Ujenzi wa "Mfumo Magufuli", hatari na janga kwa taifa kuliko Rais Magufuli mwenyewe

Ninavyojua mimi hata siku moja hakuna mtu aliyeomba dictator tu bali siku zote wakati wa awamu ya nne watu walikuwa wanaomba 'benevolent dictator'; siyo 'ruthless dictator. Mfano wa benevolent dictator ni Nyerere mwenyewe.

'Unavyojua Wewe' sio inavyojulikana sasa naanzia wapi kukubishia
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa uzi mujarab. Haya anayoyafanya jiwe ndio hasa sababu kubwa ya Waafrika kuendelea kuwa duni, hohehahe katika bara lao. Na hii iko mahali pengi barani Africa. Jiwe si tu ni katili.. bali pia hana akili nyingi.. ni mtu wa kukurupuka sana.. na kwa udhaifu huo.. hapendi wanaomzidi akili.

Kutengeneza mfumo Jiwe ni kiama kwa nchi yetu.. na sofahamu hawa watu wanaotengeneza mifumo wao akili zao zinakuwa zinaangalia wapi.. Jiwe kama walivyokuwa wengine hawezi kuishi milele.. kwa hiyo ni upuuzi mtupu kujenga mfumo usioweza kudumu..

Badala ya kujenga mfumo jiwe, jamaa angekuwa na akili na nia njema kwa Tanzania angetumia muda wake kujenga taasisi imara kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu kwa miaka 100 ijayo.. taasisi hizi ni kama ifuatavyo

1. Mahakama.. mfumo jiwe haujielewi hata kidogo. Kama ungekuwa na nia ya dhati ungeimarisha mhimili huu muhimu ambao kimsingi uimara wake ungetokana na uhuru wake, kuwa na uongozi wake usiotegemea muhimili mwingine na pia mhimili huu kuwa na bajeti yake isiyoyumbishwa na mtu yeyote.

2. Bunge.. hii ilitakiwa iwe ni taasis imara yakuisimamia serikali badala ya ilivyo sasa ambapo tasisi hii ni ya hovyo na haina msaada wowote kwa nchi kwani inaendeshwa kwa maagizo kutoka Ikulu.. hii ni tasisi ambayo kwa kiwango kikubwa inachangia mateso kwa wananchi kwani imeshiriki kufanya maamuzi ya kipuuzi ili tu kumfurahisha jiwe.. hapo hatuwezi kusogea popote

3. Taasisi za kiserikali
Taasis hizi bado ni dhaifu mno.. kuliko watu wengi wanavyodhani.. ni dhaifu kiasi kwamba bado taasisi hizi utendaji wake unafuata nani aliyepo ikulu.. hii ni hatari sana. Utakuta akiwepo mtu serious, taasis nazo zinakuwa serious, akiwepo mtu bogus, nazo zinakuwa bogus. Taasisi nyingi bado hazina watumishi wenye uwezo kitaaluma.. yaani wapo wapo tu.. na kwa vile mhimili wa bunge ni mbovu, hata kuziwezesha hizi tasisi kibajeti bado ni tatizo kubwa. Hata zile ambazo zinawezeshwa kibajeti, accountability ndani yazo ni hafifu sana..

4. Jamii
Jamii ni tasisi muhimu sana ambayo maendeleo yote hutegemea ushiriki wa jamii hiyo.. taasis hii bado ni dhaifu sana kwa kila hali. Jamii haina interest kuhusika na chochote kinachofanywa na serikali kwa niaba yake. Jamii iko mbali sana na maamuzi yanayofanywa na taasis zingine, iwe au isiwe matokeo ya maamuzi hayo yaathiri moja kwa moja au vinginevyo, jamii husika. Wanajamii wengi ni wazembe, kwa maksudi au vinginevyo, hawawezi kuhoji swala lolote. Jamii haina nafasi bado linapokuja swala la kupanga mustakabali wa nchi. Mfumo jiwe wenyewe unataka jamii isifie tu maswala ambayo mengi ni ya hovyo..

