Mbayo wa Giika
JF-Expert Member
- Apr 9, 2014
- 205
- 107
Wadau wa ujenzi naombeni msaada wenu. Eneo ninalotaka kujenga lina chumvi nyingi inakula kuta na tofali, nifanyeje kuizuia? Ahsanteni!
Pole kwa changamoto
1. Fahamu chanzo cha chumvi ni kipi ili upate the right course of action for the problem. Mfano chumvi ambayo iko juu juu kabisa kama kule Ununio, DSM treatment yake ni extreme manake uta-deal na foundation, jamvi mpaka kuta na paa ila kama source ni unyevunyevu kutoka deep soil basi unaweza weka tu damp-proof -membrane+ course, yani nailoni kwenye jamvi+ tofali ili kuzuia unyevunyevu usipande juu.
2. Chumvi haitembei yenyewe, mobility ya chumvi is by water. Sasa hoja ni kuzuia aina tatu tuseme za upenyezi wa maji na chumvi
3. Vya kuzingatia wakati unajenga
- Maji yanayotembea zaidi tuseme kwenye site mfano mabomba yaliyopasuka, mvua, sewer spoilt drainages etc sbb yatapeleka chumvi paka kwenye nyumba/fence etc.
- Rate of evaporation, hapa unyevunyevu husababisha chumvi kutembea kwa mfano hadi kwenye ukuta wa nyumba, so exposed surfaces should be far from the evaporation process.
- Matundu yanaruhusu chumvi kupita. Mfano ukuta ukiwa wa matofali ya kawaida manake joints za tofali ziko likely kupitisha chumvi ukilinganisha kama ungejenga na zege.
Nimejaribu kuwa general.
- Itumike damp proof membrane. ni nailoni ambayo unailaza kabla ya kumwaga zege la jamvi baada ya kupanga matofali. inafunika eneo lote la nyumba
- Tumia damp proof course, ni mkanda wa nailoni ambao huwekwa chini ya tofali la kwanza baada ya jamvi la zege.hii inawekwa mzunguko wote wa matofali
- Hakikisha movement ya maji kwenye site imepangiliwa yani water drainage, sio mvua ikinyesha, ukute kumejaa pavement so maji yote yanasimama na yanaelekea kwenye nyumba.
- Kutoa eneo kubwa la udongo na ku replace na mwingine "cut and fill"
- Kutengeneza mteremko wa site tofauti na nyumba
- Uangalifu wa landscaping na umwagiliaji wa hiyo landscape
- Pia treatment za materials mbali mbali zinatofautiana kama ni tofali la cement-sand, ni concrete, ni bricks etc.
Nakushauri watafute wataalum kabla hujafanya chochote.