Ujenzi wa "flats" 20 za ghorofa nne kwa Tshs bilioni 10, kila flat ni Tshs milioni 500. Twende kazi!

Mm sina nia mbaya lkn hivi wanaohusika ktk hiyo kazi hakuna ma engeneer wanaojua zaidi yako hadi wameshindwa ku realize vitu kama hivyo au kuna kitu gani ? Mbona nahisi na ww utakuwa upande wa siasa tena upande wa wale wanaokosoa kila kitu ? Any way ngoja tusubiri utakachotuletea kama evidence
Engineers wa serikali unawajua kweli? Kumbuka ndo wanaoongoza kwa utendaji wa chini ya kiwango. Wengi wa wahandisi pale TBA tunawafahamu na wengine tumesoma nao tunaujua uwezo wao! Natamani ungekuwa na uelewa kuhusu haya mambo pengine ungejiweka pazuri kutokana na mashaka yako!
 
Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu
Nyumba ya 15m? hicho ni kibanda, umeezekea mabati ya sh ngapi na mangapi.

Gharama ya kiwanja hui hesabu, mafundi...sidhani kama ni kweli.
 
Mtu yoyote akitaka kwenda kukagua anaruhusiwa?
Ndugu zangu kusema ukweli jengo ka kipindi hiki ambalo inabidi waishi wanafunzi kwa milioni 500 ninawasiwasi sana. Maana tuchukuliwe mtu anayejenga nyumba ndogo ya ghorofa moja yenye vyumba kama vinne anaweza kweli kuimaliza kwa milioni 100?

Ujenzi wa majengo makubwa umebadili sana hasa ukizingatia tahadhari kubwa inabidi ichukuliwe kwa sababu wanaishi watu wengi kwa wakati mmoja. Nina wasiwasi sana na ubora wa hayo majengo.
 
Hiyo nayo umepigwa mkuu. Unless unaudanganya Uma wa Jf. Just a normal residential apartment haiwezi gharimu 350m. Am a construction expert tena wa muda sana
Mkuu, kwa Dar bei ya kiwanja tu kama huna 50-100m hujapata labda vile vya hatua 20x20 unsurveyed plots ambazo hata nyumba ya vyumba 2 ngumu kujenga.
 
Mimi naisubiri taarifa ya mtoa mad, G Sam ndio nita comment. Mainjina mnatuchanganya hapa maana mnaona mnaharibiwa dili. Wengine ndio mko kwenye mchakato wa kusaini dili na kupiga, sasa taarifa ya aina hii ni chungu. Lazima mtu atukanwe hapa.
 
Hivi Tanzania kuna mtu anaweza simama na kujiita Engineer kweli, Pale Coet Udsm mnasoma theory tu hakuna kitu pale, Sijajua huko DIT na Mbeya, Kuna Engineer Coet kweli au wale maprofesa uchwara
unakuta mtu kama wewe hata certificate ya engineering huna!
Ila kukosoa ndo unajua
 
Tuna waandishi waaminifu pale Mlimani wanajua ubora wa ujenzi ktk viwango vya kitaifa na kimataifa. Na wapo site kila siku na hayo ni majengo yao
Waandishi wanahusikaje kwenye ujenzi?
 
Kwanza naomba kuweka wazi kuwa mimi ni Engineer na nimeshiriki miradi kadhaa ya ujenzi katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania...

Hata ukinichinja nipo tayari kuliko kuamini kuwa pale UDSM flat moja ya ghorofa nne imegharimu Tshs milioni 500 hadi kukamilika!

Wakuu, naahidi kuwa hii thread nitai-update baada ya kutembelea ujenzi wa UDSM hapo jumanne wiki ijayo. Naahidi kuwa nitadadavua kila kitu na mwisho tukubaline kuwa kama ni sahihi kudanganywa kuwa kila block imegharimu Tshs 500 milioni mpaka kukamilika. Nitakagua ubora wa jengo na nitaweka humu kila kitu! Mods naomba mnilindie thread yangu.
Engineer "umekurupuka" kuweka bandiko hili.

Engineer huhitaji kuapiza ili bandiko lako liaminike.

Engineer, kwa taaluma yako, ungejenga hoja kwa takwimu km BOQ kuthibitisha gharama za hayo majengo, na siyo ahadi yako ya "Nitakagua ubora wa jengo na nitaweka humu kila kitu!". Unakwenda kukagua nini sasa!

