Ujenzi unaoendelea jangwani hauna athari zozote kwa mazingira? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi unaoendelea jangwani hauna athari zozote kwa mazingira?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mesaka, Sep 13, 2012.

 1. M

  Mesaka Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ndugu wana jamii,

  Kila ninapopita jangwani nashindwa kupata majibu ya maswali yanayo zunguka kichwani mwangu. Je huu ujenzi unaoendelea hapa hauna madhara yoyote kwa mazingira? na je wanamazingira (NEMC) wameshafanya Enviromental impact assessment? kama wamefanya wameshauri nini? na je, hakutakuwa na madhara yoyote baadaye?

  Maswali haya yanatokana na uzoefu wa yaliyotokea Desemba 2011 na mpaka serikali kutoa agizo la kuwahamisha wote walijenga na kuishi kwenye bonde la mto Msimbazi.

  Kwa uelewa wangu mafuriko ya mwaka jana yalikuwa na madhara sana kwa sababu maji yaliyotokana na mvua kubwa ya kihistoria iliyonyesha Dar nzima, na wakati maji yalishindwa kuingia baharini kwa sababu wakati huo bahari ilikuwa imejaa (high rise), hivyo kusababisha maji kjaa sana kwenye bonde hilo. Mafuriko yalianza kupungua baada ya bahari kupwa kwani hapo maji yaliweza kuingia baharini.

  Hivyo kwa uzoefu na uelewa huo naona kwa kuendelea kulijenga bonde hilo, maana yake bonde linapungua ukubwa hivyo maji kushindwa sehemu ya kupumulia kwani naamini bonde hilo ni sehemu ya kupumulia bahari ya hindi wakati wa sea rise.

  Mapendekezo yangu bonde hilo lingeweza kutengenezwa mfereji mkubwa mpaka gongola mboto, ambapo ingeweza kuwa njia meli ndogo au boti, ambazo zingefanya safari kati ya gongo la moto na posta pia mpaka tegata hata bagamoyo.

  Kwa hayo machache pamoja na kwamba ujenzi unaendelea, naomba wana jamii mliangalie kiundani zaidi. NAWASILISHA.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unachanganya madhara ya mazingira na maafa ya watu ya kujitakia, jangwani na mabondeni miaka nenda miaka rudi watu wanaambiwa wasiishi huko hawasikii wala hawataki kuelewa.

  Madhara kwa watu yakitaka kutokea hata Japan na uwezo wao hawawezi kuyazuia wala NEMC hawana uwezo huo.

  Mazingira hutazamwa athari zake kabla ya mradi na hufanywa mapendekezo ya nini kifanyike ili kupunguza athari za kuharibu mazingira kwa muda mrefu na mfupi, Hili limefanyika.
   
Loading...