Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Najipongeza kwakweli maana 60% nimeikamilisha...nikashaezeka naingia mambo mengne yatanikuta humohumo
Hongera sana mkuu ila 60% bado ukipaua na kuchimba shimo la choo unaweza jipa asilimia hizo. Kumbuka 100% ina include fence/ukuta na pavings chini.
 
Kujenga kusikieni tu
Ni shughuli pevu kwakweli
Hasa unapofikia ktk kupaua...kupau kunahitaji fedha sana...kupaua hakuna kulaza ukichokoza ndo mpka umalize tofauti na kupandisha boma unaweza kujenga koz 5 ukaacha kwanza...kupaua lazma mbao ziwepo za kutosha,bati za kutosha,misumali,na fedha ya fundi muda huohuo...
Kwakweli mwenye nyumba aheshimiwe!!!
Hapa kichwa kinakokotoa hesabu namna ya kupata bajet ya kuuzeka majengo wangu..moja haikai mbili haikaiView attachment 1504003
Hongera mkuu.

Hii nyumba ina room ngapi?
 
Me naomba msaada kwa mwenyewe raman nzuri anitumie walau nianze taratibu kupiga hatua.
Natanguliza shukrani
 
Why? Standard kabsa nyumba inatakiwa kuwa ya vyumba vinne. Chako,Cha boys( kitanda bouble decker) na girls( kitanda double decker) nacha wageni( Mimi ninae baba yangu namuuguza nyumbani kwangu leo mwaka wa pili) Nina watoto wanne binti wa kwanza yupo form two shule ya bweni,wanafata mapacha wa kike na kiume wako darasa la tatu Wana miaka tisa anafuata kitinda mimba wa kike ana miaka miwili na nusu. Kijana wa kiume ana chumba chake( kitanda double decker)pacha wake wa kike ana share chumba na mfanyakazi pamoja na shangazi yangu( kitanda double decker na single kitanda kimoja) ambaye kazi yake ni kushugulika na kumtunza baba yangu basiii( chakula,kumfulia) alifiwa mme na ni mtu mzima kiasi. NIKO COMFORTABLE NA FAMILIA....nikipata mgeni wa kiume anaenda kulala na kijana wangu wa kiume nikipata mgeni wa kike anaenda chumba cha wasichana. Baba yangu analala peke yake mpaka watoto wanakiita chumba cha babu...nilifiwa na mama yangu mzazi Oct 2015. SIJAWAHI KUTEMBELEWA NA MGENI AKAJA NA MKEWE AU MMEWE. Na sijui wakija nitawalazaje.

Hii imekaa vizuri, mi nafikiriaga vyumba vitatu tu. Ila kwa maelezo yako naona ni reasonable sana kujenga vyumba vinne
 
Big up sana mkuu. Umepambana kiume.
Yah mkuu MUNDENDE alimradi tuna pumzi na hela tunazitafuta bora tufanye mambo ya msingi kama haya,maisha yanakuwaga very tough kama mtu unagonga 50 halafu bado unapanga mabanda ya uwani kwenye nyumba za wazee wenzako.
 
Una maneno mengi sana mdomoni, mi nimeuliza swali dogo tu...ila majibu jaji wewe, hakimu wewe, wakili wewe!

Utakuwa ni muongo sana afu njaa kali mkuu

Kuna mtu hana njaaa wewe....mie kweli njaa kali ndio maana nataka kuwekeza ili uzeeni nirelax na warembo tunagegedana.

Wee kama unauza njoo tupange mambo
 
Yah mkuu MUNDENDE alimradi tuna pumzi na hela tunazitafuta bora tufanye mambo ya msingi kama haya,maisha yanakuwaga very tough kama mtu unagonga 50 halafu bado unapanga mabanda ya uwani kwenye nyumba za wazee wenzako.
Point kabisa mkuu, tupambane vyovyote ila at 40yrs ni muhimu mtu kuwa kwako. Ukichelewa unaeza jikuta baba mwenye nyumba wako ana umri sawa na mwanao hakupi shikamoo.
 