Tunatokaje hapa?
Kama ulivyosema hapo awali.. kama jamii lazima tuwe na uwezo kuzuia kujengeka mfumokwere, mfumogongo.. mfumomaembe.. mfumolwasha.. nk...
Upenyo pekee wa kuingilia ni njia ya katiba mpya. Jamii ya watanzania lazima waendelee kuelimishwa kuhusu ubovu wa mifumo watu. Jamii ione uhitaji wa katiba mpya kwa ajili ya jamii yenyewe. Katiba inayotumika sasa ni katiba ya hovyo sana na si ajabu uduni wetu kama jamii umechangiwa na katiba hiyo. Katiba iliyokuwa na lengo la kujenga "Yes Nation". Ukisikia mazuzu pale bungeni yansema Ndioooo, juwa kwamba hiyo ni athari ya likatiba la kijinga linalotumika kwa sasa..

Mimi na wewe tuendelee kuielimisha jamii, yakiwemo mazwazwa machache yanayooangalia mwisho wa pua zao kuwa maendeleo ya nchi yetu yanategemea kwa kiwango kikubwa namna tutakavyoamua namna inayifaa kujitawala..

Shukrani sana kwa hoja

mkuu huu ni moja ya michango bora kabisa kuwahi kusoma kwenye jukwaa hili. fikra huru na pana kama zako zinahitajika kulijenga taifa letu. umengeza uzito wa kipekee kwenye mada yangu maana umejikita kwenye majawabu.
 
Nyerere ndo chanzo cha hii katiba mbovu itukuzao MTU badala ya utaifa,aliiga toka Kwa rafiki yake Mao aliyekuwa akiabudiwa kama mungu.Ilitakiwa nyerere kabla ya kung'atuka ili kulinda heshima baada ya kuona hawezi pambana na mabeberu angeibadili ili iwe katiba ya wananchi kutoka kuwa katiba ya kulinda watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kula tano mwanangu. Nyerere alijua hii katiba ni mbovu lakini hakuona shida kwani alizungukwa na watu wanaojipendeza na kumsifu kwa kila jambo kama ilivyo sasa kwa magu. Hivyo alitumia hiyo katiba mbovu kujivika uungu mtu
 
Swadakta,, huu uzi utakuja kufukuliwa miaka si mingi,, na ww unaweza ukaitwa mbashiri

kwanza niseme sikushangai maana wewe ndio aina ya watu wanaotengenezwa na wanaotakiwa na MfumoMagufuliNiJanga. kinachofurahisha ni pale tu unapotaka kujionesha wewe ni mtaalamu wa riviu za maandishi. kwa hiyo kwa utaalamu wako wa riviu unaamaini kabisa kwamba kusema kikwete aliruhusu familia yake kuishi kifalme na kuingilia mambo ya uongozi kinyume chake ni kawa rais magufuli kuficha tusijue watoto wake na mke wake kuwa mnyonge? pia utaalamu wako wa riviu unakuambia rais kuwa mkatili kwa familia yake (mke na watoto) haina uhusiano na uongozi wake? kama anaweza kuwa mkatili kwa anayelala naye kitanda kimoja au kumfanya kuwa mnyonge unadhani roho ya kuwafanya watanzania kuwa wenye furaha ataipata wapi?
 
Contradictions:
Mzee Kikwete analaumiwa kwenye Uzi huu kwa kuifanya familia yake iishi kifalme na watoto wakawa na kauli hadi siku za mwisho wa utawala wa baba yao.
Ndani ya Uzi huo huo, unamkosoa Rais JPM kwa kutoitambulisha familia yake, kuozesha wanawe bila sherehe n.k.
Nashindwa kuelewa, tusimamie lipi ikiwa ulichokikosoa kwenye utawala uliopita, kimefanywa tofauti awamu hii lakini pia hujaridhika nacho.
Tuwe na kauli thabiti...ili tujulikane tunalolisimamia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Jitambue, ukiambiwa umejaza chakula chumvi, kujirekebisha sio kutokuweka chumvi kabisa.
 
