndogo. Kwa ghorofa moja yenye slab ya mita za mraba 140 inahitajika kama shilingi milioni 3.5 - 4.
Kuhusu Mbao, plywood, iron sheet na mirunda kuna haja ya kubuni mbinu mbalimbali za kupunguza gharama kama ifuatavyo:
1. Tafuta jirani aliye kwenye hatua inayofanana na wewe kwenye ujenzi na ukubaliane naye akuuzie materials zake akimaliza au wewe umuuzie ukimaliza.
2. Ulizia iwapo kuna wakodishaji wa vifaa hivyo. Hakikisha unakubaliana bei na jinsi ya kufidia mbao na mirunda itakayokatwa.
3. Nunua materials mpya na uanzishe biashara ya kuzikodisha baada ya kutumia.
4. Fanya urafiki na watu wenye makampuni ya ujenzi. You can even get these materials FOR FREE!!!
5. Anza kukusanya materials kidogokidogo toka kwa wajenzi wasiohitaji. Kama jirani yako anataka kutupa mrunda muombe akupe, akiweka mbao jalalani chukua. Kama kichaa vile lakini inaweza kusave you a great deal of money.
6. Kuwa mkali kwa fundi asitupe na kupoteza vipisi ambavyo vingeweza kufanya kazi na more importantly "asikosee mahesabu".
7. Nunua vifaa unavyohitaji kwa wingi kwa pamoja katika maduka ya jumla. Ukiamua kufanya hivyo hakikisha una utaratibu salama wa kuvihifadhi.
Njia hizi zinaweza kupunguza gharama za materials hizi "disposable" kwa asilimia 50-90!
Katika thread hii wale wenye biashara za kukodishe mbao, plywood, iron sheer, mirunda, vyumba etc tafadhali wekeni terms za biashara zenu ili kuwapa members picha halisi ya jinsi wanavyoweza kupunguza gharama za ujenzi wa slab.
Iwapo umejenga slab na una materials zilizobaki. Tumia thread hii kuingia deal na wadau ili uwauzie au kuwakodisha. Kwenye ujenzi tunasema "every shilling is GOOD". Save shilling yako kwa kuuza mbao ambazo zingeliwa na mchwa.
Kabla sijaanzakijenga nyumba ninayo ishi sasa, nilitamanis ana kujenga kagorofa ka kishkaji lqkini ardhi niliyo nunua nikaona haitaweza kumudu gorofa. Nikaanza ujenzi wa kawaida, kama mnavyo jua msingi wa nyumba wa kawaida hauendi chini sana kama wa gorofa, baada ya kupauwa na finishing nyingine ndogo ndogo nikaamua kuchimba shimo la choo.
Siku wanaanza kuchimba sikuwa site jioni nikapigiwa simu kuwa kazi ngumu sana kutokana na mapatano yalivyokuwa, kesho yake nikaenda site nikakuta wamesha chimba kama futi tatu hivi lakini kando kulikuwa na na mawe makubwa wakasema wametoa ndani ya shimo. Ardhi ilikuwa ni nzuri yenye kuweza kubeba hata gorofa kumi. Nilijisikia vibaya na nilikuwa nishachelewa.
Baada ya miaka 6 nikanijia wazo la kubomia hii nyumba nijenge house of my dream lakini nikiangalia gharama nilizotumia mpaka sasa nashindwa nini cha kufanya.
Nimemaliza kumwaga zege. Nina mirunda 700 (bei @ 1,500) Marin Board 65 (bei @ 40,000) Mpya zimebaki 5 ambazo naziuza kwa (@ tshs 50,000) na Mbao za 4x2, 6x2 na 10x1 nyingi). zote zimetumika mara moja na ziko katika hali nzuri. kwa anayehitaji zitakuwa available baada ya wiki 2 kuanzia leo. unaweza anza fanya booking mapema na ukajiandaa kuzichukua. ni PM au piga 0713 60 28 00
Jamani tukae tukijua kuwa mbao si re usable materia hasa kwenye ujenzi.....kwani uimara wa structure yako ni pamoja na uimara wa form works ulizotumia.......
Iko hivi kaka mbao inapoteza strenth kila inapotumika so the more inatumika ndivyo strenth inavyoisha na kwenye structure ili ikae ni lazima kile kilichoshikilia kiwe na strenth ya kuweza kuhimili forces.zaidi kama ni slab itasag kama unatumia mbao zilizotumika mara nyingi kuna kitu kinaitwa bending moment. Inashauriwa mbao isitumike zaidi ya mara tatu kama sikosei. Mwisho mi sio eng ni architect so majibu sahihi ni yale atakayoshauri eng thanks
Iko hivi kaka mbao inapoteza strenth kila inapotumika so the more inatumika ndivyo strenth inavyoisha na kwenye structure ili ikae ni lazima kile kilichoshikilia kiwe na strenth ya kuweza kuhimili forces.zaidi kama ni slab itasag kama unatumia mbao zilizotumika mara nyingi kuna kitu kinaitwa bending moment. Inashauriwa mbao isitumike zaidi ya mara tatu kama sikosei. Mwisho mi sio eng ni architect so majibu sahihi ni yale atakayoshauri eng thanks