Engineer, ujenzi unaendelea, ulikuwa wapi muda wote, kutoa ushauri uliomo kwenye bandiko lako!
 
Mkuu, kwa Dar bei ya kiwanja tu kama huna 50-100m hujapata labda vile vya hatua 20x20 unsurveyed plots ambazo hata nyumba ya vyumba 2 ngumu kujenga.
Unazungumzia viwanja vya wapi hivyo mkuu? Maana hata mbweni vya 25-30m vipo. Au unazungumzia dar IPI mkuu? Kwa bei hizo za 50-100m sisi wengine tungejenga mjini kweli.?

Mbona kama unajaribu kuwakatisha tamaa vijana waogope kujenga mjini? Hivi (30x30m x 8'000) mbona hata million kumi haifiki?
 
Gulwa!mbona unaonyesha udhaifu wa kutokujiamini?.kwa taarifa yako wajanja atujengi Nyumba wewe,haswa sisi Waafrika wajanja tunapangisha tuu , nakupa akili hii . Ukitaka familia yako siku ukifa isiparanganyike usiache nyumba au mali. Wewe Mungu akikijalia somesha watoto wako wapate Elimu vya kutosha , ukiondoka unaondoka ukiwa umewapa Ufunguo wa maisha watoto wako ambayo ni Elimu sio Kuwaachia funguo ya Nyumba , maana mwisho wa siku hili kukuridhishia hilo Nyumba itauzwa , watoto watagombana na hata kuana au kurogana,.Acha kuogopa maisha.
Mkuu tunajenga kwa sababu hakuna social security, uzeeni itakuwa taabu, tafakari kidogo
 
Kwanza naomba kuweka wazi kuwa mimi ni Engineer na nimeshiriki miradi kadhaa ya ujenzi katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania.

Nimejikuta nikitamani sana kwenda kuukagua ujenzi unaoendelea pale UDSM ambao ni (typical lay out) ya flats 20 huku kila flat ikiwa na ghorofa nne. Kwa mantiki ya "typical lay out ina maana kila flat imegharamiwa sawa, hii ni kusema kuwa kila flat imegharamiwa kwa Tshs milioni 500?

Ikumbukwe kuwa TBA ni consultant tu ambaye inamlazimu kutafuta main contractor na huyo main contractor ambaye ni mjenzi pia atafute sub contractors kwenye upande wa plumbing na electrical. TBA amejithibitisha mbele ya rais Magufuli kuwa tender document ya contractor pamoja na subs aliowatafuta haikufika Tshs bilioni 10 kwa flats zote maana na yeye ni lazima kwenye hiyo bilioni 10 apeleke wakaguzi site na vikao vya kila muda kwa mujibu wa taratibu pia ni lazima abaki na akiba kama mfanyakazi anayetakiwa kuendesha ofisi. Any way swala la usafiri limeepukwa kwa kuwa mradi upo kilomita chache tu kutoka zilipo ofisi za TBA.

Sasa kweli kila flat imegharimu Tshs milioni 500 kwa kila kitu? Building structure + mechanical, plumbing + electrical installations? Ubora wa jengo?

Kwenye mambo ya ujenzi kama haya huwa kuna kitu tunaita "additional works" yaani kutokana na mabadiliko ya bei za vifaa, kukosea kwenye quotation, kuongezeka vitu vya ziada inamlazimu mkandarasi kuandika "claim" ya kuomba fedha zaidi kutokana na hilo.

Pengine huu mradi wa Tshs milioni 500 kwa kila flat una "claims" kibao za additional works ila tutakuja kuambiwa kuwa zimetumika tu Tshs milioni 500 kwa kila flat. Nani atakagua? Mchakato wa ujenzi na taratibu zilifuatwa?

Hata ukinichinja nipo tayari kuliko kuamini kuwa pale UDSM flat moja ya ghorofa nne imegharimu Tshs milioni 500 hadi kukamilika!

Wakuu, naahidi kuwa hii thread nitai-update baada ya kutembelea ujenzi wa UDSM hapo jumanne wiki ijayo. Naahidi kuwa nitadadavua kila kitu na mwisho tukubaline kuwa kama ni sahihi kudanganywa kuwa kila block imegharimu Tshs 500 milioni mpaka kukamilika. Nitakagua ubora wa jengo na nitaweka humu kila kitu! Mods naomba mnilindie thread yangu.
Nimejenga flat moja kwa million 80 huu mwaka wa 4 na dunda tu hebu tuwe na subira kwanza tuone
 
Back
Top Bottom