Hatari kubwa ni kuwa Magufuli mfumo wake tofauti na wenzake anauweka kwenye sheria hivyo utaishi miaka mingi baada ya yeye kuondoka. Mfano, Sheria kama za takwimu, za vyama vya siasa nk.
Anahakikisha mfumo wake unakuwa na support kisheria. Hii ni hatari kubwa sana.
 
Acheni Blaa Blaa
Rais Magufuli Kaja wakati muafaka Sana kunyoosha Hii Nchi

Naunga Mkono juhudi Za Juma Nkamia Za Miaka 7, Tena ikiwezekana iende sambamba Na kufuta Ukomo wa Urais ili John Magufuli apate fursa ya kunyoosha mikunjo yote iliyosalia
Anainyosha nchi kutoka wapi na kuekekea wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi wenzangu wa The Home of Great Thinkers niwasalimu. kwanza nichukue nafasi hii kuwaaga wale wadarisalama maana sisi wenzenu watumishi wa umma kikokotoo cha kutuhamishia Dodoma ndio kimekamilika mwaka huu hivyo wachache tuliobaki kumpa joto mzee ndio tunapaki mabegi tayari kwa safari muda wowote atakapotoa kauli.

tunapoanza mwaka wa 2019 nataka niwaachie mada ya kutafakari kuhusu Rais Magufuli. leo sitataka kujadili mambo yaliyo nyuma ya matukio na maneno yake ambayo wakati mwingine yako kama bongo muvi bali nataka mumtazame magufuli kama mfumo na hatari inayoikumba nchi yetu sasa na huko tuendako kutokana na mfumo magufuli. kama kawaida, nisome ukiwa na fikra huru ili unielewe.

kama mbavyo Mwalimu Nyerere amewahi kutuambia huko nyuma, katiba yetu imempa rais wa nchi mamlaka ya kifalme. yule mzee wa kikwere pale msoga asiyetuletea janga kupitia magufuli aliwahi kusema katiba imempa mamlaka makubwa sana hadi anaogopa kuyatumia. ukubwa wa mamlaka haya una mambo mengi lakini kubwa ya yote ni jinsi ambavyo yanampa rais uwezo wa kujenga mifumo mingi ambayo inaweza kuwa na faida au hasara na ikaleta kicheko au mamumivu kwa wananchi kwa muda mrefu. nitoe mifamo michache.

nguvu ya mamlaka ya rais ndio ilimfanya Mwalimu Nyerere aheshimiwe na fikra zake kuchukulia kama vile ni maandiko ya dini hadi leo. urasi ulimfanya awe wa kipekee. pia ndio ilimfanya aweze kutekeleza kila mpango alituletea hata kama ulikua na maumvi na bado tukaona ni sawa tu. alituletea azimio la Arusha, vijiji vya ujamaa, kilimo cha kufa na kupona, na mengine mengi na tulitekeleza. hii ni kwa sababu nguvu aliyokua nayo ilimtisha kila mtu. nguvu ya urais wake ilimrahisishia kujenga mfumo Nyerere wa taifa la watu wapole, wenye utu, na wenye kiburi cha mdomoni na maneno mengi lakini wanyonge kifikra mbele ya mataifa mengine.

mzee Mwinyi alipokuja na mama Siti wake nao wakaja na yao. mamlaka ya urais ikamfanya kutekeleza sera zake tofauti na za Mwalimu na kuacha mambo mengi yakaenda ovyoovyo ikiwa ni pamoja na mama Siti kuwa na mamlaka kama vile ndio msaidizi wa rais kikatiba. hakuna aliyeweza kupingana na waliyokua wanayafanya. matokeo yake nchi ikawa na mfumo wa ovyo, rushwa ikatapaa na kuzidi, siasa ikawa biashara, na mengine mengi. wale wazee wenzangu mutakumbuka maisha yalivyokua na madhara mfumo mwinyi ulioendelea hata baada ya kuondoka kwake.