Hongera sana mkuu ila 60% bado ukipaua na kuchimba shimo la choo unaweza jipa asilimia hizo. Kumbuka 100% ina include fence/ukuta na pavings chini.
Hizo fence na paving si muhimu sana..hazina ulazma kuna vitu vya ulazma kama milango,madirisha na choo!
 
Ni kweli mkuu ukijenga nyumba ya vyumba vitatu ni standard kwa familia hadi utapumzika kwa miaka mingi bila kuwaza ujenzi mwingine.
Ila ya vyumba viwili baada ya miaka 5 mbele utaanza kuwalaza sebuleni baadhi ya watoto ambayo itakupa stress tena.
ila ya vyumba vitatu umemaliza maana unakuwa na chumba master chako mwenyewe na mkeo,chumba cha watoto wa kike,chumba cha watoto wa kiume.
Mgeni akija kama ni wa kiume atajimix na watoto wa kiume,na kama ni wa kike atajimix na watoto wa kike akiona kero baada ya wiki ataaga aondoke zake
Ni wazo zuri ila usipende kuchanganya wanao na wageni ,ni hatari pia maana atuzifaham tabia za wageni japo ni ndugu zetu
 
Kwa wakazi wengi wa mjini kuna jambo moja ambalo limekuwa kizungumkuti sana kwa watu wengi hasa sisi wa uchumi mdogo.

Hakuna mtu anayependa kuishi kwenye Nyumba za kupanga hivyo kila mtu anapenda kujenga awe na kwake, mahala ambapo atakuwa huru kufanya anavyotaka yeye.

Nimefanya uchunguzi ni kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao.

1. Watu wengi wanaogopa kujenga, yaani mtu anakuwa anasubiri awe na pesa nyingi ndio aanze ujenzi.
Mara nyingi kadiri mtu umri unavyoongezeka na majukumu nayo huongezeka hivyo kipato hakitaruhusu uwe na pesa nyingi

2. Watu wanatamani vitu ambavyo hawana uwezo navyo. Jirani yangu kuna mama alipata pesa yake kiasi akaamua kwenda kuanza ujenzi kwenye kiwanja chake, pasipo kufanya tathmini ya uchumi wake alianzisha msingi wa jumba kubwa kiasi kwamba pesa aliyokuwa nayo yote iliishia kwenye msingi.

Mpaka sasa anajikongoja lakini kutokana na ukubwa wa nyumba basi imesogea mpaka kwenye madirisha ndani ya miaka kama mitano sasa. Lakini ukipiga hesabu vizuri ni kwamba pesa aliyokwisha tumia angeweza kujenga nyumba ndogo angalau ya vyumba viwili na sebule na leo angekuwa anaishi kwake.

So tukadirie haya mambo
Hoja yako iko wapi hapo. watu wamesogea kwenye vibanda vyao lakini pesa hata ya kuweka bandalling wanashindwa 5 yrs
 
Nilikuwa nawaza sana suala la ujenzi. Nikishaenda kwa architecture akanichorea ramani moja tamu sana ila nilipopiga hesabu nikagundua ile nyumba ili niikamilisha basi itanipasa kupambana na kuitesekea sio chini ya miaka 10.

Basi nikaona isiwe kesi nikamchukua fundi tukaenda site last week tukapima nikamwambia aniwekee kijumba changu cha room 2 na sebule tu.

