PreGE2025 Ujenzi wa kiwanja cha ndege Shinyanga wafikia asilimia 75 ukitarajiwa kukamilika Juni 10, 2025

PreGE2025 Ujenzi wa kiwanja cha ndege Shinyanga wafikia asilimia 75 ukitarajiwa kukamilika Juni 10, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dk Charles Msonde amesema ujenzi wa kiwanja cha ndege Shinyanga umefikia asilimia 75 na utakamilika Juni 10, mwaka huu.

Amesema kukamilika kwake kutawezesha ndege aina ya Bombadier Q400 kuanza kukitumia kiwanja hicho chenye urefu wa mita 2200 na upana wa mita 30 kilichogharimu Sh48.5 bilioni.

Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Akizungumza leo Machi 20, 2025 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma (PIC), iliyokagua maendeleo ya ujenzi huo, Dk Msonde amesema njia za kuruka na kutua ndege, maegesho na barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani zimekamilika.

"Kilichobaki ni jengo la abiria ambalo ujenzi wake upo kwenye hatua ya mwisho kukamilika," amesema.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustine Vuma Holle ameiagiza wizara ya ujenzi kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.

Amesema hatua ambayo umefikia ni nzuri, akiipongeza wizara ya ujenzi na Wakala wa Barabara (Tanroads), kwa kazi nzuri na kuwahimiza kumsimamia mkandarasi ili asilimia 25 iliyobaki ikamilike kwa wakati na huduma kiwanjani hapo zianze.
 
Back
Top Bottom