ngumu hiyohiyo aliingia nayo mzee mkapa na sera ya uwazi na ukweli. pamoja na mambo mengine mazuri aliyofanya kujenga uchumi na taasisi, ilimwezesha kuuza mashirika ya umma ovyoovyo, kuuza nyumba za serikali kishikaji hadi magufuli akahonga zingine kwa ndugu na mahawara zake, na akaruhusu baadhi ya watu wakawa na nguvu kubwa sana kiuchumi. huyu akatuachia mfumo mkapa ambapo ukata ulionekana sehemu ya maisha huku kundi dogo likifaidi.

mzee wa kikwere alipokuja na mfumo wake wa wanamtandao, alitumia mamlaka makubwa ya kiti cha urais kuishi kifahari yeye na familia yake na kufanya kila alichotaka. tutakumbuka alivyoanza uraisi kwa starehe za safari ya kuzunguka dunia kwa kile alichoita kujitambulisha na akaendelea hivyo kwa miaka kumi hadi mwezi wa mwisho wa urais wake akiendelea na ziara za alichokiita kuaga nchi washirika utadhani walimchagua wao. madaraka na utajiri wa nchi ulioachwa na mkapa akafanya vikawa vya kugawana na washikaji wake. akajenga mfumo wa watumishi wa umma kula bata kwa safari za kila siku na kila mahali. kwa urais wake akaruhusu wala rushwa wengi wao wakiwa ni washikaji wake na waliomweka madarani wakafanya wapendavyo huku yeye akitabasamu. tunajua ni skendo ngapi za wizi kaziacha. kama vile haitoshi, familia yake ikawa ya kifalme na tukashuhudia watoto wake wakitoa kauli za ajabu kabisa hadi siku za mwisho za uongozi wake na hawakua na hofu. akatuachia nchi yenye mfumo kikwete ambao ni mdebwedo, wa kizembe, na dhaifu kama ambavyo wapinzani wake walivyokua wanamwita. mbaya akataka kutuamulia nani awe rais ili kuendeleza mfumo kikwete na matokeo yake ndio yakalipelekea taifa kupata janga kubwa la rais ambaye hadi sasa anaendesha nchi kikatili na kama familia yake. yako baadhi ya mambo machache mazuri ya kuenzi kama ilivyo kwa waliomtangulia aliyoyaacha lakini sio sehemu ya mada hii kuyajadili kwa sababu yanafunikwa na janga alilotusababishia.

nimekupa mifano hiyo ili ikusaidie kuelewa ninachamaanisha kwa kumtazama Magufuli kama mfumo na madhara yake kwa taifa. hao wote waliotangulia walitumia nguvu ya mamlaka ya urais kujenga mifumo ambayo kwa namna moja ua nyingine iliboresha hali ya maisha yetu na wakati mwingine ikatuletea matatizo ambayo hadi sasa yanatuandama. hata hivyo uharibifu wao ni ngumu kuufananisha na ubaya wa mfumo magufuli.

sasa tumfazame ujenzi wa mfumo magufuli. kwa kuwa lengo kuu ni kuitahadarisha nchi juu ya madhara ya Mfumo Magufuli nijikite kwenye yale ambayo nataka tuyatafakari na yatusaidie kuamua mustakabali wetu juu ya uongozi wake huko tuendako. yale machache mazuri ya kumsifia niwaachie waliopewa jukumu la kusifia na kuyatumia hayo kama kivuli cha kufunika ujanga unaotukabili. nitaongea kwa kifupi ili nisikuchoshe.