Leo hii nafunga lenta na wala haijaniumiza sana kiasi hata cha kuathiri biashara zangu. Na finishing pia sioni hata dalili ya kuja kunitesa na nina uhakika Mungu akipenda basi nitaikamilisha hata ndani ya mwaka huu
bado unasafari nzito. nyumba kueka bati ikiwa na madirisha wazi na milango hapo kasheshe itaanzia hapo, wakuu nashindwa hata kupaka madirisha rangi nyeusi bado ina ile ya kwanza. ivi niikiiacha vile vile kuna matatizo?

watu tunaposhauriana kuhamia hatuambiani kwamba tutafute mafundi wa aina gani na plasta ya mchanga wa aina gani, na cement ili mtu usiteseke unangia ndani ya nyumb plasta mbya, fundi mchafu, sio msafi hata kidogo, fundi ataanza kukuambia najua kufanya kila kitu. maanina, ukianza na fundi kwa mkataba fulani hakikisha huendelei naye hatua nyingine tafuta mzoefu, wanaharibu kazi
 
Ni kweli, ujenzi siyo lelemama, kila mtu ajenge kulingana na kipato chake, Kama unaona hali ya kiuchumi siyo nzuri, jenga nyumba ndogo utakayoimaliza kwa wakati, usijilinganishe na watu wengine, waache wajenge majumba yao makubwa, uwezo wao ni mkubwa pia.
Binafsi nimejenga nyumba yangu kwa miaka sita, nilianza kuweka msingi wa nyumba yote, baada ya muda kidogo nikasimamisha vyumba viwili na kupaua,nikahamia. Nikiwa naishi humo ujenzi ukaendelea, ni miaka kadhaa imepita Sasa baada ya nyumba hiyo kukamilika. Lakini baada ya mambo kukaa vizuri nyumba nyingine nilianza ujenzi mwanzo mwisho. Mleta mada hongera kwa uzi huu.
 
Mkuu kwa nyumba hiyo umetumia kiasi gani mpaka kuimaliza?
Mkuu haijamalizika yote maana hatu huu upande mwingine bado Sijapauwa imefika kwenye linta ,Hivyo wiviwili master imenilila kama 7 hivi na kuweka magetini na kuchimba choo .
Napia bati ilinibidi hivi viwili kupiga gaji 28 kutokana na aina ya uwezekaji wa hiden roof sijui ndo mnavyoita ,kwahiyo ili nicoat sana
 
Me naomba msaada kwa mwenyewe raman nzuri anitumie walau nianze taratibu kupiga hatua.
Natanguliza shukrani
Nakushauri ili upate ramani nzuri andaa japo laki mbili ufike na mchoraji site aangalie site yako ilivyo umpe mahitaji yako akuchoree kitaalamu nyumba ya chaguo lako. Kuliko kutumia ramani za watu.
 
Jinsi ya kupunguza gharama za gypsum board.
Piga hesabu unahitaji boards ngapi. Mfano unahitaji 50pcs. Nunua 20pcs kwanza. Mwambie fundi aweke nzima nzima,yaani aweke sehemu zinazoingia nzima nzima nyumba nzima. Zile sehemu zinazohitaji vipande aziache kwanza.
Utashangaa nzima zinaingia 20 au pungufu.
Zile sehemu zinazohitaji vipande nenda hardware ongea nao wakuuzie damaged boards(hizi huwa zinakuwa zimemeguka kidogo wakati wa kumshusha mzigo hawawezi kuuza kwa wateja wa kawaida) hizo utauziwa moja 5000-7000. Unanunua kama 30pcs ndio unaenda kuweka sehemu zinazohitaji vipande.
Hesabu iko hivi
Boards nzima 50 ni 50*14,000=700,000
Kwa njia hii nilioshauri
Board nzima 20 ni 20*14,000=280,000
Damaged board 30*6000=180,000
Total 460,000
700,000-460,000=240,000
Umeokoa 240,000.
We ndugu yangu unatumia akili sana kwenye ujenzi, unawaza kimkakati sana @PRONDO hapo utaokoa gharama kubwa sana sana kwa kutumia njia hiyo ya kweka nzima then the rest unatafuta hizo, zangu ziliingia pc 61 gypsum bodi na mikanda na screw iligonga laki 8, ningetumia hiyo njia ingenisaidia sana na ningeokoa hela na hela ya mafundi ingepatikana hapo hapo
 
Back
Top Bottom