Ujenzi: Nondo vs Flat bar Grills

Safi sana! Naamini hapo mambo mengine ya idara hiyo tudndelee kujulishana
 
Dirisha la 150*150 nondo ni 100,000-120,000 wakati size hio hio flat bar ni 150,000+
Kaulize bei ya flat bar na nondo urefu sawa ulete mrejesho.

Nondo bei ghali sana
 
Dirisha la 150*150 nondo ni 100,000-120,000 wakati size hio hio flat bar ni 150,000+
Kaulize bei ya flat bar na nondo urefu sawa ulete mrejesho.
Duh basi nimepigwa mkuu nimetumia nondo dirisha za futi saba kwa saba gharama nimepewa laki 7 na selathini kwa dirisha...pamoja na kupachika...
 
Duh basi nimepigwa mkuu nimetumia nondo dirisha za futi saba kwa saba gharama nimepewa laki 7 na selathini kwa dirisha...pamoja na kupachika...
Umepigwa...ninalo moja urefu sahihi sikumbuki ila ni floor to ceiling upana futi nne hilo nimelipia kama 270,000 tu! Kupachika dirisha moja 5,000-10,000.
 
Huwa wezi wanakuwa na kifaa fulani wanachotumia mafundi kukunjia flat bars na hizo nondo, its so easy my brother. Hasa hizo nondo zinazounganishwa kwa kuchomelea ni rahisi sana kuzikata.

Kwa mwizi hakuna linashoshindikana.
Sio rahisi kama flat bars. Ndio point. Hata milango ya jela inavunjwa.
 
Hapa nalinganisha flat bars na nondo. Sisemi kuwa nondo wezi hawawezi kuvunja.
Mzee wa european cars kwema! ni ukweli mtupu flat bar wezi wanazikata kirahisi mnoooo, ila kuna nondo fulani hivi aisee mwizi atafanya kazi kubwa mnoooooooooo kuzikata! shida wabongo huwa tuna haraka ya kuhamia na kuachana na kupanga na ukiongeza na pressure za wanawake ndo kabsaaaa matokeo yake ndo hayo ya kuweka viflat bar ambavyo navyo vinakuwa supported na visquare pipe dhaifu why mwizi asivikate?? kisa bei rahiso Ila kingine wananchi tu watu wa hovyo sana kwa baadhi ya maeneo, mathalani unamkuta mtu/watu hatutaki kuchangia mathalani elfu 30-50 ya ulinzi shirikishi kwa mwezi kwa vijana ambao wako tayari kufanya ulinzi, ila tupo tayari kutumia laki kadhaa up to millions kurejesha vifaa vya gari ambavyo mwizi ameiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…