matendo na maneno ya magufuli tangu aingine kwenye urais yanajulikana. ni mtu anayejitahidi sana kujionesha ni mwema lakini ndani yake akiwa na roho mbaya, katili, na yenye ushetani mwingi. tumeshuhudia chuki ya ajabu toka kwake kwa wale anaowaona kama adui au wapinzani wake. tumeona vifo na tumeona uminywaji mkubwa wa haki na uhuru kupitia matamko, amri, sheria na kanuni mbalimbali. kwa mara ya kwanza tumeona rais ambaye anafurahi majeshi kuliko raia na ambaye haoni aibu kuwasifia hadharani hata wanapotenda kinyume na katiba. kwa mara ya kwanza kwenye historia ya nchi tunaona rais ambaye hajali maadili na utukufu wa utumishi wa uma. kateua watu wa ajabu kuwa viongozi na kawapa amri na mamlaka ya kukandamiza wengine. ni rais anayewapa zawadi watenda makosa na anayepandisha vyeo wala rushwa, wakatili na wasiotii sheria. tunaona rais ambaye ana chuki ya kutisha kwa vyama vya upinzani na kaamua kuongoza zoezi la rushwa ya kununua wapinzani wawe upande wake. tuna rais anayechukia haki na demokrasia kupita kiasi. kwa mara ya kwanza taifa linaongozwa na rais ambaye halijawahi kumwona akijitambulisha na familia yake. taifa halijui watoto wake, watoto hawana ujasiri wa kujitambulisha na sina hakika kama wana ufahari na urais wa baba yao, na mke wake siku zote ni mnyonge. tuna rais anayejisifia hadharani kwamba watoto wake hawafanyi hata sherehe za harusi kwa amri zake na anataka tuone ni sawa.

bila shaka umeona mfumo magufuli, ujenzi wake na una sifa gani. mzee huyu anatujengea nchi ya mfumo wa kikatili. mfumo unaonyima watu haki zao kwa amri za kijinga. mfumo wa mtu kutokua na hakika ya kuishi maana muda wowote unaweza kuuawa kwa kwa sababu yoyote ile. mfumo ambao watu waovu walio karibu na rais wako salama na wanaweza kufanya lolote na maovu yao kutakatishwa. mfumo magufuli ndio umezaa viongozi aina ya Makonda, Ali Happi, Jeri Muro, Sabaya, Mnyeti, kamanda Siro, Mwambosasa, na wengine kama wao. mfumo wenye jeshi la polisi katili kwa raia na usalama wa taifa kuwa chombo cha mauaji na mateso ya raia. mfumo usiojali maisha na uhai . mfumo unaodharau katiba na sheria za nchi. mfumo wa watu wasiokua na fikra huru bali wako radhi kusifia kila kauli na matendo ya rais hata kama yeye mwenyewe haamini katika hayo, mfumo wa chama cha mapinduzi cha mazuzu wasio na uwezo wa kuhoji wala kuuliza bali kufuata maagizo ya rais. mfumo ambao umewafanya wasomi na wanataalamu kukosa uhuru wa kutoa mawazo ya kisomi kwa uhuru kwa kuogopa kupingana na rais maana hajulikana anasimamia nini. mfumo uliotuondolea uhuru tuliokua nao wa kujadili siasa na viongozi kwa uhuru na mtu yoyote mahali popote bila kuogopa kuwa unawindwa. mfumo uliowateka viongozi wetu wa kiimani na kuwafanya kuwa wanafiki bila woga. mfumo wa chaguzi kukosa maana na kura kuporwa mchana na watu kumwaga damu.

