Reagan Carima
Member
- May 20, 2015
- 44
- 194
Kwa wakazi wengi wa mjini kuna jambo moja ambalo limekuwa kizungumkuti sana kwa watu wengi hasa sisi wa uchumi mdogo.
Hakuna mtu anayependa kuishi kwenye Nyumba za kupanga hivyo kila mtu anapenda kujenga awe na kwake, mahala ambapo atakuwa huru kufanya anavyotaka yeye.
Nimefanya uchunguzi ni kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao.
1. Watu wengi wanaogopa kujenga, yaani mtu anakuwa anasubiri awe na pesa nyingi ndio aanze ujenzi.
Mara nyingi kadiri mtu umri unavyoongezeka na majukumu nayo huongezeka hivyo kipato hakitaruhusu uwe na pesa nyingi
2. Watu wanatamani vitu ambavyo hawana uwezo navyo. Jirani yangu kuna mama alipata pesa yake kiasi akaamua kwenda kuanza ujenzi kwenye kiwanja chake, pasipo kufanya tathmini ya uchumi wake alianzisha msingi wa jumba kubwa kiasi kwamba pesa aliyokuwa nayo yote iliishia kwenye msingi.
Mpaka sasa anajikongoja lakini kutokana na ukubwa wa nyumba basi imesogea mpaka kwenye madirisha ndani ya miaka kama mitano sasa. Lakini ukipiga hesabu vizuri ni kwamba pesa aliyokwisha tumia angeweza kujenga nyumba ndogo angalau ya vyumba viwili na sebule na leo angekuwa anaishi kwake.
So tukadirie haya mambo