watanzania, hii ndio hatari inayotukabili. tunaohoji kauli, matendo na uongozi wa magufuli haya ndio tunayotaka watu wayaone. yeye mwenyewe ni janga na tishio lakini kinachotisha kupitiliza ni mfumo magufuli anaotujengea. mfumo unachukua muda kujengwa na kuimarika na unachukua muda kuuvunja na kuubadilisha. ndio maana hadi leo tunateseka na baadhi ya mifumo tuliyoachiwa na Nyerere. pia magufuli bado anapambana na mfumo kikwete. mfumo huu wa kikatili utaitesa Tanzania kwa miaka mingi sana baada ya urais wa magufuli hasa iwapo tutamruhusu kuendelea kuujenga kwa miaka 10. nchi zilizoongozwa na viongozi wakatili zimeteseka kwa miaka mingi sana kuvunja mfumo huo. mfumo wa mauaji uliojengwa na chama cha KANU chini ya Moi unaitesa Kenya hadi sasa. wakenya wamendelea kuuana na kuchukiana hadi leo. ni kawaida kupigwa risasi, kupotea au kuuawa njiani. uganda wanateseka na mfumo wa iddi amini hadi leo. ukatili ndio unaendesha nchi na umetamalaki kwenye majeshi.

watanzania, magufuli ni janga kwa nchi yetu maana anatujengea mfumo magufuli ambao ni hatari na wa kutisha kuliko magufuli mwenyewe . tuna nafasi ya kuukataa mfumo huu na kuharibu ujenzi wake kabla hatujachelewa. tusidanganyike na miradi ya ujenzi na maamuzi ya ajabuajabu kama ya kununua ndege kama nyanya sokoni. haya ni mambo madogo sana ukilinganisha na athari ya mfumo magufuli.

wekeni kumbukumbu ya ujumbe huu kwa matumizi ya baadaye

#MfumoMagufuliNiJanga

tukutane Dodoma
Naunga mkono hoja huu mfumo ni wa makatili tupu yamejazana serikalini.
 
Nyie ndio machizi juzi mlikuwa mnalia CCM ni mafisadi leo kwa kuwa na akili fupi mnapinga mambo yote ambayo Mheshimiwa Rais Magufuli anatekekeza ikiwa pamoja na sera zenu. Je mnataka Rais wa aina gani. Bro ningewashauri mjaribu kwenda kuishi Kwenye sayari ya Mars ili mpate aina ya Rais mnaomtaka.
Rais Magufuli is a great asset kwa watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kilichotufanya tujue ccm ni mafisadi ni uhuru wa vyombo vya habari. Je sasa uhuru huo upo? Kama ufisadi umeisha kipi kimemfanya CAG aseme bunge ni dhaifu kuhoji ufisadi aliouonyesha? Sasa hivi hakuna vita ya ufisadi bali kuna mapambano dhidi ya matumizi ya neno fisadi.
 
kwanza niseme sikushangai maana wewe ndio aina ya watu wanaotengenezwa na wanaotakiwa na MfumoMagufuliNiJanga. kinachofurahisha ni pale tu unapotaka kujionesha wewe ni mtaalamu wa riviu za maandishi. kwa hiyo kwa utaalamu wako wa riviu unaamaini kabisa kwamba kusema kikwete aliruhusu familia yake kuishi kifalme na kuingilia mambo ya uongozi kinyume chake ni kawa rais magufuli kuficha tusijue watoto wake na mke wake kuwa mnyonge? pia utaalamu wako wa riviu unakuambia rais kuwa mkatili kwa familia yake (mke na watoto) haina uhusiano na uongozi wake? kama anaweza kuwa mkatili kwa anayelala naye kitanda kimoja au kumfanya kuwa mnyonge unadhani roho ya kuwafanya watanzania kuwa wenye furaha ataipata wapi?
Mkuu ujanielewa tu,, mi sijapingana na wewe,, ila namaanisha kuwa Kuna watu kwasasa watakupinga,,
Ila Ipo siku ulichokiandika madhira yake yatakapomuenea kila mtu au kumfika,, basi ndio watatambua kuwa uliandikaga ukweli mtupu
 
Jamaa kashakuambia hata kina Hitler walikuwa na mazuri yao! Lakini je, ushawahi kusikia wakikumbukwa kwa mazuri yao? Kama unasadiki, je ni kwa nini hawakumbukwi kwa mazuri?
Mimi pia nimeliona hili. Yaani kwake yeye hakuna hata mmoja mwenye jema! Kila zama kwake ni mbaya? Basi labda ije ghalka ndio labda nafsi yake inaweza ridhika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifupi magufuli atakumbukwa kwa udikteta wake na sii vinginevyo! Jitu gani lisilotaka kukosolewa bwana?
Kumtaka hayawani aishi kama binadamu ni kukosa akili.
Mbona haumvalishi chupi na gauni au suruali huyo mbwa ili kuficha tupu zake?
Si unataka aishi kama binadamu?

Kilicho cha aibu ktk jamii yako sio aibu kwa jamii nyingine. Aibu au haya ni subjective, ninaweza kuona haya kula hadharani lakini kwa mwingine haoni haya tena anaona anaekula ndani kwa kujificha ni mchoyo.

Wewe unae mcheka mtu anaekula hadharani kesho unaenda shuleni wanakofunza maadili unakula hadharani au harusini unakula hadharani na waalimu wako wa nidhamu?!!!
 
Kilichotufanya tujue ccm ni mafisadi ni uhuru wa vyombo vya habari. Je sasa uhuru huo upo? Kama ufisadi umeisha kipi kimemfanya CAG aseme bunge ni dhaifu kuhoji ufisadi aliouonyesha? Sasa hivi hakuna vita ya ufisadi bali kuna mapambano dhidi ya matumizi ya neno fisadi.
Toka mwaka 1996 mpaka mwaka 2015 pamoja nakudai kuwepo kwa demokrasia Tanzania ilipoteza shilingi ngapi kwa ufisadi. Rais Magufuli amejitahidi hata kwa muda wa miaka 3 tumeona anavyoshughilikia miundo mbinu na kuweza kukusanya kodi vizuri sana. Sasa nyie mafisadi ama lazy people msikimbilie mgongo wa demokrasia kumukwamisha huyu kiongozi shupavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUJIKUMBUSHE NA KAULI ZA BAADHI YA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI KATIKA KUTABIRI RAISI TULIYENAYE SASA.

Kumbukumbu na ushahidi unaniambia kuwa manabii hawakutulia bali wote kwa umoja wao walipaza sauti kila ilipoitwa leo kutabili Raisi ajaye. Na utabili huu ulianza mwishoni mwa mwaka 2010 na kuzidi kati ya miaka ya 2014.
Ni wakati ambapo timu ambayo ilikuwa machachali na timu ya hatari tena ilikuwa balaa katika tabiri nyingi za nafasi ya URAISI na Mungu wa Mbiguni alikuwa upande wao kutimiza tabiri hizo.

Zifuatazo ni baadhi ya tabiri hzo.

>Tunataka Raisi ambaye hata angalia sura ya mtu (Mhs. John Myika 2012 akiwa Kirombero Morogoro).

>Tunataka Raisi mkali asiye cheka cheka na mtu (Mch. Msigwa akuwa Mbeya).

Tunataka Raisi asiye safiri safiri nje (Mh: Freeman Mbowe akiwa kanda ya Ziwa 2013).

>Nchi hii inahitaji Raisi Dikteta na sivinginevyo (Mh: Tundu Lisu akiwa Dar).

>Tunataka Raisi ambaye atakuwa anakusanya kodi (Mh: Freeman Mbowe akiwa Tandahimba).

>Tunataka Raisi atakaye isimamia elimu ya Tanzania ( Viti Maarumu Jina ....... Bungeni).

>Tunataka Raisi ambaye atarudisha nidhamu serikalini (Mh: Godbless Lema Mbeya).

>Nchi hii inataka Raisi atakaye wafunga jela mafisadi (Mh: Heche Tarime).

>Tunataka Raisi atakayerinda Mali asili zetu (Mh: Mchungaji Msigwa 2014 Bungeni).

>Anatakiwa Raisi atakaye kuwa anakerwa na rushwa ( Dr. Wilbroad Slaa akiwa Dar).

Nchi hii inataka Raisi atakayekuwa na maamuzi magumu (Mh: Selasini akiwa Rombo ).

Kama kumbukumbu haziko sawa twaweza rekebishana.
Raisi wetu tukubali au tukatae ametusaidia sana kuwaelewa wanasiasa maana mtu anasema tunataka Raisi atakaye kuwa anakusanya kodi wakati yeye halipi kodi. Tunataka Raisi wa kufufua shirika la ndege TZ, lkn ndege zikinunuliwa wanasema cyo priority. Tunataka Raisi asiyesafiri, sasa hasafiri wanasema anatakiwa kwenda kutembea nchi za wenzetu. Tunataka Raisi atakaepunguza/kuondoa michango mashuleni baada ya kufanya hvo wanasema ilikuwa bado kwa TZ kutoa elimu bure. Tunataka Raisi anatakayesimamia madini yetu, baada ya kuanza kufanya hvo wanasheria wa upinzani wanawaunga mkono wezi wa madini. Kwakweli siasa ni shidaa!

Kwenye hizo kauli zote za hao wapinzani hukusikia wanataka katiba mpya inayotaka rais akifanya makosa ashitakiwe? Ulipowasiliza hukusikia wakiongea tume huru ya uchaguzi? Kama hayo uliyotaja ndio yanafanyiwa kazi, je hayo aliyoacha kamuachia nani? Au masikio yako na yake yanachuja baadhi ya maombi ya wapinzani? Unafiki haukubebi kwenye hili.
 
Si wajibu wangu kukufundisha kuandaa propaganda hasa zenye mlengo wa kukufaidisha wewe binafsi na kundi lenu la wachumia tumbo wachache.
Wewe huwezi kuona mapungufu ya kitaaalamu ya bandiko hili.
Hiyo taaluma ya kufanya review ya maandishi ya watu sio kazi rahisi.

Mfano mmoja rahisi ni pale anapomshambulia Kikwete kwa kuiiingiza familia yake ktk masuala ya kisiasa au kutumia mamlaka na ofisi ya taasisi anayoiongoza (uraisi na mwenyekiti wa CCM).

Huku upande wa pili anamshutumu Magufuli kwa kuiweka familia yake mbali na taasisi ya uraisi na uenyekiti wake wa chama.

Huoni hapo anajichanganya na kupangua hoja zake mwenyewe?

Ukiacha kujichanganya angalia pia kama kuna umuhimu kama taifa tujikite ktk kujadili familia ya rahisi kwamba mkewe na watoto wake hatujaona wakitabasamu au wakifanya sherehe za harusi ili kuufurahisha umma kwamba wapo vizuri kama familia. Hii haiwezi kuwa ajenda ya kitaifa bali ni ajenda ya kuuzia magazeti ya udaku au kukusanya followers na likes nyingi kwenye social media.
Hivi kipimo cha furaha ya mke wa rahisi ni kipi?
Je mke wa raisi si binadamu? Huoni kwamba kuna mengine yanayo mfurahisha angefanyiwa na raisi angekuja kumtukana hapa kama Mama Siti Mwinyi alivyo mtuhumu kwa lugha ya kejeli?

Kuna mengi sana amekosoa huku kwa awamu iliyopita kisha anarudi kulaumu awamu nyingine haijayafanya. We call it contradiction.

Na kama alitaka yafanyike lakini kwa kiasi fulani basi angalisema wazi kiwango kipi. Atuwekee kipimo chake na kwa sababu zipi.

Nikipata muda nitakuja kumchambua kila hoja aliyojipinga mwenyewe. Zipo hoja zaidi ya tatu amejichanganya kiasi unaona huyu hakijui anachotaka na asichotaka.

Point ni simple, kama mtu kashindwa ku take care ya familia yake, je ataweza taifa?
 
Back
Top Bottom